Thursday, October 24, 2013

MAMA KANUMBA "HUYU MCHUNGAJI KAIRUKI ANANITAFUTA KWA KUDAI KANUMBA YUPO HAI"

Baada ya hivi karibuni kuibuka tena kwa yule nabii na Mchungaji George Kaiuruki na kudai kuwa Marehemue Steven Kanumba bado yu hai, FROLA Mtegoa - mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji nyota filamu wa Bongo marehemu Steven Kanumba amesikitishwa na tabia ya mtu anayejiita Nabii George Kairuki kwa kutumia jina na kifo cha marehemu mwanaye kama njia ya kujitengenezea fedha na umaarufu, mama Kanumba anasema kuwa awali Kairuki alitumia msiba wa mwanaye katika kuongelea vitu ambavyo hata familia haivijui isipo kuwa yeye pekee yake.

Mama Kanumba anadai kuwa hivi karibuni Kairuki alijitokeza kwa kudai kuwa Kanumba hajafa na amemtumia fedha katika simu yake, na kusema kuwa karibu atamrudisha duniani na kuendelea na maisha yake jambo ambalo mama wa marehemu anapingana nalo kwa kusema kuwa yeye kwa imani yake anaamini kuwa mwanaye amefariki na hakuna miujiza mingine.

“Huyu mtu anayeitwa Nabii George Kairuki sijui anatafuta nini katika familia yangu, Kanumba alikuwa ni kipenzi cha watu na sisi sote tumeshuhudia hilo kama kweli yeye ana uwezo wa kumfufua amfufue watu wote watafurahi kipenzi chao kurudi kama anavyosema yeye, mimi simjui hata sura zaidi ya kumuona katika picha,”anasema mama Kanumba

Mama Kanumba anasema kuwa iwapo Kairuki ataendelea na tabia hiyo itabidi afanye utaratibu wa kumfungulia mashitaka na hata ikibidi kumfungulia mashitaka na kumfunga endapo ataendelea na tabia ya kutumia sana jina la Kanumba katika kujitafutia fedha na kutangaza maneno ya ajabu ajabu.

VATICAN YAMSIMAMISHA ASKOFU KWA KUPENDA RAHA


Page_12_0_47c17.jpg
Kumekuwa na kelele za waumini nchini Ujerumani wakishinikiza askofu huyo afukuzwe kwa kukiuka taratibu.
Vatican City. Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Duniani (Vatican) yamemsimamisha kazi Askofu wa Jimbo la Limburg, Ujerumani Franz-Peter Tebartz-van Elst anayekabiliwa na kashfa ya matumizi mabaya ya fedha kwa shughuli za kifahari.
Vatican ilieleza jana kuwa uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuridhika kuwa Askofu van Elst amekiuka maadili yaliyowekwa na Papa Francis kwa viongozi walioko chini yake akiwataka waishi maisha ya uchaji, umaskini.
Hadi sasa, kumekuwa na kelele nyingi miongoni mwa waumini nchini Ujerumani wakitaka askofu huyo afukuzwe kazi.
Miongoni mwa matumizi yake makubwa ni ujenzi wa makazi yake binafsi yaliyogharimu Euro 2.9 milioni (Dola 3.9 milioni), ukumbi wa chakula wenye mita za mraba 63 ambao ni pamoja na mesi na bafu yenye thamani ya Euro 15,000.

M23 WAIVURUGA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

m3 8b114
KUNDI la waasi wa M23, linalopambana na Jeshi la Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), limetajwa kuwa chanzo cha kuisambaratisha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kauli hiyo imetolewa juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, katika mahojiano yake na kituo cha redio cha Clouds.


Membe amesema kinachosababisha Tanzania itengwe na baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya ya EAC, ni hatua yake ya kupeleka majeshi katika mji wa Goma ulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kwa ajili ya kupambana na waasi wanaoipinga Serikali ya Rais Joseph Kabila.
Amesema hatua hiyo ya Tanzania ilizikera baadhi ya nchi wanachama wa EAC, zenye maslahi ya moja kwa moja na kundi hilo na kusisitiza kuwa hata kama itatengwa, kamwe haitaondoa vikosi vyake DRC na badala yake vitaendelea kupambana.

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 24, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.

.
.

