Friday, July 25, 2014

MAGAZETI YA LEO IJUMAA JULAI 25, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


1_ba461.jpg
2_a3788.jpg
3_25f32.jpg 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

TIBA, KINGA YA UKIMWI VYANUKIA

Watafiti wakitoa sampuli za damu kutoka kwa sokwe mtu katika utafiti wa Ukimwi huko Gabon. Picha ya Mtandao 

Watafiti katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha Temple, Marekani wamegundua dawa ya kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambayo ni ya uhakika zaidi ukilinganisha na zilizowahi kupatikana katika tafiti za awali duniani.
Dawa yao inaweza kutumika kwa tiba ya wanaoishi na VVU na kinga kwa wale ambao bado hawajaambukizwa.
Mmoja wa watafiti hao, Dk Kamel Khalili aliwaambia waandishi wa habari juzi mjini Philadelphia, Marekani kuwa tofauti na utafiti mwingine, wao wamegundua namna ya kukiondoa kirusi kilichoingia kwenye kinasaba (DNA) ndani ya CD4 na kukitoa nje na hatimaye kukiua.
Alisema dawa hiyo inafanya kazi hiyo bila kuathiri seli za mwili wa binadamu.
Dk Khalili alisema ugunduzi wao ni wa hali ya juu zaidi kwa sababu teknolojia ya kutengeneza dawa hiyo ni tofauti na nyingine zilizokwisha kugunduliwa ambazo hazina uwezo wa kupenya ndani ya seli za binadamu, bali kuathiri tu VVU vilivyopo nje yake, ndani ya mfumo wa damu.
“Dawa yetu inakivuta kirusi nje ya seli (CD4) bila kuiathiri seli yenyewe na kukiua. Hivyo dawa hii itatumika kwa muda fulani na kuua virusi vyote mwilini na hakuna haja ya kuitumia wakati wote kama ilivyo dawa ya kufubaza VVU (ARV).” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MABAKI YA NDEGE ALGERIA YAONEKANA

Mabaki ya ndege iliyopotea ikiwa na watu 116 njiani kutoka Burkanafaso kwenda Algers yamepatikana nchini Mali. Maafisa wa Jeshi wa Burkina faso wamesema ndege hiyo iliyokuwa chini ya shirika la ndege la Algeria imeanguka karibia kilomita 50 kutoka mpaka wa Burkanafaso.
Waongoza ndege walipoteza mawasilino na ndege hiyo muda mfupi baada ya kupata taarifa kutoka kwa Rubani kuwa alikuwa kwenye eneo lenye hali mbaya ya hewa. Utafutaji wa ndege hiyo umeanzia katika eneo la Gao mpaka Tessalit. 
Kumekuwepo na hali mbaya ya hewa kwa zaidi ya saa 24. Waziri wa mambo ya nje wa ufaransa, Laurent Fabius amesema inaonekana ndege ilihamishwa mwelekeo kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.
 "Walikuwa wameelekezwa kubadili njia ya kawaida kutoka na mabadiliko ya hali ya hewa. Ndege ilikuwa ikipaa juu ya eneo la Malian. Pamoja na juhudi kubwa , mapaka sasa hakuna dalili za kupatika na kwa ndege hiyo. Pengine ndege imeangua" Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Sunday, June 29, 2014

HOTUBU YA WAZIRI MKUU MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA YA KUAHIRISHA BUNGE

PG4A9702
UTANGULIZI

a)    Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,
1.    Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutupatia uzima na afya hadi kufikia siku ya leo. Tumekuwepo hapa kwa takriban miezi miwili ambapo tumeweza kupokea na kujadili Taarifa za Mapitio ya Utekelezaji wa Kazi za Serikali kwa mwaka 2013/2014 na Mwelekeo kwa mwaka 2014/2015 kwa Wizara mbalimbali na hatimaye kupitisha Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2015.


2.    Napenda kutumia nafasi hii ya awali kuwapongeza Waheshimiwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ya kutukuka ambayo wameifanya kwa nidhamu na ufanisi mkubwa, hususan wakati wa Mjadala wa Bajeti ya Serikali na Mafungu ya Wizara za Kisekta. Kipekee niwashukuru Wajumbe wa Kamati ya Bajeti chini ya Uongozi mahiri wa Mheshimiwa Mtemi Andrew John Chenge, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Magharibi kwa kazi yao nzuri ya kuchambua Bajeti ya Serikali na Sheria zinazoambatana na masuala ya Bajeti. Changamoto zilikuwa nyingi,   lakini   kwa   pamoja   tumekubaliana   na   kuafikiana. Kazi kubwa iliyoko mbele yetu ni kwenda kushirikiana na Wananchi katika utekelezaji wa Bajeti hii ili kuwaletea maendeleo.

