Ripoti
zinasema kuwa maandamano yamefanywa katika mji wa Beni, mashariki mwa
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, baada ya mauaji ya karibuni yaliyofanywa
na wapiganaji.
Kituo cha redio cha huko kinasema kuwa waandamanaji
wanaodai ulinzi zaidi, wameshambulia sanamu ya Rais Joseph Kabila saa
chache baada ya kujulikana kuwa watu 7 zaidi waliuwawa Jumamosi usiku.Inakisiwa kuwa watu kama 100 wameuwawa katika eneo la Beni katika mwezi uliopita.
Wanaoshukiwa kufanya hayo ni wapiganaji wa ADF - kundi la wapiganaji Waislamu kutoka Uganda ambao sasa wanapigana na jeshi la Congo na askari wa Umoja wa Mataifa.
Alipozuru mji wa Beni Ijumaa, Rais Kabila aliahidi ulinzi zaidi kwa raia na aliomba kuwa kikosi cha Umoja wa Mataifa huko kizidishwe. Asante kwa kutembelea blog hii, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na BBC