Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa wamepozi nje ya Hotel Ritz na mchambuzi wa soka Edo Kumwembe huko Angola tayari kwa kupambana na Libolo siku ya leo katika mechi ya pili ya Mabingwa wa Afrika. |
Sunday, March 03, 2013
SIMBA NDANI YA ANGOLA TAYARI KUPAMBANA NA LIBOLO
Tume ya Wajumbe 15 iliyoundwa na Waziri Mkuu ya kuchunguza Matokeo CSEE 2012 hii hapa.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda jana Jumamosi, Machi 2, 2013 amezindua Tume maalum
aliyoiunda ili ifanye uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne
yaliyotangazwa Februari 18, mwaka huu na kuwataka wajumbe wa Tume hiyo
watafute kiini cha mserereko wa kushuka kwa ufaulu kuanzia mwaka 2010
hadi 2012.
Waziri
Mkuu amezungumza na wajumbe wa Tume hiyo kwenye ukumbi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulihudhuriwa
pia na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa.
Amesema
kwa mujibu wa hadidu za rejea, wajumbe wa tume hiyo watatakiwa
kuangalia ni sababu zipi zimechangia kuwepo kwa matokeo hayo mabaya,
mserereko wa kushuka umekuwa ukiongezeka kwa sababu gani, usimamizi
katika Halmashauri ukoje, ukaguzi wa elimu na uhamishiwaji wa sekta ya
elimu kwenye Wizara ya TAMISEMi umechangiaje kushuka kwa kiwango cha
ufaulu.
Vilevile,
watatakiwa kuangalia mitaala na mihutasari ikoje, kuangalia uwiano
uliopo kwenye mitihani inayotungwa ikiwa ni pamoja na uhakiki wa
mitihani hiyo; kuangalia mazingira ya kufundishia, mfumo wa upimaji,
usimamizi na uendeshaji, na kutokuwepo kwa chakula shuleni kunachangiaje
kushuka kwa utendaji mbaya wa wanafunzi katika masomo yao.
Tume
hiyo yenye wajumbe 15, imepewa muda wa wiki sita kuanzia Machi mosi iwe
imekamilisha kazi hiyo na kuwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu.
Tume itaongozwa na Prof. Sifuni Mchome wa Tume ya Vyuo Vikuu, na Makamu wake atakuwa Bi. Bernadetha Mushashu (Mbunge wa Viti Maalum – Kagera).
Wajumbe ni Bw. James Mbatia (Mbunge wa kuteuliwa), Bw. Abdul J. Marombwa (Mbunge wa Kibiti), Prof. Mwajabu Possi (Chuo Kikuu – UDSM), Bibi Honoratha Chitanda (CWT), Bibi Daina Matemu (TAHOSSA) na Bw. Mahmoud Mringo (TAMONGSCO).
Wangine ni Bw. Rakhesh Rajani (TWAWEZA), Bw. Peter Maduki (CSSC), Mwl. Nurdin Mohamed (BAKWATA), Bw. Suleiman Hemed Khamis (Baraza la Wawakilishi, Zanzibar), Bw. Abdalla Hemed Mohamed (Chuo Kikuu – SUZA), Bw. Mabrouk Jabu Makame (Baraza la Elimu Zanzibar na Bw. Kizito Lawa (Taasisi ya Kukuza Mitaala).
Mkutano wa CUF Jimbo la Kwamtipura mjini Zanzibar
Mwakilishi
wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail
Jusa Ladu wakushoto akiwa na Mkurugenzi wa Habari,Uwenezi na
Mawasiliano ya Umma wa CUF Salum Abdallah Bimani wakisikiliza kwa makini
risala ya vijana wa jimbo la Kwamtipura katika mkutano wa hazara
uliofanyika katika kiwanja cha mpira kwamtipura.
Wananchi
wa Jimbo la Kwamtipura wakisikiliza kwa makini hutuba ya Mwakilishi wa
Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail
Jusa Ladu hayupo pichani katika Mkutano wa hazara uliofanyika huko ktk
kiwanja cha mpira kwamtipira
Mwakilishi
wa Mji Mkongwe ambae pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CUF Ismail
Jusa Ladu akihutubia wananchi wa Jimbo la Kwamtipura katika Mkutano wa
hazara uliofanyika ktk kiwanja cha mpira kwamtipira.(Picha na Makame
Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Makamu wa Rais Dkt. Bilal Kufungua Miradi ya Maendeleo ya Ujenzi Mkoani Mara.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib
Bilal atakuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Miradi ya
Maendeleo inayotekelezwa na Wizara ya Ujenzi kuanzia tarehe 04/03/2013
mkoani Mara.
Pamoja
na shughuli nyingine, siku ya Jumatatu tarehe 04 Machi 2013 akiwa
mkoani humo, Mhe. Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya
ukarabati wa barabara ya kutoka mpakani mwa Mkoa wa Simiyu na Mara hadi
Musoma yenye urefu wa kilomita 85.5. Barabara ambayo ujenzi wake
utawekewa jiwe la msingi ni sehemu ya Barabara ya Mwanza – Nyanguge –
Makutano – Musoma ambayo ni kiungo muhimu na nchi jirani za Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi. Hivyo kukamilika kwake ni fursa nyingine
nzuri ya kuibua uchumi wa nchi yetu na ukanda huu.
Jumanne
ya tarehe 5 Machi 2013 asubuhi Mhe. Makamu wa Rais atazindua Kivuko cha
Musoma kinachotoa huduma kati ya Musoma na Kinesi. Siku hiyo hiyo
mchana Makamu wa Rais ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa
Nyumba za Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) zilizoko eneo la Old Customs
katika barabara ya Lake Side, Musoma.
Uzinduzi
wa miradi hii ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya nne ya
kuboresha miundombinu muhimu ya usafiri na makazi kwa wananchi wake.
Aidha, uzinduzi wa Kivuko cha Musoma (MV Musoma) kinachotoa huduma kati
ya Manispaa ya Musoma na Kinesi Wilayani Rorya ni utekelezaji wa ahadi
za Mheshimiwa Rais baada ya kupokea ombi la Kivuko kutoka kwa wakazi wa
Musoma na vitongoji vyake.
Saturday, March 02, 2013
Siku chache baada ya Wema sepetu kutangaza nafasi za kazi mrebo huyo ashangazwa na wingi wa Emails
Hivi karibuni Miss Tanzania wa zamani,
Wema Sepetu alizindua rasmi ofisi za kampuni yake iitwayo Endless Fame
Films zilizopo maeneo ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Uzuri wa
ofisi zake unadaiwa kuifanya kampuni yake kuwa ya kwanza nchini ya aina
hiyo yenye ofisi za nguvu zaidi. Baada ya kutangaza nafasi za kazi
mbalimbali wiki hii, Wema ameshangazwa na wingi wa email alizopokea
kiasi cha kupost picha kwenye Instagram yenye maneno: da emails omg...
im tryng ma best to reply ol of dem....
Mshindi wa Tigo Smartcard Promotion Julius Kanza awasili nchini Hispania.
Mshindi
wa Tigo Smartcard Promotion Bw. Julius Raphael Kanza akiwa Madrid
Hispania tayari kusubiri pambano la el classico kati ya Real Madrid na
Fc Barcelona litakalofanyika kesho kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Julius Kanza akitembelea sehemu mbalimbali za jiji hilo.
DStv REWARDS YAENDELEA KUIBUA MAMILIONEA: AHMED SALIM SALEH ASHINDA Tshs.5,000,000
Ahmed
Salim Saleh, mshindi wa Tshs, 5,000,000 za DStv Rewards akiwa na uso wa
furaha huku ameshikilia mfano wa hundi aliyokabidhiwa.
Katika
muendelezo wa kampeni ya DStv Rewards kampuni ya MultiChoice Tanzania
inayo furaha kumtangaza rasmi mshindi wake wa tatu. Mshindi huyo ni Ahmed Salim Saleh,
mfanyakazi wa Access Bank ya jijini Dar-es-Salaam.
Kupitia droo ya DStv Rewards, MultiChoice Tanzania inaibua baadhi ya
wateja wao kuwa “mamilionea” ambapo katika kila wiki mteja mmoja huibuka
mshindi wa kitita cha Shilingi Milioni 5. (Tshs 5,000,000)
Meneja
Masoko wa MultiChoice Tanzania, Furaha Samalu, akiwa na mshindi wa DStv
Rewards kwa wiki ya tatu, Ahmed Salim Saleh, baada ya kumkabidhi mfano
wa hundi ya kitita cha Tshs. 5,000,000 alichojishindia.
DStv Rewards
ni sehemu ya kampeni maalum ya kampuni ya MultiChoice Tanzania
kuwashukuru wateja wao kutokana na ushirikiano mkubwa inaoupata kutoka
kwao.
Kampeni hiyo maalumu ilianza tarehe 5 February, 2013 na inaendelea mpaka
tarehe 10 April, 2013. Wateja ambao wanakuwa na nafasi ya kuibuka
“mamilionea” ni wale ambao hulipia akaunti zao za DStv kabla
hazitajakatwa kwa kulipia kifurushi chochote kati ya DStv Access, DStv
Family, DStv Compact, DStv Compact Plus na DStv Premium.
Mshindi
wa DStv Rewards, Ahmed Salim Saleh, akisaidiwa na baadhi ya wafanyakazi
wenzake kushangilia kwa kuibuka mshindi wa Tshs, 5,000,000 alizoshinda.
WANAO DAI KUWA LULU MICHAEL KAFANYIWA SHEREHE YA KUTOKA GEREZANI NI WAONGO NA WANAMPANGO WA KUMKWAMISHA KISHERIA..:...FAMILIA YA LULU YANENA
Kulipuka
kwa habari kuwa staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’
amefanyiwa sherehe na kigogo baada ya kutoka Segerea, Dar kwa dhamana,
familia yake imecharuka na kudai kuwa hakukuwa na jambo kama hilo wala
haifikirii kufanya hivyo
Habari
za uhakika zilidai kuwa Lulu ambaye anakabiliwa na kesi ya kumuua bila
kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba, mara baada ya kuachiwa kwa
dhamana Januari 26, mwaka huu, kuliibuka minong’ono kutoka kwa marafiki
zake mbalimbali walioelezwa kuwa walitaka kumfanyia pati lakini ndugu
walikataa.
Ilielezwa
kuwa licha ya ndugu hao kukataa kumfanyia sherehe ndugu yao (Lulu),
bado kuna kikundi cha watu kiliendelea kueneza taarifa za kizushi kwamba
lazima kuwe na sherehe ya kumpongeza baada ya kutoka gerezani.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana ndani ya familia ya Lulu zilieleza
kuwa taarifa zilizosambaa mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba alifanyiwa
bonge la pati na kikundi hicho kama madai ya awali yalivyokuwa, hazikuwa
na ukweli wowote na mbaya zaidi zililenga kumjengea Lulu mazingira
magumu ya kisheria.
Akizungumza
na mwandishi wetu kwa sharti la kutochorwa jina , dada wa Lulu alisema
kuwa familia ilikerwa kupita maelezo na kuwepo kwa taarifa hizo huku
akisisitiza kwamba hazina ukweli wowote.
“Sisi
kama familia hatujamfanyia wala hatufikirii kumfanyia sherehe ya aina
yoyote kwa ajili ya kumpongeza. Tunaomba ieleweke hivyo na hao
wanaoeneza habari za uongo waache haraka, hatuzipendi,” alisema dada
huyo.
HATIMAYE SERIKALI YAANZA KUJENGA KIWANDA CHA GESI MTWARA
***********
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema jana kuwa ujenzi huo
unaofanywa na Kampuni ya China Petroleum and Technology Development Co-operation
(CPTDC), ambao awali, ulipaswa kuanza wiki iliyopita, umeanza juzi baada ya
Serikali kufikia mwafaka na wananchi wa Kijiji cha Msimbati
kinapojengwa.
“Mkuu wa Wilaya
ya Mtwara (Wilman Ndile) na vijana wake walilazimika kufika Kijiji cha Msimbati,
ambako wananchi walikuwa na mgogoro na watu wa Marine Park,” alisema
Maswi.
KILIMANJARO MARATHON YAZINDULIWA
Maandalizi ya Mbio za
Nyika za Kilimanjaro Maarufu kama Kilimanjaro Marathon 2013 yanafikia kiele hii
leo na kesho ndio kivuvumbi na jasho wakati maelfu ya wanariadha na watu wa
kawaida wakitimua vumbi katika mbio hizo zinazofanyika katiua mji wa Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Pichani ni baadhi ya
wakimbiaji wakijiandikisha kwaajili ya kushiriki mbio hizo zitakazo fanyika
Machi 3,2013 mjini Moshi na zitakuwa za makundi mbalimbali 42KM, 21KM na 5km Fun
Run.
Makundi mbalimbali katika
Jamiui nayo yanashiriki ikiwa ni pamoja na walemavu ambao pichani wakiwa katika
banda la kujiandikishia.
Maofisa watakao simamia
Mbio hizo Machi 3, 2013 wakiwa Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi kuchukua
vifaa.
Mbio za kujifurahisha kwa
watoto na watu wazima zipo na hapa wakijiandikisha.
Baadhi ya wadhamini wakiwa
tayari wamesha pamba mabanda yao ndani ya Uwanja wa Ushirika Mjini
Moshi.
Mitaani napo Mabango ya
Mbio hizo yamewekwa
Rais Obama awa miongoni mwa viongozi walioalikwa katika sherehe za kumuapisha rais mpya wa Kenya.
Rais
Barrack Obama wa Marekani amekuwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa
dunia walioalikwa katika hafla ya kuapishwa kwa rais wa nne wa Kenya.
Mkuu
wa Huduma za Jamii Francis Kimemia serikali imewaalika viongozi kama
vile Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon na Mkuu wa Mataifa ya
umoja wa Ulaya.
Pia
wamealikwa marais wa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki (EAC) ikiwa ni
pamoja na rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, rais Paul Kagame wa Rwanda na rais Pierre Nkurunziza wa
Burundi.
Rais
mpya wa Kenya anatarajiwa kuapishwa kuchukua madaraka hapo Machi 3
mwaka huu, ikiwa ni wiki tatu baada ya wakenya kufanya uchaguzi.
Wafanyakazi Ikulu Waadhimisha Siku ya Mazingira Afrika kwa Kufanya Usafi wa Mazingira.
Naibu
Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzana Mlawi (mwenye blauzi ya kijani) na
Mkurugenzi wa Huduma Ikulu Bw. Julius Mogore(mbele) wakiongoza
shughuli za usafi kuzunguka maeneo ya Ikulu jijini Dar es salaam leo
Machi 1, 2013 katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Afrika. Siku hiyo
itaadhimishwa kitaifa siku ya Jumapili.
Picha
zingine zinaonesha Wafanyakazi wa kila kada Ikulu bila kujali nyadhifa
zao wanafanya kazi bega kwa bega kuhitimisha Siku ya Mazingira Afrika
kwa kufanya usafi.(PICHA NA IKULU).
Subscribe to:
Posts (Atom)