Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba. PICHA|MAKTABA
Mwenyekiti wa
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wizi
wa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow, mvutano kati ya
mihimili ya dola na viongozi kukosa maadili ni matokeo ya nchi kuwa na
Katiba isiyo na majibu ya masuala hayo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Jaji Warioba alisema Bunge la Katiba lilifanya makosa kutoviweka vifungu vinavyozungumzia mambo hayo katika Katiba Inayopendekezwa ambavyo awali vilipendekezwa na Tume yake katika rasimu ya pili.
“Katika mchakato wa Katiba Mpya tulisema kuwe na mgawanyo wa madaraka na kila mtu ajue madaraka yake ni nini na kutenganisha Serikali na Bunge. Kama Serikali na Bunge vingetenganishwa bungeni usingeibuka mvutano kuhusu waliochota fedha za escrow. Bunge lingekuwa huru katika utendaji wake wa kazi,” alisema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz