Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
Tuesday, December 16, 2014
MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 16, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
THIERRY HENRY ATANGAZA RASMI KUSTAAFU SOKA
Katika ulimwengu wa soka leo kuna habari kubwa ambayo imeenea duniani kutokana
na staa mkubwa na mkongwe Thierry Henry kutangaza kustaafu soka na kujiunga na
shughuli nyingine. Nyota huyo ambaye ameng’aa kwenye mchezo huo kwa
muda mrefu sana akichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Arsenal na
Barcelona.
Henry ametangaza rasmi kustaafu soka
dakika chache zilizopita na kusema kuwa kuanzia mwakani ataanza
kujishughulisha kama Balozi wa Sky Sports huku akisema kuwa anajisikia
furaha kuchezea vilabu vikubwa na pia anaamini anajiunga na kituo
kikubwa cha Television na matarajio yake ni kuwa mchambuzi bora wa
michezo kwenye kituo hicho.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
HAYA NDIYO MAAMUZI MAGUMU YA YANGA KUHUSU MBRAZIL EMERSON
Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari
hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa
kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa
na Yanga.
Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.
Emerson alishindwa kuwaridhisha
mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa
kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.
Emerson alikuja nchini siku chache
zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji
Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini
kufuatia kusimama kwa ligi.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year
Tuesday, December 09, 2014
ANGALIA PICHA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA UHURU WA TANZANIA BARA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akiwapungia mikono wananchi waliofurika katika uwanja wa Uhuru Jijini
Dar es Salaam katika Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Uhuru wa
Tanzania Bara akiwa katika Gari maalum liliozunguuka katika uwanja huo
leo.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,Jenerali Davis
Mwamunyange.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikitoa salamu ya heshma wakati Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili katika
Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam leo katika sherehe za kilele cha
maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za
kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara
zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
Gwaride la Vikosi vya Ulinzi na Usalama lilioandaliwa katika sherehe za
kilele cha Maadhimisho ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara
zilizofanyika leo katika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 09, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Monday, December 08, 2014
WAHAMIAJI 70 WAFA MAJI YEMEN
Watu 70 wamekufa baada ya boti iliyokuwa imejaza wahamiaji haramu kupinduka baharini, magharibi mwa Yemen.
Maafisa nchini Yemen wamesema wengi ya watu waliokuwa katika boti hiyo ni raia wa Ethiopia.Hali mbaya ya hewa inaelezwa kwamba ndio chanzo cha kuzama kwa boti hiyo.
Mamia kwa maelfu ya wahamiaji wamekuwa wakihatarisha maisha yao kwa safari zisizo na usalama katika nchi zilizo katika pembe ya Afrika na Yemen kila mwaka.
Umoja wa Mataifa unamini kwamba kiasi cha watu watu mia mbili wamezama maji katika kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
EBOLA YAUA DAKTARI MWINGINE S-LEONE
Wakuu wa Sierra Leone wanasema daktari mwengine amefariki kutokana na Ebola - ni daktari wa 10 kufa na ugonjwa huo.
Aiah
Solomon Konoyima alifariki Jumamosi kwenye kituo cha matibabu karibu na
mji mkuu, Freetown, siku moja tu baada ya wenzake wawili kufa na
ugonjwa huo huo.Mwezi wa Julai daktari maarufu kabisa kutibu wagonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, Sheik Umar Khan, piya mwisho aliuliwa na virusi vya Ebola.
Vifo 1,600 vya Ebola vimesajiliwa nchini humo.
Sierra Leone imekuwa ikijaribu kukarabati huduma za afya baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka ya 1990s.
Na daktari kutoka Cuba ambaye alipona Ebola, ameahidi kuwa atarudi Sierra Leone kumaliza kupambana na ugonjwa huo nchini humo.
Dakta Felix Baez, ambaye alipata Ebola nchini Sierra Leone, alisema hayo aliporudi Havana baada ya kujaribiwa matibabu aina mpya nchini Uswiswi ambayo yalimponesha.
Dakta Baez alikuwa kati ya madkatari na wauguzi wa kwanza 250 walioambukizwa Ebola Afrika magharibi.
Cuba ndio nchi iliyotuma huko wafanyakazi wa utabibu wengi kabisa kwenda kupambana na Ebola.
Mchango huo wa Cuba umesifiwa kimataifa hata na Marekani, adui yake wa kisiasa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC
Sunday, December 07, 2014
MUTHARIKA AJINYIMA NYONGEZA YA MSHAHARA
Rais Peter Mutharika wa Malawi na naibu wake wameakhirisha kujipa nyongeza ya mishahara baada ya kuzuka malalamiko.
Nyongeza
kutoka mshahara wa dola 3,000 na kufikia dola 5,000 kila mwezi,
imezusha malalamiko nchini Malawi ambako pato la nusu ya wananchi
halitimii dola moja kwa siku.Bwana Mutharika na makamo wake, Saulos Chilima wamesema hawatojipa nyongeza ya mishahara hadi uchumi wa nchi utengenee.
Kabla ya viongozi hao kushika madaraka wafadhili walisimamisha msaada wa dola 150-milioni kwa sababu ya wasiwasi kuhusu rushwa.
Mishahara ya wabunge itazidishwa asili-mia-mia-tatu (300%) Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
MUGABE ATEULIWA TENA KUONGOZA ZANU-PF
Rais Robert Mugabe ameteuliwa tena kuongoza chama tawala nchini Zimbabwe na mke wake Grace akapewa wadhifa wa juu katika chama.
Kupandishwa
cheo kwa Grace Mugabe kuongoza tawi la wanawake la Zanu-PF kunamuweka
katika nafasi nzuri ya kumrithi mumewe katika siku zijazo,wanasema
wachambuzi.Mke huyo wa Rais amewashtumu wakinzani wake wa kisiasa akiwemo Makamo Rais Joyce Mujuru, katika miezi ya hivi karibuni.
Bwana Mugabe mwenye umri wa miaka 90,anatazamiwa kugombea tena urais mnamo mwaka 2018.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Zanu-PF,Bwana Mugabe aliwashukuru maelfu ya wafuasi wake kwa kumchagua kuongoza chama . "Najua nilikotoka.. mimi si bora kushinda watu walonizaa ," alisema Mugabe, ambaye ameiongoza Zimbabwe tangu mwaka 1980.
Madai ya mauaji
Kuteuliwa kwa mke wa Mugabe kuongoza tawi la wanawake kunaonekana kama ni ishara nyigine zaidi kwa Joyce Mujuru ambae wakati mmoja alionekana kama angeweza kumrithi Mugabe sasa amepigwa pande.
Bi Mujuru alipigania pamoja na Bw.Mugabe uhuru wa Zimbabwe kutoka utawala wa wazungu wachache.
Lakini alijikuta matatani wakati Bi Mugabe mwenye umri wa miaka 49, kujitumbukiza katika siasa mnamo mwaka huu na kumshutumu makamo wa rais wa kula njama dhidi ya mumewe. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Subscribe to:
Posts (Atom)