Mheshimiwa Spika,
3.    Katika kipindi hiki tukiwa hapa Bungeni, yapo matukio ya kusikitisha yaliyotokea ambapo baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walipoteza Wapendwa wao. Aidha, yapo matukio ya Kitaifa yaliyosababisha kupoteza maisha ya Ndugu, Jamaa na Marafiki. Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote waliofikwa na misiba na majanga mbalimbali, ikiwa ni pamoja na wote waliopotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

JAMBO TZ BLOG INAWATAKIA WATU WOTE KHERI YA MFUNGO WA RAMADHANI

http://jambotz8.blogspot.com/

 Jambo Tz Blog inawatakia Watanzania wote kheri ya mfungo mtukufu wa Ramadan.
http://jambotz8.blogspot.com/
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 29, 2014 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ANGALIA PICHA ZA KIATU CHA MALKIA ELIZABETH WA UINGEREZA ALICHOVAA KWA MIAKA 50...!!!

kiatu

Hizi ndiz0 Picha za kiatu cha aina moja alichovaa malkia Elizabeth wa Uingereza kwa miaka 50. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

kiatu1
kiatu2
kiatu4
kiatu5 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

ADA YA VYUO VYA UALIMU YAPANDA MARADUFU...!!!


Baadhi ya wahitimu wa chuo cha Ualimu.PICHA|MAKTABA
Serikali imepandisha maradufu ada kwa wanafunzi wanaosomea ualimu kwenye vyuo vya ualimu nchini kuanzia muhula ujao wa masomo. Ada hizo kwa wale wa ngazi za cheti na stashahada ambazo zimeongezwa kwa karibu mara mbili au zaidi ya zile zilizokuwa zikilipwa awali. Uamuzi huo ambao huenda ukawaathiri zaidi wanafunzi ambao waliona ualimu kama kimbilio, unaelezwa na baadhi ya wadau wakiwamo walimu, wanafunzi na hata wakufunzi wa baadhi ya vyuo nchini kuwa ni wa ghafla.
Kwa mujibu wa baadhi ya wakufunzi, uamuzi huo umetolewa kupitia waraka wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na unatarajiwa kuanza kutekelezwa muhula wa pili wa masomo utakaoanza Julai 2, mwaka huu.
Kabla ya kupandishwa kwa ada hizo, wanafunzi wanaosomea ualimu kwa ngazi ya cheti walikuwa wakilipa Sh200,000, lakini sasa watalazimika kulipa Sh300,000, ikiwa ni ongezeko la asilimia 50. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

CHINA HAITATUMIA MABAVU DHIDI YA MATAIFA MENGINE

Rais Xi Jinping amesema nchi yake haitawahi kutumia nguvu dhidi ya mataifa mengine Rais Xi Jinping wa Uchina amesema nchi yake daima haitojaribu kulazimisha nchi nyengine kufuata matakwa ya Uchina, hata Uchina itapokuwa na nguvu kubwa zaidi.

Alisema hayo mjini Beijing ambapo aliwapokea viongozi wa India na Myanmar (Burma). Rais Xi alisema tabia ya uonevu na kutumia nguvu za kijeshi haimo katika damu ya watu wa Uchina, na kwamba enzi za mabavu ya mataifa makuu zimekwisha.
Mwandishi wa BBC mjini Beijing anasema hotuba ya Rais Xi ilikusudiwa kuwatuliza majirani wa Uchina pamoja na Marekani, ambao wana wasi-wasi kwa vile bajeti ya jeshi la Uchina inazidi kuongezeka, na kile kinachoonekana kama sera ya Uchina ya kudai ardhi katika mizozo kadha na majirani zake.
Mkutano unaofanywa Beijing unaadhimisha miaka 60 ya makubaliano ya ushirikiano wa salama uliotiwa saini na Uchina, India na Burma - ambayo piya inajulikana kama Myanmar. Na nchini Taiwan shughuli mbili zimefutwa wakati wa ziara ya afisa mwandamizi wa Uchina, baada ya waandamanaji kuurushia rangi msafara wa magari yaliyokuwa yakimsindikiza afisa huyo.
Zhang Zhijun, ambaye amemaliza ziara ya siku nne Jumamosi, hakuumia katika mvurugano huo. Watu wengi wa Taiwan hawapendi Uchina kuonesha madaraka yake juu ya kisiwa hicho kinachojitawala, na ambacho Uchina inakiona kama ni chake. Katika miaka ya karibuni kiongozi wa Taiwan amekuwa akijaribu kuzidisha fungamanisho za kibiashara baina ya nchi mbili hizo.
Siku ya Ijumaa, Bwana Zhang alisema Beijing inaheshimu uamuzi wa watu wa Taiwan kuhusu aina ya maisha yao na mfumo wao wa jamii. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC Swahili

Thursday, June 26, 2014

UBABE BUNGENI, MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NUSURA AMPIGE KAFULILA

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kushoto) akizuliwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutomfuata Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila baada ya kupandwa na hasira kufuatia mbunge huyo kumtuhumu kwa kumuita mwizi kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 
Kwa ufupi
“Profesa Muhongo aliliambia Bunge kuwa Serikali ililipa fedha hizo ili kuondokana na kesi hiyo lakini ninazo nyaraka za Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), kuteua kampuni mbili za uwakili kwenda kuiwakilisha katika kesi nchini Uingereza,” alisema Kafulila.


Kama siyo kuzuiwa na mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema jana angezua tafrani bungeni kutokana na kitendo chake cha kutaka kumpiga Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. 

Sakata hilo lilitokea jana asubuhi baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Azzan Zungu kuahirisha kikao cha Bunge hadi jioni, ikiwa ni muda mfupi baada ya Werema na Kafulila kurushiana maneno bungeni. Jaji Werema alichukia baada ya Kafulila kumwita mwizi, akijibu mapigo baada ya mbunge huyo kuitwa tumbili na mwanasheria huyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...