Thursday, May 05, 2016

SNURA AWAOMBA RADHI WATANZANIA, AWASILISHA VIDEO SAFI YA CHURA BASATA

Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
 
Jana video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa la taifa, BASATA.
 
Kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania ambayo itaikagua. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

HUKUMU KESI YA KAFULILA MEI 17

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi, David Kafulila inatarajia kutoa hukumu Mei 17, mwaka huu.

Jaji wa mahakama hiyo anayesikiliza kesi hiyo mjini Kigoma, Ferdinand Wambali, alisema kuwa amepanga kutoa hukumu tarehe hiyo baada ya pande zote mbili kuwasilisha ushahidi na maelezo yao.

Baada ya kukamilika kwa ushahidi huo, Jaji Wambari aliomba kupatiwa muda wa kutosha kupitia ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo ili aweze kutoa hukumu ya haki.

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo ni mshtakiwa wa tatu katika kesi hiyo. Katika kesi hiyo namba 2 ya mwaka 2015, Kafulila anaishawishi mahakama itengue matokeo yaliyompa ushindi aliyekuwa mgombea wa CCM, Hasna Mwilima badala yake imtangaze yeye kama mshindi halali wa jimbo hilo.

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni pamoja na Mbunge wa jimbo hilo Hasna, aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uvinza, Ruben Mfune ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na Mwanasheria wa Serikali ambaye anaiwakilisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika kesi hiyo, Wakili Kenedy Fungamtama anamtetea Husna huku Kafulila akitetewa na mawakili watatu, Profesa Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Rumenyela.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MEI 05, 2016 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

20160505_074606 20160505_074619 20160505_074634 20160505_074644


Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...