Monday, December 01, 2014

RAIS KIKWETE AMTEUA PROFESA ASSAD KUWA CAG MPYA


Profesa Mussa Juma Assad 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Desemba Mosi, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, inasema kuwa uteuzi wa Bwana Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu, 2014.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Bwana Assad ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 2, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar es Salaam. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz 

BOKO HARAM WAVAMIA MIJI MIWILI NIGERIA

Nia kuu ya Boko Haram ni kuwa na dola ya kiisilamu inayofuata sheria za kiisilamu.
 
Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram wamefanya mashambulizi katika miji miwili eneo la Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
La kwanza lilikuwa la kujitoa mhanga pamoja na shambulizi lengine katika kituo cha polisi cha Damaturu.
Wenyeji wa mji wa Maiduguri walielezea kusikia milipuko miwili kwenye soko moja.
Mashambulizi mengine ya kujitoa mhanga eneo hilo wiki iliyopita yaliwaua zaidi ya watu 70.
Mapema leo Jumatatu watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram waliteketeza kituo cha polisi katika mji wa Damataru kilicho umbali wa kilomita 100 Magharibi mwa mji wa Maiduguri.
Inaarifiwa watu 5 wameuawa katika mashambulizi hayo ya mabomu yaliyotokea katika soko lililokuwa na watu wengi.
Mjini Damaturu , milipuko na milio ya risasi ilisikika huku wanamgambo hao walipokuwa wanashambulia mjini huo.
Boko Haram imeahidi kubuni dola ya kiisilamu katika maeneo ambayo kundi hilo linadhibiti.
Milipuko hio ilitokea Jumatatu katika soko la Maiduguri , mji mkuu wa jimbo la Borno ambayo ilisababishwa na wasichana wawili waliojilipua.
Takriban watu 32 walijeruhiwa katika milipuko hio. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ICC YAKATAA OMBI LA MUASI LUBANGA

Mahakama ya ICC imetupilia mbali ombi la Lubanga kupunguziwa kifungo jela.
 
Mahakama ya kimataifa ya ICC mjini Hague, imetupilia mbali ombi la rufaa lililowasilishwa na muasi wa zamani nchini DRC Thomas Lubanga dhidi ya hukumu aliyopewa kwa makosa ya kuwatumia watoto kama wanajeshi.
Viongozi wa mashtaka walisema wavulana wadogo wenye umri wa miaka 10 walitekwa nyara na kusajiliwa kama wanajeshi DRC katika vita hivyo vilivyoanza mwaka 1999.
Wasichana nao walitumiwa kama watumwa wa ngono.
Mnamo mwaka 2012, Lubanga alikuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa na mahakama hio.
Aliwahi kuwa kiongozi wa kundi la wapiganaji la (UPC), ambalo lilikuwa la kabila la Hema ambalo lilihusika katika vita eneo la Ituri Mashariki mwa DRC.
Mahakama ilimpata na hatia kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na kuwatuma kwenda kumpigania. Alihukumiwa kifungo cha miaka 14.
Kundi la UPC, lilikuwa moja ya makundi sita ya wapiganaji waliopigana kudhibiti eneo lenye utajiri wa madini la Ituri hadi mwaka 2003.
Mgogoro ulianza kama mvutano wa kupigania mali asili, ingawa baadaye ilipanda daraja na kuwa vita vilivyohusisha jeshi la Uganda.
Kadhalika mgogoro huo uligeuka na kuwa vita kati ya jamii za Hema na Lendu ambapo takriban watu 50,000 waliachwa bila makao. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Sunday, November 30, 2014

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI NOVEMBA 30, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


DSC06297

DSC06285
DSC06286 
Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HONGERA DIAMOND: ATWAA TUZO 3 ZA CHANNEL O AFRIKA KUSINI

Diamond akiwa na tuzo.
MSANII Naseeb Abdul 'Diamond Platumz' ametwaa tuzo tatu za Channel O usiku wa kuamlia leo nchini Afrika Kusini. Tuzo hizo ni; Most Gifted new comer, Most Gifted Afropop na Most Gifted East kupitia wimbo wake wa Number One! Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TAZAMA PICHA ZA AJALI YA HELIKOPTA ILIYOANGUKA JANA JIJINI DAR



Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akifafanua jambo mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaa,Mh.Sadick Meck Sadick akizungumza mbele ya Vyombo vya habari katika eneo la ajali, kufuatia kutokea kwa ajali hiyo iliyopelekea vifo vya watu wanne.


Baadhi ya Watu wakishuhudia mabaki ya helikopta hiyo iliyopata ajali maeneo ya Kipunguni B Moshi Bar, Ilala jijini Dar es Salaam.  Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ZIARA YA KINANA MTWARA MJINI

Vijana wa Bodaboda wakiongoza msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiwasili Mtwara mjini ambapo alishiriki shughuli mbali mbali za kujenga na kuimarisha chama pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.
 Msafara wa Katibu Mkuu ukielekea Mtwara mjini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mikindani mara baada ya kukabidhi leseni kwa madereva 70 wa boda boda waliohitimu mafunzo chini ya udhamini wa Mbunge wa Mtwara mjini Hasnain Murji.
 Wananchi wa Mikindani mkoani Mtwara wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana . Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS KIKWETE ' NIMEPONA SARATANI'

Rais kikwete akitoa hotuba yake kwa taifa .Amesema kuwa amepona saratai ya kibofu.
  Rais Jakaya Kikwete amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani. Rais Kikwetemwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WALIOKUFA KWA EBOLA WATIMIA 7,000



Takwimu mpya zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani, WHO, zinaonesha kuwa watu karibu 7,000 wamefariki hadi sasa kutokana na Ebola, karibu wote Afrika Magharibi.
Hao ni watu zaidi ya elfu moja kuliko idadi iliyotangazwa na WHO Jumatano tu.
Vifo vingi zaidi vimesajiliwa Liberia.
WHO inasema watu zaidi ya 16,000 wameugua Ebola hadi sasa.
Waandishi wa habari wanasema kuongezeka kwa idadi ya waliokufa siyo lazima inamaanisha ugonjwa unazidi kutapakaa kwa kasi kwa sababu takwimu nyengine ni za zamani. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Saturday, November 29, 2014

SWAPO YAELEKEA KUSHINDA TENA NAMIBIA

Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi mkuu wa Namibia yanaonesha kuwa chama tawala cha SWAPO kimeshinda kwa kura nyingi.
SWAPO imetawala Namibia tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka wa 1990.
Lakini wanasaiasa wa upinzani kwa mara nyengine tena wanataka kura ibatilishwe, wakidai kuwa kanuni zilikiukwa na wapigaji kura waliendelea kupiga kura hata baada ya muda uliowekwa.
Mahakama makuu katika mji mkuu, Windhoek, yalitupilia mbali madai ya kuahirisha uchaguzi uliofanywa Ijumaa.
Wanasiasa wa upinzani wanasema upigaji kura wa digitali, bila ya kutumia karatasi, unatoa fursa ya kufanya udanganyifu.
Tume ya uchaguzi imekiri kuwa kulitokea matatizo kwenye mashini wakati wa kupiga kura, hata hivyo inasema matokeo yatakuwa ya kuaminika. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KESI DHIDI YA MUBARAK YATUPILIWA MBALI

Aliyekuwa rais wa Misri Hosni Mubarak. Kesi ya mauaji dhidi yake imetupiliwa mbali na mahakama moja nchini humo.
Mahakama moja nchini Misri imetupilia mbali kesi dhidi ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak kutokana na mauaji ya mamia ya waandamanaji wakati wa maandamano ya kumng'atua mamlakani.
Aliyekuwa waziri wa maswala ya ndani wakati wa uongozi wa Mubarak ,Babib al Adly pamoja na maafisa kadhaa pia wameondolewa mashtaka.
Mubarak alihukumiwa miaka miwili iliopita lakini mahakama ya rufaa ikamuondela kifungo cha maisha gerezani.
Mahakama hiyo pia ilimuondolea rais huyo wa zamani mashtaka ya ufisadi.
Bwana Mubarak tayari anahudumia kifungo cha miaka mitatu kutokana na mashtaka ufujaji wa mali ya uma. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

KOCHA WA LIVERPOOL AHOFIA HATMA YAKE

Mkufunzi wa Liverpool Brenda Rodgers asema kuwa anahofia kufutwa katika timu hiyo kutokana na matokeo mabaya 
 
Mkufunzi wa timu ya liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa anakabiliwa na tishio la kufutwa kutokana na msururu wa matokeo mabaya ya timu hiyo.
Baada ya Liverpool kupata alama moja pekee katika mechi nne za mwisho ilizocheza,Liverpool iko katika nafasi ya 12 katika ligi ya Uingereza ,ikiwa na alama 18 nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Chelsea.
Miezi kadhaa iliopita ,nilikuwa mkufunzi mzuri msimu huu , na sasa mimi ninakabiliwa na tishio la kufutwa'',alisema Rodgers ambaye ameorodheshwa katika nafasi ya tatu miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kushinda ligi msimu huu.
''Ni mambo ambayo makocha hukumbana nayo katika maisha ya soka'',aliongezea koch huyo.Liverpool tayari imepoteza mechi sita katika ligi msimu huu ,ikiwa ni nyingi ikilinganishwa na alama zote walizopoteza msimu uliopita.
wachezaji wa Liverpool
Lakini siku ya Jumatano waliweza kupata sare ya 2-2 dhidi ya kilabu ya Ludogorets Razgad na hivyobaisi kuimarisha matumaini ya kilabu hiyo kufuzu iwapo itaichapa Fc Basel katika michuano ya muondoano ya taji la kilabu bingwa barani Ulaya.
''Kitu ambacho mtu hutakiwa kufanya ni kuendelea kujaribu kutafuta matokjeo mazuri''.,alisema Rodgers.
Kocha huyo wa zamani wa kilabu ya Swansea pia amemtetea kipa Simon Mignolet aliyeshtumiwa na mlinda lango wa zamani wa kilabu hiyo Bruce Grobbelaar. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

HENRY ATAKA KUISAIDIA ARSENAL

Thiery Henry
Uwezekano wa Thiery Henry kujiunga na Arsenal kama mkufunzi umeongezeka baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kufichua kwamba bado ana ndoto ya kuisadia Arsenal kushinda taji la kilabu bingwa barani Ulaya.
Henry huenda akaweka viatu vyake vya soka chini jumamosi wakati ambapo kilabu yake ya New York Red Bulls itajaribu kulipiza kichapo cha mabao 2-1 ugenini katika fainal ya raundi ya pili dhidi ya New England Revolution.
Mchezaji huyo mwenye miaka 37 amekamilisha kandarasi yake na kilabu hiyo na ijapokuwa anasema kuwa hakuna kilichoafikiwa kuhusu hatma yake ameanza kutoa maoni yake kuhusu maisha yake baada ya kusakata soka.
Arsene Wenger
Na baada ya kocha Arsene Wenger kumfungulia milango mchezaji huyo ,Henry amesema kuwa angependelea kuisaidia kilabu yake ya zamani.
''hakuna kilicho wazi''Henry aliliambia gazeti la L'Equipe.''Sijafanya uamuzi wowote na mimi sipendelei uvumi'',.
''Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba nitasalia katika soka kama mkufunzi ama afisa mkuu ,lakini tutaona'',alisema Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Friday, November 28, 2014

ASKOFU KILAINI, NZIGIRWA WAZUNGUMZIA TUHUMA YA ESCROW

Baba Askofu Methodius Kilaini  

Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini amekiri kupokea Sh80.5 milioni kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira akisema si mara yake kwa kwanza kupokea fedha kutoka kwa mfanyabiashara huyo kwa kuwa mara nyingi huwa anachangia kwa uwazi miradi ya jamii.
Askofu huyo alikuwa akizungumzia Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyosomwa bungeni juzi ikimtaja kuwa ni miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni kutoka katika akaunti ya escrow.
Katika ripoti hiyo, Zitto aliwataja viongozi wengine wa dini walioingiziwa fedha katika Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa Katoliki kuwa ni Askofu Eusebius Nzigirwa (Sh40.4 milioni) na Padri Alphonce Twimanye Simon (Sh40.4 milioni). Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ESCROW NJIAPANDA, WABUNGE WAGAWANYIKA...!!!




Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msangi (katikati)  akiwasihi Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (kushoto) na Mbunge wa  Nkasi, Ali Kessy wasigombane kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo jana alipangua hoja zilizotolewa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), kuhusu ufisadi uliofanyika katika Akaunti ya Tegeta Escrow na kuacha wananchi njia panda kwa kutokuelewa nani anasema ukweli kati yake na kamati hiyo, inayoongozwa na Zitto Kabwe.

Juzi, kamati hiyo ya Zitto iliwasilisha ripoti yake kuwa imethibitisha kuwa Profesa Muhongo amekuwa mara kwa mara akilipotosha Bunge na Taifa kwa ujumla kwamba ndani ya fedha hizo hakukuwa na fedha za umma.

Kamati hiyo ilieleza kuwa imebaini kuwa Profesa Muhongo ndiye aliyekuwa dalali mkuu aliyewakutanisha Singh Sethi na James Rugemalira tena katika ofisi ya umma na pengine hilo ndilo lilikuwa sababu ya upotoshaji.

Akiwasilisha taarifa ya Serikali kuhusu hoja hiyo, Profesa Muhongo alianza kupangua hoja moja baada ya nyingine ingawa katika mjadala wa baadaye, zilihojiwa na wachangiaji wengine waliohoji uhalali wa vielelezo alivyotoa. Asante kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...