AJALI MBAYA YATOKEA IRINGA JANA




k_fe241.jpg
Daladala aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha Bibi.
l_dd9a2.jpg
m_74746.jpg
Taxi ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika eneo la tukio.

n_7bc78.jpg
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).

MSAFARA WA RAIS KIKWETE WAKUMBWA NA BALAA LA MOTO MKALI

Moto mkubwa ukiteketeza msitu wa Sao Hill Mufindi



 Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa  umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka katika msitu huo jana mchana.


 Askari polisi akimamisha  msafara  wa rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga


 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa  yamesimama


 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito  ulitanda barabarani

ZIARA YA WAZIRI MKUU MHE. MIZENGO PINDA CHENGDU - CHINA

IMG_0119
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakipata maelezo kuhusu kiwanda cha kutengeneza maligafi za viwanda vya plastiki cha Hongda Chlor alkali Chemical Base cha Chengdu nchini China akiwa katika ziara ya kikazi Oktoba 22, 2013,. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdallah Kigoda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) IMG_0427
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa kampuni ya Dalian International ya China kwenye hoteli ya Shangri-la, Chengdu akiwa ktika ziara nchini China. Oktoba 22, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_0496
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akikagua eneo la Mradi wa umwagiliaji la Dujiangyan lililopo Chengdu nchini China akiwa kaika ziara nchini humo Oktoba 22,2013.(Picha naOfisi yaWairi Mkuu)
 IMG_0573
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akitia saini kitabu cha wageni baada ya kutembelea mradi wa umwagiliaji wa Dujiangyan uliopo Chengdu nchini China akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo   Oktoba 22, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, October 21, 2013

TUME YA WARIOBA YAOMBA MUDA ZAIDI

warioba_1_bc902.jpg
Tume ya Mabadiliko ya Katiba imeomba kuongezewa muda wa mwezi mmoja kutokana na ugumu wa kazi ya uchambuzi wa maoni yaliyotolewa na wananchi na asasi mbalimbali.
Tume hiyo inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba ilitakiwa kufanya kazi kwa miezi 18 kwa mujibu wa Sura ya 83 ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Maana yake ni kuwa Tume hiyo iliyoanza kazi Mei 1, mwaka jana ilitakiwa kukamilisha kazi yake Novemba 1, mwaka huu.
Ikiwa maombi hayo ya Tume yatakubaliwa ina maana watatakiwa kukabidhi ripoti yake Desemba 1, mwaka huu.
Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Augustine Ramadhan aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa wamepeleka serikalini maombi ya kuongezewa muda wa kufanya kazi.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 21, 2013

DSC 0057 aae29
DSC 0058 6a210

Sunday, October 20, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 20, 2013

.

.

KENYATTA ARUHUSIWA KUTOHUDHURIA BAADHI YA VIKAO VYA KESI


017113680_35400_1b04e.jpg
Mahakama ya ICC jana Ijumaa(18.10.2013)ilimruhusu kwa kiasi fulani Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake, ili kumpa muda wa kushughulikia majukumu ya kisiasa.
Kenyatta , ambaye alichaguliwa kuwa rais mwezi Machi mwaka huu, amekuwa akidai kwa muda mrefu sasa kuwa kesi hiyo mjini The Hague itazuwia uwezo wake wa kuiongoza nchi.
"Mahakama hiyo kimsingi inamuondolea Uhuru Kenyatta ulazima wa kuwapo wakati wote katika kesi dhidi yake inayoanza Novemba 12, imesema mahakama hiyo ya ICC katika taarifa, lakini ikasisitiza kuwa ni lazima afike kwa ajili ya ufunguzi wa kesi hiyo.
Majaji wamesema kuwa ruhusa ya Kenyatta inatolewa kwa misingi kwamba anaweze kutimiza majukumu aliyonayo kama rais wa Kenya, na sio kwasababu ya kutoa hadhi kwa kazi yake kama rais.
Atakuwapo wakati wa kutoa ushahidi
Mahakama hiyo iliyoko nchini Uholanzi pia inasisitiza kuwa Kenyatta anapaswa kuwapo wakati pande zote zitakapokuwa zinatoa taarifa zao za mwisho katika kesi hiyo, wakati wahanga wanatoa ushahidi wao na pia,iwapo kutakuwa na haja wakati wa kikao cha kutoa hukumu.

