Tuesday, December 29, 2015

ARSENAL YAPAA KILELENI


Wachezaji wa timu ya Arsenal

Washika bunduki wa London, Arsenal wamekaa kileleni mwa ligi ya England kwa pointi 39 baada ya kuichapa Bournemouth kwa mabao 2-0.

Arsenal walipata mabao yao kupita kwa beki Gabriel Paulista aliyefunga bao la kwanza Dakika ya 27 ya mchezo kisha kiungo wa Kijeruman Mesut Ozil, akahitimisha kazi kwa bao la pili alilolifunga katika dakika ya 63.

Nao Mashetani Wekundu wa Man United wakaenda sare ya 0-0 na mabingwa watetezi Chelsea, Everton wakicheza katika dimba lao la Goodson Park wakalala kwa kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Stoke city.

Matokeo mengine ni: Crystal Palace 0 – 0 Swansea Norwich 2 – 0 Aston Villa Watford 1 – 2 Tottenham West Brom 1 – 0 Newcastle West Ham 2 – 1 Southampton

Monday, December 28, 2015

MLINZI WA OSAMA BIN LADEN AFARIKI DUNIA


Al Bahri


Taarifa kutoka Yemen zinasema aliyekuwa mlinzi wa Osama Bin Laden, amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Vyanzo vya habari vya kitabibu vimesema kwamba Nasser al Bahri ambaye pia alikuwa akijulikana kama Abu Jandal alifariki siku ya Jumamosi, katika Hospitali iliyoko kwenye mji wa Mukalla kusini mwa Yemen.

Alirudi nchini humo mwishoni mwa mwaka 2008, baada ya kuachiliwa kutoka katika kizuizi alichowekewa na Marekani huko Guantanamo.

Al Bahri alijulikana kuhusika na mashambulizi yaliyofanywa na mtandao wa kigaidi katika miaka ya 90, katika nchi za Afghanistan, Somalia na Bosnia.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...