Thursday, March 14, 2013

PAPA MPYA FRANCIS 1 AMEANZA KAZI


Papa mpya Francis Vatican

   

....akiwa pungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake
 
Kazi ya kuchaguwa wasaidizi…
 
Papa Francis I (katikati) akiwa na Kardinali Santos Abril wa Hispania (kushoto) na Kardinali Agostino Vallini ambaye pia ni Kasisi Mkuu (Vicar General) wa Roma (kulia) wakiupungia umati leo asubuhi.
 

Papa Francis I akihutubia kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa.
 
....akiwapungia mkono waumini waliofika eneo hilo wakati wa kutangazwa kwake.
Siku yake ya kwanza ofisini kama Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza kazi. Papa anatarajiwa kuwateua
wafanyakazi wakuu watakaohudumu katika Vatican chini ya uongozi wake. Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika hekalu ya mtakatifu Maria Maggiore mjini Rome. Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya Papa Francis, utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi uliozongwa na kashfa nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua kwa kanisa hilo.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama papa. Hata hivyo yeye mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1, siku ya Jumanne.
Chanzo: BBC SWAHILI

Timuatimua yawakera wanafunzi vyuo vikuu

RAIS Jakaya Kikwete ameombwa kuchukulia kwa uzito vitendo vya timuatimua wanafunzi katika vyuo vikuu vya umma kutokana na wanafunzi hao kudai haki wanazopaswa kuzipata wawapo vyuoni.
Msemaji wa Umoja wa  Wanafunzi waliofukuzwa  katika Vyuo Vikuu nchini (UUEST), Philipo Mwakibingwa, alitoa kauli hiyo jana wakati wa uzinduzi wa umoja huo na kusema kuwa lengo kubwa la umoja huo ni kutetea wanafunzi waliofukuzwa.
Alisema tangu miaka ya 2000 hadi sasa, suala hilo limezidi kukua nchini, watawala wa vyuo vikuu ambao ni maprofesa na baadhi ya viongozi waliopo serikalini kulichukulia kama mila na desturi.

Mwakibingwa alisema wanafunzi hao wamekuwa wakifukuzwa kutokana na kutoa mawazo mbadala, kuhoji mambo, kukosoa uovu uliopo na unaondelea kutendeka ndani ya vyuo, hivyo na kutoa ushauri pale inapobidi kwa masilahi ya taifa lao.

Akizungumzia umoja huo, alisema wamefikia hatua ya kuunda umoja huo kutokana na serikali pamoja na Bunge kushindwa kutatua matatizo yao na kuongeza kuwa hali hiyo imesababishwa na taarifa potofu zilizotolewa na watawala wa vyuo vikuu hivyo.

“Kwa sababu watawala wa vyuo vikuu wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kututenganisha na jamii zetu, familia zetu, jamaa, viongozi wetu wa kidini na asasi kwa taarifa za uongo kupitia vyombo vya habari, tumeona suluhu ya maisha yetu ni kuungana. Muungano huu umeundwa kwa ajili ya kutetea maisha yetu,” alisema Mwakibingwa.

CHADEMA yalisulubu Bunge

WANASHERIA wameunga mkono msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wale wa NCCR- Mageuzi kupinga hatua ya Ofisi ya Bunge kuliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wabunge wake ili wakahojiwe.
 Wakizungumza mwanasheria mashuhuri hapa nchini na wakili wa kujitegemea, Mathew Kakamba, alisema ni kinyume cha sheria na ni matumizi mabaya ya madaraka kwa Ofisi ya Bunge kutumia polisi kuwakamata wabunge katika masuala yanayolihusu Bunge.

Wanasheria hao walitoa maoni yao kuhusiana na mvutano mkubwa wa kisheria uliozuka baina ya CHADEMA na Ofisi ya Bunge ambayo imeagiza kukamatwa kwa wabunge kadhaa wa upinzani ili wakahojiwe na Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, ambayo CHADEMA wanadai kuwa haipo.

Wakili Kakamba katika maoni yake alisema ni makosa kisheria kutumia nguvu za mhimili mwingine katika kuendesha masuala yanayohusu mhimili wa pili.

“Kuna mgogoro unaojulikana kwa  Watanzania karibu wote kuhusiana na vurugu zilizotokea katika mkutano wa Bunge lililokwisha, na kuvunjwa kwa kamati za kudumu za Bunge.

“Pamoja na kuvunjwa kwa kamati hizo, bado kama sikosei, wajumbe wake hawajateuliwa na kwa maana hiyo, kisheria utendaji wake haujaanza. Kwa lugha nyingine, haziwezi kuitwa kamati rasmi kwa sababu hazina wajumbe,” alisema Wakili Kakamba.
Kauli ya Wakili Kakamba imeungwa mkono na wakili mwingine, Aloyce Komba, ambaye  amekiita kitendo cha Ofisi ya Bunge kutumia polisi kuwakamata wabunge wao wa upinzani kuwa ni udhalilishaji mkubwa na uvunjaji wa haki za binadamu.

Komba anayetoka Kampuni ya Uwakili ya Haki Kwanza, alisema Bunge ni chombo kinachojitegemea na linazo sheria na kanuni zinazopaswa kutumika kumlazimisha mbunge kutimiza agizo la wito.

“Masuala yote ya Bunge yanatakiwa kuendeshwa kibunge bila kutegemea vyombo vingine vya nje, labda tu ikiwa kuna mwingiliano kutoka katika mhimili mwingine.
“Si sahihi kwa spika kutumia polisi kuwakamata wabunge wakati wanazo kanuni na taratibu nzuri tu, na sidhani kama ni utaratibu mzuri na unaolenga kudumisha demokrasia.
“Mbunge akishindwa kufika, kwani hakuna sheria nyingine hata za kuzuiwa kuhudhuria vikao kadhaa vya Bunge, hadi leo wanataka kutumia polisi kuwakamata?” alihoji Komba.

Akizungumzia uhalali wa kamati hizo, Komba ambaye ni mtaalamu wa sheria katika mambo ya utawala, alisema kimsingi hazipo, kwa sababu tangu kuvunjwa kwake na kuundwa nyingine, bado spika hajateua wajumbe wa kamati mpya.
“Hajateua wajumbe wa kamati hizo, na ni sawa kabisa kuwa hazipo. Sasa wanaitwa kuhojiwa na kamati gani? Mtazamo wa kisheria ni kwamba hazipo.

Alikwenda mbali zaidi na kuilaumu Ofisi ya Bunge kwa madai ya kuvunja haki za msingi kwa sababu aliyetendewa kosa ni spika (kiti), anayelalamika ni spika, mteuzi wa kamati ni spika na ushahidi mwingi utatoka kwa spika, hivyo kupingana kabisa na haki za sheria ambazo mlalamikaji hapaswi tena kuwa mwendesha mashitaka.
Hata hivyo, mawakili hao walikubaliana na kuwataka wabunge wote waliopata barua za wito kutoka Ofisi ya Bunge kuitikia na si kukaidi.
“Pamoja na kasoro hizo, kama wameitwa na Ofisi ya Bunge, wanatakiwa kwenda na si kugoma. Huko ndiko mahali pekee wanakotakiwa kuwakosoa hao wakubwa, na hata wanao uwezo wa kukataa kuzungumza hata kama kamati yenyewe ingekuwa hai kisheria,” walisema wanasheria hao.

CHADEMA wagoma
Juzi  Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alimwagiza Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni kuiandikia barua Ofisi ya Bunge ya kukataa wabunge wake kukamatwa na polisi ama kuhojiwa na kamati waliyodai ni hewa, kwa kuwa zilizokuwapo zilivunjwa na Spika Anne Makinda katika kikao kilichoisha mwezi uliopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kisheria, kanuni na taratibu za Bunge, kamati ambazo zimeshavunjwa haziwezi kufanya kazi yoyote kwa kuwa ni batili mpaka hapo zitakapoundwa kamati nyingine.

Alilitaka Bunge kurejea kanuni za kudumu za Bunge namba 113 (7), inayozungumzia ukomo wa uhai wa kamati za Bunge, uhai wake unaishia Mkutano wa Kumi wa Bunge ambapo inakuwa ni nusu ya kwanza ya uhai wa Bunge lenyewe.
Dk. Slaa alisema kutokana na kifungu hicho, inaonesha dhahiri kwamba Spika Anne Makinda na wasaidizi wake wana matumizi mabaya ya sheria, kutoifahamu vizuri ama kulewa madaraka, hali ambayo CHADEMA haitakubaliana nao.

Hivyo alisema Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge ambayo ilikuwa chini ya Mbunge wa Mlalo, Brigedia mstaafu Hassan Ngwilizi (CCM), haitawahoji wabunge wake kwa kuwa imekwisha kumaliza kazi yake tangu Februari 8, mwaka huu.
Msimamo wa CHADEMA unakuja zikiwa ni siku mbili tangu Ofisi ya Bunge kupitia Katibu Mkuu, Dk. Thomas Kashililah, itumie Jeshi la Polisi kuwataarifu baadhi ya wabunge wa chama hicho kuwa wanahitajika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano na kamati hiyo.

Katibu Mkuu huyo alisema kama wabunge wa CHADEMA wanaitiwa kuhusu vurugu zilizotokea bungeni Februari 4, mwaka huu, tayari zimeshatolewa hukumu yake kwa kuwataja wahusika kuwa ni Tundu Lissu (Singida Mashariki), John Mnyika (Ubungo), Paulina Gekul (Viti Maalumu) na Joshua Nassari ( Arumeru Mashariki).

Alisema katika hukumu hiyo ambayo ilisomwa na Spika Makinda ilikuwa ya upande mmoja wa kamati yenyewe iliyokaliwa na wabunge wa CCM ambao waliwaona wabunge wa CHADEMA pekee ndio waliofanya vurugu huku ikishindwa kuwaita wahusika kwa mahojiano.
Aidha, alisema hata kama kamati ya Brigedia Ngwilizi ingekuwa hai, wabunge wake wasingeitii, kwa kuwa tayari imekwisha kuwahukumu.
Hata hivyo Dk. Slaa alitumia nafasi hiyo kumtaka Spika Makinda kwenda kozi kwa ajili ya kujifunza sheria za kuongoza Bunge kutokana na kushindwa kwake katika kipindi chote alichokalia kiti hicho.
“Nasikia Spika Makinda huwa anasema kuwa niwafundishe wabunge wangu sheria, kanuni na  taratibu za Bunge kwa kuwa nazifahamu vizuri, kwani yeye na wanasheria wake wanafanya nini? Kupoka kwake sheria na taratibu za bungeni ndizo zinazosababisha vurugu?” alihoji Dk. Slaa na kuongeza:
“Nataka nimwambie kwamba wakati nipo bungeni, maspika waliokuwa wakiongoza Bunge akiwamo Samuel Sitta walikuwa wakijua kuongoza, kwa kufuata sheria na kanuni zake na ndiyo maana hakuna vurugu zilizokuwa zikitokea na si yeye.”
Aidha, alisema maspika hao walikuwa wanajua kwamba mabunge yote ya Afrika na yale ambayo Tanzania inaiga kutoka kwao yana sheria na taratibu zinazowaruhusu kushangilia hata kuzomea kwa kutaja chama chao na si hivi ambavyo Spika Makinda anavyofanya.
Lissu anena
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Lissu alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za Kamati ya Haki, Kinga na Maadili ya Bunge, zinamtaka Katibu Mkuu wa Bunge Dk. Kashililah kuandika barua hizo kwa niaba ya Spika Makinda lakini hakufanya hivyo.
Lakini pia Lissua alisema hata barua ya polisi (police message) waliyopewa si taarifa tosha ya kujipeleka wao kuhojiwa bali walipaswa kupelekewa taarifa ya kuitwa kwa ajili ya mahojiano na Bunge.
Kutokana na maelezo hayo Lissu alisema hakuna jambo lililofuatwa kisheria, hivyo hakuna watakayemwona, na alidai kuwa tayari hukumu yao ilishatolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Brigedia Ngwilizi Februari 8, mwaka huu.

WANYARWANDA WAKOMALIA NDOA YA UWOYA

KATIKA kile kilichoonekana ni kuikomalia ndoa ya msanii wa filamu Bongo Irene Uwoya, baadhi ya wadau nchini Rwanda wameendelea kutambua kuwa yeye ni mke halali wa msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.
Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards.
Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia.
“Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut.
“Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.
Chanzo Global Publishers

ADAIWA KUMCHINJA MPENZI WAKE KAMA KUKU

Na  Globalpublishers
VILIO vilitawala Kata ya Nyahanga wilayani hapa wakati wa kuuaga mwili wa binti Jessica Elialinga (19) aliyeuawa kinyama kwa kuchinjwa kama kuku na mpenzi wake, Musa Petro (27) mkazi wa Shunu kwa sababu zinazodaiwa ni wivu
wa kimapenzi.
Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.
Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.
Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.
 “Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.
“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.
 Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.
 Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.
 Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.
Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.
Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.
 Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.

HII NDIO HISTORIA FUPI YA PAPA FRANCIS 1: JORGE MARIO BERGOGLIO

          Francis (/ˈfrænsɨs/, /ˈfrɑːnsɨs/; Latin: Franciscus [franˈtʃiskus]; born Jorge Mario Bergoglio; 17 December 1936) is current pope of the Catholic Church. He serves as the 266th pope, having been elected on 13 March 2013. In that role, he is both the leader of the Catholic Church and sovereign ruler of the Vatican City State.

A native of Buenos Aires, Bergoglio was ordained as a priest in 1969. From 1998 until 2013, he served as the Archbishop of Buenos Aires, and Pope John Paul II made him a cardinal in 2001. Elected as pope in 2013 following his predecessor Pope Benedict XVI's resignation, Bergoglio chose "Francis" as his name. This marked the first time in papal history that this name had been used, and along with Pope John Paul I is one of only two times since Pope Lando's brief 913 reign that a serving pope held a name unused by a predecessor. Francis is both the first Jesuit priest and the first native of the Americas to be elected Pope. He is also the first non-European pope since Syrian-born Pope Gregory III, who died in 741.

Jorge Mario Bergoglio was born in Buenos Aires, Argentina, one of the five children of Italian immigrants Mario José Bergoglio, a railway worker, and his wife, Regina María Sívori, a housewife. As a teenager Bergoglio had a lung removed as a result of an infection. He studied and received a master's degree in chemistry at the University of Buenos Aires before he decided to pursue an ecclesiastical career . According to another reference, he graduated from a technical school as a chemical technician, and at the age of 21 decided to become a priest.

Bergoglio entered the Society of Jesus on 11 March 1958 and studied to become a priest at the Jesuit seminary in Villa Devoto. In 1960 Bergoglio obtained a licentiate in philosophy from the Colegio Máximo San José in San Miguel; in 1964 and 1965 he taught literature and psychology at the Colegio de la Inmaculada, a high school in the province of Santa Fe, Argentina, and in 1966 he taught the same courses at the Colegio del Salvador in Buenos Aires.

In 1967, Bergoglio finished his theological studies and was ordained to the priesthood on 13 December 1969, by Archbishop Ramón José Castellano. He attended the Facultades de Filosofía y Teología de San Miguel (Philosophical and Theological Faculty of San Miguel), a seminary in San Miguel, Buenos Aires. Bergoglio attained the position of novice master there and became professor of theology.

The Society of Jesus promoted Bergoglio and he served as provincial for Argentina from 1973 to 1979. He was transferred in 1980 to become the rector of the seminary in San Miguel, and served in that capacity until 1986. He returned to Argentina to serve as confessor and spiritual director in Córdoba.

Kwa Kusoma Zaidi Juu ya Historia Fupi ya Papa Mpya Jorge Mario Bergoglio BOFYA HAPA

TGNP yashinda kesi ya Jengo Mahakama Kuu

 Jengo lenyewe la TGNP
Usu Mallya

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), walinunua  jengo la ofisi hii kutoka kwa Mfilisi wa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited (TSTML) yaani Benki ya Rasilimali ya Tanzania mnamo tarehe 15th June, 1997. 

Wapangaji wasiohalali walikwenda mahakamani wakiwashitaki Benki ya Rasilimali ya Tanzania pamoja na TGNP na kesi ilifunguliwa tarehe 16th July 1997 kesi ilipewa Na. 215/1997. Madai ya washitaki yalikuwa yafutayo:
    a)        TGNP ilipendelewa katika mchakato mzima wa tenda ya manunuzi ya jengo hili na kwamba TGNP hawakuwa wazawa.
   b)        Utoaji wa tenda kwa upande wa Beki ya Rasilimali Tanzania ulikuwa batili kwa sababu haukufuata/haukuzingatia sheria ya nchi ya manunuzi na hivyo kukiuka haki za kimsimgi (failure to observe the law, public policy and the rules of natural justices)

TGNP kama washitakiwa walishinda kesi hiyo ya  madai namba 215/1997 iliyofunguliwa na waliokuwa wapangaji. Jengo lenye kesi ni jengo la gorofa moja zilipo Ofisi za Makao Makuu ya Shirika Mabibo Dar es salaam.

Chini ya Mhe. Jaji T.B. Mihayo, 15 Oktoba 2009, TGNP Ilishinda kesi hiyo na walalamikaji walidai kuwa TGNP imependelewa. Oktoba 19, 2009, walifungua rufaa katika makahakama kuu ya Rufaa ya Tanzania, wakiipinga hukumu ya kesi ya msngi namba 215/1997 na kukawa na kesi ya rufaa namba 129/2009 ili pia waendelee kukaa kwenye jesngo hilo.

TGNP iliiomba mahakama kufuta ombi la walalamikaji la kuendelea kuwa kwenye jengo ili shirika liweze kufanya shughuli zake, kesi ambayo ilisikilizwa na majaji watatu waheshimiwa jaji Msasali, jaji Msofe, na jaji Rutakanga Julai 22,2011.

Tarehe 23. 08.2011, TGNP iliamua kwa mujibu wa sheria kuwatoa kwa nguvu wapangaji hao ambao kwa muda wote wa zaidi ya miaka 10 wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye jengo la TGNP bila kulipa kodi wala ruhusa yao, lakini siku chache baadaye walirudi. Pamoja na ushindi walioupta TGNP bado waliendelea kuheshimu maamuzi ya mahakama kutokana na shauri walilolipeleka mahakamani.

Mwaka 2012 walalamikaji walienda tena Mahakama Kuu wakiomba kurekebisha majina ya watu waliosomewa hukumu kuwa  watu wengine walio hukumiwa hawakuwa sehemu ya kesi hii!!  TGNP tuliona kuwa hii ni  mbinu tuu ya kuchelewesha  kesi ambayo imekuwa ikitumika  kwa miaka mingi. Jaji Mwaikugile aliikubali hiyo barua akitaka wakaandike vizuri zaidi ili hoja yao isikilizwe. Kesi hii imepangiwa kusikilizwa tena hapo tarehe 26 Februari 2013, lakini hadi tarehe 08.03.2013 hawakuwa wamewasilisha na leo tarehe 13.03.2013 jaji ametupilia mbali ombi lao.

Kesi hii imekuwa ni changamoto kwa TGNP, huu ni mwaka wa 16 tangu shirika linunue jengo hili.

Sote kwa pamoja tunaamini katika haki na na rasilimali lazima zirudi kwa wananachi!

Imetolewa na:
Usu Mallya
Mkurugenzi Mtendaji TGNP

Rais Kikwete akutana na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry Ikulu jijini Dar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (The World Intellectual Property Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry (wa tatu kushoto) akiwa na ujumbe wake wakati alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Haki Miliki Duniani (The World Intellectual Property Organization –WIPO) Dr. Francis Gurry katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi.Joyce Mapunjo (katikati) wakimsikiliza kwa makini Rais Dr. Kikwete wakati akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO (hawapo pichani).
Baadhi ya Maafisa mbalimbali wa Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mh. Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry aliyeambatana na Ujumbe wake. Wa pili kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimwonyesha Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry mmoja ya mti wa Mwembe (haupo pichani) uliodumu kwa miaka mingi Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry mara baada ya mazungumzo alipomtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara Dr. Abdallah Kigoda.
Rais Dr. Jayaka Mrisho Kikwete na Mkurugenzi Mkuu wa WIPO Dr. Francis Gurry. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).

Wednesday, March 13, 2013

CARDINAL JORGE MARIO BERGOGLIO ACHAGULIWA KUWA PAPA MPYA; KUTUMIA JINA LA PAPA FRANCIS

Hatimae Jopo la Makardinali 115 wa Kanisa katoliki wamemchagua Kardinali wa Buenos Aires kutoka Latin Amerika Jorge Mario Bergoglio (68) kuwa kiongozi mpya atakaye chukuwa nafasi ya  Papa Benedict aliyejiuzuli hivi karibuni.

Jorge Mario Bergoglio ambaye ni Muagrgentina tayari amechagua jina la atakalo litumia katikakipindi chake cha Uongozi kuwa atatambulika kama Papa Francis.

Jopo la Makardinali wamemchagua Cardinali kutoka Latin America Cardinal Jorge Mario Bergoglio, kushika wadhifa mpya wa  Papa katika uchaguzi uliofanyika kwa mara ya tano kwa kura zilizopugwa na Makadinali 115 waliokuwa wakikutana katika kanisa la Sistine Chapel huko Vatican , Roma.

Maelfu ya watu walikuwa wamefurika katika eneo la la St. Peters huko Vatican huku mamilioni wengine wakishuhudia Papa huyo mpya akitangzawa mbele yao.

MOSHI MWEUPE ISHARA YA PAPA MPYA KUPATIKANA

White smoke appeared from the chimney above the Sistine Chapel, and bells from St. Peter's Basilica have pealed, meaning the 115 Roman Catholic cardinals gathered at the Vatican from all over the world have chosen a new pope.
The church's 266th pontiff will replace Benedict XVI, whose surprise resignation last month prompted the cardinals to initiate a conclave, a Latin phrase meaning "with a key," to pick a new leader for the world's almost 2 billion Catholics.

Although it's not immediately clear who received the necessary two-thirds vote, several candidates were mentioned as front runners, including what could be the first African pope or the first pope from the U.S. or Canada.

The new church leader takes over an organization many say is in crisis, from damaging allegations of internal squabbling to the cover-up and abetting of sexual abuse, though the latter issue came to light before Benedict's papacy.

Some sources say the Catholic Church in the U.S. has paid out as much as $3 billion to settle sexual abuse claims, though others estimate a billion less. At least eight U.S. Catholic dioceses declared bankruptcy protection. Benedict said in a 1998 U.S. visit that he was ashamed of the sex abuse scandal, and assured that the church would not allow pedophiles to become priests.

The Pope Emeritus also faced criticism for his role in overseeing the church's reaction to the sexual abuse crisis, as well as revelations from the "Vatileaks" incident. The pope's butler was implicated in the leaking of documents that included what Italian media first characterized as evidence of blackmail and disarray among church leaders regarding how to address growing concerns about money laundering.

Though Benedict basically dismissed those allegations as exaggerated, he remarked that the leaks and results of the ensuing investigation he commissioned had saddened him. Church outsiders have speculated that the results of Benedict's investigation may have led to his decision to resign from the papacy, a move unprecedented in six centuries.

The new pope will also face pressure to modernize the church on issues from reforming the clergy to allowing contraception. It's unclear if the cardinals will pick a pope who will change the church or a conservative leader who will remain dedicated to its current principals.

MZEE KINGUNGE ATAKA VIONGOZI KUENZI LUGHA YA KISWAHILI

 Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati  uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi  katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na kulia ni Brigedia Hashimu Mbita.
Baadhi wa wadau  wakifuatilia kwa makini  uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi  katika hafla iliyofanyika leo  kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.
Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi  katika hafla iliyofanyika leo  kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam. Picha na Magreth Kinabo – Maelezo
*******************************************

NA: FRANK SHIJA & BENEDICT LIWENGA- MAELEZO

VIONGOZI wahimizwa MWANASIASA mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kuwataka viongozi nchini kukienzi na kuthamini lugha ya Kiswahili ili kuendelea kujenga taifa lenye umoja na mshikamano.

Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Mzee Kingunge ambaye alikuwa  mgeni ramsi katika hafla ya uzinduzi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee,  jijini Dar es Salaam .

“Hatima ya Taifa inategemea lugha ya Kiswahili. Viongozi wanawajibu mkubwa katika kuhakikisha kuwa lugha ya Kiswahili inakuwa kwani wao ndio wanaweza kukipandisha au kuiua lugha ya Kiswahili kwakuwa jamii inawategemea kwa kiasi kikubwa,” alisema Mzee Kingunge.

Aidha  Mzee Kingunge anawaasa kuwa wazalendo na kutumia lugha ya hiyo kwa ufasaha tofauti na ilivyo sasa katika shughuli mbalimbali mfano Bungeni.

Hata hivyo, aliunga mkono  lugha hiyo kuwa rasmi kufundishia, lakini ametoa changamoto kuwa yatupasa kuwa makini katika kuitumia hususani katika ngazi elimu ya msingi, sekondari hadi vyuo vikuu.

Mzee Kingunge alitolea mfano wa wajukuu zake kuwa masomo mengine kama vile hesabati wanapata  alama 90 hadi 95,lakini lugha hiyo wanapata alama ya 60 mpaka 70. Hivyo inaelekea ufundishaji wake ni tatizo.

“Kama kufundisha lugha ya Kiswahili katika elimu ya sekondari ni tatizo na Kiingereza ni tatizo . Kiswahili kipi kifundishwe katika elimu ya Chuo Kikuu,”alisema. Huku akitolea mfano kuwa kumekuwa na matumizi ya maneno ambayo si sahihi kama vile neno masaa badala ya saa.

Kwa upande wake mwanazuoni na mdau wa lugha hiyo  Profesa Mugyabuso Mulokozi na  Profesa Joshua Madumula wameiomba serikali kuwa na utaratibu wa kuenzi   fasihi za Watanzania.

GODBLESS LEMA AITISHA MAANDAMANO

Lema aitisha maandamano
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, ametangaza kuandaa maandamano makubwa yatakayoshirikisha wanawake na watoto katika Jiji la Arusha ili kushinikiza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Arusha (AUWSA) kuwasambazia maji.

Akizungumza jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji safi.
“Nimewaandikia barua AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa umma,” alisema Lema.
Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya hakupatikana kuelezea kama amepokea barua hiyo baada ya kutopatikana ofisini, pia simu yake ya mkononi ilikuwa haipatikani.

MAPOZI" YA LULU MICHAEL AKIWA KITAA.


Lulu back to basics how sweet

MUONEKANO MPYA WA WEMA SEPETU BAADA YA KUZITIA MKASI NYWELE ZAKE



Mrembo na Miss Tanzania wa zamani, Wema Sepetu ameamua kubaki natural baada ya kuzinyoa nywele zake. Kupitia Instagram, Wema ameshare picha hizo na kuandika, ‘me apa nimenyoa nywele’. Ingia ndani kusoma maoni aliyoyapata baada ya kunyoa.

Mh. Pinda kubariki Tamasha la Pasaka jijini Dar

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Pasaka Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa tayari Ofisi ya Waziri Mkuu imeshathibitisha kuhusiana na ujio wake kwenye tamasha hilo.

“Tunafurahi kwamba tamasha letu mwaka huu Dar es Salaam mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, mwaka jana alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe,” ilisema taarifa hiyo ya Msama.

Waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo, ambapo wan je ya nchi ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda.

Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro, Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 
 
 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...