Takriban
watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana
wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha
mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.