Tuesday, February 09, 2016

MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA POLE KWA MKE WA PINDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za pole Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Mama Tunu Pinda aliyepatwa na ajali ya gari, iliyotokea jana tarehe 08 Februari, 2016 akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mkundi lililopo katika Manispaa ya Morogoro ambapo gari aliyokuwa akisafiria Mama Tunu Pinda, ilipinduka baada ya kumgonga mwendesha pikipiki aliyeingia ghafla barabarani.

Katika salamu hizo alizozituma kupitia kwa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko taarifa za kutokea kwa ajali hiyo na amemuombea Mama Pinda na Majeruhi wengine kupona haraka.

"Kupitia kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu Pinda, naomba unifikishie pole nyingi kwa mkeo Mama Pinda kwa kuumia katika ajali hii, na namuomba Mwenyezi Mungu awaponye majeruhi wote ili waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku" alisema Rais Magufuli.

Mama Tunu Pinda anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es salaam, na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
09 Februari, 2016

MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARI 09, 2016


DSC00926 DSC00927 DSC00928 

Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Friday, February 05, 2016

HAYA NDIO MAGARI MAPYA YA POLISI UGANDA


 Magari Maalum ya Jeshi la Polisi la Uganda yakiwa yamewasili Bandari ya Mombasa Nchini Kenya, tayari kwa safari ya kuelekea Kampala.

Jeshi la Polisi la Uganda limejiimarisha zaidi kipindi hiki cha kampeni na hasa siku ya Uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni.


MAGUFULI: MIMI SI KICHAA WALA DIKTETA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Magufuli.


RAIS Dk. John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini, alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisifu kazi kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora zikawasaidia wananchi.

“Ninapochukua hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,” alisema.

Alipongeza kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.

“Mnafanya kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’, nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.

UBELGIJI VINARA VIWANGO VYA UBORA FIFA


 Ubelgiji imeendelea kukaa katika nafasi ya kwanza kwenye viwango vya ubora vya FIFA kwa muhjibu wa viwango viliyotolewa Alhamisi.

Katika kumi Bora imebaki vile vile bila mabadiliko huku Mabingwa wa Dunia, Germany, wakiwa Nafasi ya 4.

Ivory Coast imeporomoka hadi Nafasi ya 9 kwa bara la afrika na sasa ipo Nafasi ya 28 Duniani ikifuatiwa na Cape Verde ambayo ipo Nafasi ya 33 baada ya kupanda Nafasi huku Algeria ikiwa Nafasi ya 36 baada ya kushuka Nafasi 8.

Timu nyingine katika ishirini bora ni Ubeligiji, Argentina, Uhispania, Ujerumani na Chile.

20 bora katika viwango vya Fifa.

1 Ubelgiji

2 Argentina

3 Uhispania

4 Ujerumani

5 Chile

6 Brazil

7 Portugal

8 Colombia

9 England

10 Austria

11 Uruguay

12 Switzerland

13 Ecuador

14 Uholanzi

15 Italy

16 Romania

17 Wales

18 Croatia

19 Hungary

20 Uturuki

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...