Sunday, July 28, 2013

GADNA AFUNGUA MILANGO KWA WASANII


MTANGAZAJI aliyejizolea umaarufu kupitia kipindi chake cha Maskani kinachorushwa katika kituo cha redio Times, Gadna G. Habashi ameweka mikakati ya kutoa nafasi ya kucheza muziki wa kizazi kipya ndani ya kipindi hicho bila ya kuchagua.

Gadna ambaye anaamini kuwa kipindi cha redio kinapendezeshwa kwa kupiga muziki, hivyo kwa upande wake anaamini kipindi chake kinaboreshwa na muziki hususani wa bongo fleva.


Mtangazaji huyo aliweka wazi juu ya mikakati hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi, ambapo alisema njia hiyo ni moja ya mikakati yake ya kutoa fursa kwa wanamuziki wa hapa nchini, ambayo inaonekana wengine wanakosa kwenye redio nyingine.


"Unajua mimi nisipopiga muziki kipindi hakipendezi, hivyo nikipiga muziki huo kwanza ni njia ya kuutangaza muziki pamoja na msanii mwenyewe bila ya kubagua muziki huu ni wa nani?" alisema Gadna.


Alisema kwenye kipindi chake hachagui ni mwanamuziki gani apige nyimbo zake, bali anachokifanya ni kuangalia jamii inahitaji burudani ya aina gani.


Gadna ni mtangazaji anayeamini kuwa neno la kutoa fursa linaendana na vitendo, hivyo moja ya kitendo anachokiamini kinachowasaidia wasanii nyumbani ni kupiga nyimbo zao kwenye redio, ili kumuwezesha msanii afahamike na aweze kupata shoo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...