Thursday, March 21, 2013

SHILOLE, BABY MADAHA WAFUATA NYAYO ZA WEMA


WAREMBO wawili wanaotesa katika soko la muziki na filamu Bongo, Baby Joseph Madaha na Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wameamua kufuata nyayo za Wema Sepetu kwa kunyoa nywele na kuonekana katika muonekano mpya.
 

Akizungumza na paparazi wetu, Shilole ambaye amenyoa nywele staili ya kiduku alisema ameamua kufanya bhiv yo ili kuwa na muonekano wa tofauti kwani watu wameshamzoea kila siku kumuona na mawigi na rasta.
 

Kwa upande wa Baby Madaha alisema ameamua kubadilisha mfumo wa maisha kuanzia nywele hadi mavazi kwani huu ni mwaka mpya hivyo kutoka na staili mpya.
Hivi karibuni Wema alikuwa wa kwanza kutangaza kuwa na muonekano tofauti kwa kutupia picha zake mtandaoni zilizomuonesha akiwa amenyoa.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...