Friday, June 05, 2015

SERENA ATINGA FAINALI FRENCH OPEN 2015

Serena William,mchezaji tenis nambari moja duniani akifurahia ushindi.
Serena Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu kucheza fainali za mwaka huu.

Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.

Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

Tuesday, June 02, 2015

AL-SHABAAB WADAIWA KUVITEKA VIJIJI KENYA

Alshabaab
Hofu kubwa imetanda Kaskazini mwa nchi ya Kenya,baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kundi la wapiganaji wa Al shabaab Limeviteka vijiji kadhaa katika mpaka wa Kenya na somalia.
Mamia ya wakaazi wameyatoroka makaazi yao kufuatia taarifa za kuwepo kwa wapiganaji wa Alshabaab wapatao thelathini.
Shule nne zinaripotiwa kufungwa.
Naibu kamishna wa kaunti ya Mandera amenukuliwa akisema kwamba wamepokea ripoti za kuwepo kwa wapiganaji hao na watawaandama na kulidhibiti eneo hilo. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

MLIPUKO WA BOMU WAUA WATU 20 NIGERIA

Mlipuko nchini Nigeria
Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko wa bomu katika mji wa kaskazini mashariki wa Maiduguri nchini Nigeria.
Mji huo ulikuwa umeshambuliwa saa za alfajiri siku ya jumanne na washukiwa wa kundi la Boko haram .
Saa chache baadaye ,mlipuaji wa kujitolea muhanga alijilipua katika soko la kuuza ngombe la Gamboru ndani ya mji huo kulingana na walioshuhudia.
Wakati wa kuapishwa kwake rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari alisema kuwa anayahamisha makao makuu ya kijeshi katika vita dhidi ya wapiganaji hao kutoka mji mkuu wa Abuja hadi Maiduguri. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...