Tuesday, March 07, 2017

MAGUFULI AAGIZA TANESCO KUWAKATIA UMEME WASIOLIPA BILI

Rais wa Tanzania John Magufuli jana aliiagiza kampuni ya ugavi wa umeme nchini humo (TANESCO) kuwakatia umeme wateja wote wenye madeni makubwa kwa kampuni hiyo, ikiwemo serikali ya Zanzibar.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi kwenye kituo kipya cha TANESCO mkoani Mtwara, rais Magufuli alisema kuwa tasisi zote za umma zinapaswa kulipa madeni la sivyo zitakatiwa umeme.

Alisema kuwa serikali ya Zanzibar pekee, kupitia shirika la umeme za Zanzibar (ZECO), ina deni la TANESCO kiasi cha shilingi bilioni 121 za Tanzania.

"Msiogope mnapaswa kukata huduma hii kwa taasisi yoyote ambayo hailipi bili zake. Nataka kumwambia waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwamba umeme unapaswa kukatwa hata Ikulu. Nikilala gizani, halafu maafisa wa Ikulu ambao hawajalipa watawajibika na sio wewe. Una hakikisho langu kwa hili.
Pesa za kulipa bili kawaida hutolewa kwa wizara zetu, lakini badala yake hupelkwa kwingine.

"ninaambiwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haijalipa Sh121 billion. Ninyi (TANESCO) si wanasiasa... mnapaswa kuzingatia majukumu yenu ya kitaaluma... kata huduma ya umeme. Nimesema hata kama ni Ikulu, polisi, jeshi ama shule, hakuna mwenye deni anaepaswa kuachwa. Ni kwa njia hii tu tunaweza kuhakikisha kwamba pesa zilizotengewa wizara kwa ajili ya umeme zinatumiwa kama ilivyopangwa ili TANESCO iweze kuendesha kazi zake na kushughulikia matatizo ya uhaba wa umeme. TANESCO haiwezi kuboresha huduma kwa sababu ya madeni ya serikali yasiyolipwa''.

Alipozungumza na gazeti la Citizen jana, Waziri wa nchi katika ofisi ya makamu wa pili wa rais, Bwana Mohammed Aboud, alisema kuwa mipango inafanyika kwa ajili ya kuliwezesha shirika la ZECO kulipa madeni ya TANESCO.

"Maagizo ya rais Magufuli yako wazi. Madeni lazima yalipwe na yatalipwa. Tumeanza mchakato wa kuhakikishwa suala hili linatatuliwa. Pia tumeiagiza ZECO kuacha kulimbikiza madeni mapya.

Mawaziri hao wawili walifanya mkutano juu ya suala hilo hivi karibuni na kujadili namna deni hilo linavyoweza kulipwa" Bwana Aboud aliliambia gazeti la The Citizen.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...