Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
MWANAFUNZI wa Kidato cha Pili, Jofrey Robert Mwakatenya (15)
anatuhumiwa kuuawa kikatili na baba yake mzazi, Robert Mwakatenya (35)
baada ya kumkuta akiwa na barua ya mapenzi, inayodaiwa aliandikiwa na
rafiki wake wa kike.
Mzazi huyo ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Majengo ‘D’
Manispaa ya Sumbawanga, anadaiwa kumwadhibu mwanafunzi huyo, ambaye ni
mtoto wake wa kwanza kwa kupiga ngumi na mateke mfululizo kwa zaidi ya
saa tatu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Jacob Mwaruanda alithibitisha tukio
hilo, lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita. Alisema bado
wanamtafuta mtuhumiwa huyo kwani baada ya kufanya kitendo hicho
alitokomea. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.