Friday, May 02, 2014

HAMAD RASHID KUGOMBEA URAIS 2015

Hamad_Rashid6_3bea3.jpg
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amesema anapanga kujitosa kwenye kinyang’anyiro cha urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani.
Akizungumza katika mahojiano maalumu hivi karibuni mjini Dodoma, Hamad Rashid alisema: “Kama Mwenyezi Mungu akinijalia uhai na uzima mwakani, ninatarajia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha urais ama wa Muungano au wa Zanzibar.

“Ila sijaamua kama ni Bara au Zanzibar; kama ni chama cha CUF au kingine, hayo yote yatakuja baadaye,” alisema Hamad Rashid.
Mohamed ambaye ana mgogoro mahakamani na chama chake cha CUF, ametoa kauli hiyo wakati tayari viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), CUF kikiwamo wanajipanga kusimamisha mgombea mmoja wa urais katika uchaguzi ujao.
Mbali na CUF, vyama vingine vinavyounda Ukawa ni NCCR-Mageuzi na Chadema ambavyo pia vinakusudia kusimamisha mgombea mmoja kwa nafasi za ubunge na udiwani, lengo likiwa kukabiliana na nguvu ya chama tawala, CCM.
Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

WATU 19 WAUAWA KATIKA MLIPUKO NIGERIA

Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...