Baadhi ya waandishi wa habari na
wadau kutoka asasi mbalimbali nchini wakifanya usajili kwenye kongamano
la siku moja lilioandiliwa kuadhimisha Uhuru wa vyombo vya Habari
Duniani 2014 lililofanyika jijini Arusha.
Na Waandishi Wetu, Arusha
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri (TEF), Absalom Kibanda ametoa wito kwa waandishi wa habari
nchini kuyapa uzito matukio yanayowatokea waandishi wa habari na
kuyapigia kelele kwa nguvu zote ili kuyakomesha.
Kibanda aliyasema hayo
jana mjini Arusha katika kongamano lililoandaliwa kama sehemu ya
maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na kuongeza
kwamba wakati umefika kwa waandishi wa habari kuondoa tofauti zao na
kuungana pamoja kuongeza nguvu waliyonayo kukabiliana na ukatili
unaoendelea dhidi ya waandishi wa habari katika miaka ya hivi karibuni.
“Baadhi ya wahariri
huwa hawayaandiki madhila yanayowasibu waandishi wa habari na kuyapa
uzito unaostahili aidha kwa huyapuuzia au kudharau kwa kuwa hayawahusu
moja kwa moja,” alisema Kibanda.
Aliongeza kwa kusema
kuwa vyombo vya habari mara nyingi vimekuwa vikinyooshewa vidole na
kulaumiwa kwa kutokufanya kazi kwa uadilifu jambo ambalo linatafsiriwa
kuwa ni la uonevu, vinatumiwa vibaya na hakuna anayesimama kuvitetea
kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz