Saturday, November 29, 2014

HENRY ATAKA KUISAIDIA ARSENAL

Thiery Henry
Uwezekano wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya.
Henry huenda akaweka viatu vyake vya soka chini jumamosi wakati ambapo kilabu yake ya New York Red Bulls itajaribu kulipiza kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika fainal ya raundi ya pili dhidi ya New England Revolution.
Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amekamilisha kandarasi yake na kilabu hiyo na ijapokuwa anasema kuwa hakuna kilichoafikiwa kuhusu hatma yake ameanza kutoa maoni yake kuhusu maisha yake baada ya kusakata soka.
Arsene Wenger
Na baada ya kocha Arsene Wenger kumfungulia milango mchezaji huyo ,Henry amesema kuwa angependelea kuisaidia kilabu yake ya zamani.
''hakuna kilicho wazi''Henry aliliambia gazeti la L'Equipe.''Sijafanya uamuzi wowote na mimi sipendelei uvumi'',.
''Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba nitasalia katika soka kama mkufunzi ama afisa mkuu ,lakini tutaona'',alisema Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, November 28, 2014

ASKOFU KILAINI, NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA YA ESCROW

Baba Askofu Methodius Kilaini  

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni). Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ESCROW NJIAPANDA, WABUNGE WAGAWANYIKA...!!!




Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati)  akiwasihi Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa  Nkasi, Ali Kessy wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.

Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.

Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.

Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 28, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
;
.
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...