MSHAHARA WA RAIS KAA LA MOTO


jk 17ab9
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe kutaja hadharani mishahara ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, serikali imekataa kuizungumzia mishahara hiyo.
Msimamo wa Serikali kutotaja mishahara ya viongozi wakuu unatofautiana na utamaduni wa nchi nyingine kama Marekani, Afrika Kusini, Ufaransa na Kenya ambazo mishahara ya wakuu wake huwekwa wazi kwa umma.
Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema akiwa wilayani Igunga Mkoani Tabora, alisema Rais Kikwete anapokea zaidi ya Sh30 milioni kwa mwezi (sawa na Sh360 milioni kwa mwaka) ikiwa ni marupuru na mshahara kwa mwezi bila kodi, huku Pinda akipokea Sh 26 milioni kwa mwezi.
Akizungumza na Mwananchi kwa simu jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema kiongozi yeyote haruhusiwi kutaja mshahara wa mtu mwingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.
"Kuutaja mshahara wa mtu mwingine ni kinyume cha sheria na kosa, siyo utaratibu. Kwani wewe upo tayari watu waujue mshahara wako?" alihoji.

MATOKEO YA LIGI KUU YA UINGEREZA

2816039_orig_51785.jpg
Source: bongostaz

Friday, October 18, 2013

PAPII KOCHA, BABU SEYA...... NAFASI YA MWISHO, WANAHITAJI SALA NA DUA ZETU

 

Na Mwandishi Wetu

KITENDO cha Mahakama ya Rufaa kukubali kusikiliza marejeo ya hukumu ya kifungo cha maisha jela katika kesi iliyokuwa ikimkabili mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kimetafsiriwa kuwa ni kama wamepata nafasi ya mwisho ya kuweza kujinasua.


WARAKA WA PAPII KOCHA
Mahakama hiyo ilikubali ombi hilo hivi karibuni na kueleza kuwa marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa Oktoba 30, mwaka huu ikiwa ni miezi kadhaa baada ya Papii Kocha kutuma waraka wa kuomba msamaha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu ndiye aliyekubali kuufikisha kwa JK hivyo kuna madai kuwa huenda waraka huo ndiyo umezaa matunda.
 
WARAKA UMEZAA MATUNDA?
“Unajua ule waraka ulikuwa na maneno ya kuumiza sana. Inawezekana kabisa kuwa ulimfikia JK akaagiza suala hilo liangaliwe upya. Haina maana kuwa JK anaingilia sheria. Nadhani wanasheria wana vipengele vingi ambavyo vinaruhusu marejeo ya rufaa hiyo. Kilichopo hapa ni namna ya kuzitafsiri sheria kisha kuona kama rufaa hiyo inaweza kusikilizwa.

SAKATA LA UFOO SARO LACHUKUA SURA MPYA UPANDE WA WAKWE...!!!



UTATA wa risasi umegubika tukio la kifo cha mzazi mwenzake na mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro, marehemu Anthery Mushi, aliyejiua kwa kujipiga risasi. Utata huo umeibuka baada ya ndugu wa marehemu Mushi kushangazwa na kuhoji mazingira ya kifo cha ndugu yao anayedaiwa kujipiga risasi mbili kidevuni na kupoteza maisha papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana Msemaji wa familia hiyo ambaye pia ni kaka wa marehemu, Isaya Mushi alisema familia imebaki kizani juu ya kifo cha ndugu yao na kwamba anayejua siri nzito juu ya kifo hicho ni mzazi mwenzake, Ufoo.

Isaya, alisema mazingira ya kifo cha Mushi ni ya kutatanisha kwani baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi na madaktari, zilitolewa risasi mbili kichwani, huku wakihoji risasi ya pili.

Kwa mujibu wa wataalamu waliobobea katika silaha, ni vigumu mtu kujiua kwa risasi mbili katika eneo la kichwa kwa maelezo kuwa risasi moja inatosha kumaliza uhai wa mtu katika eneo hilo.

“Sisi kama familia bado tukio hili linatupa utata, hivyo tunaomba Jeshi la Polisi litumie busara katika kufanya uchunguzi wa kina kwani, Mushi haiwezekani akajipiga risasi kidevuni ikanasa kwenye ubongo, halafu akajipiga tena kidevuni upande wa kushoto… imetushangaza na hatuelewi tukio hili,” alisema Mushi.


Alisema wanafahamu fika maisha aliyoishi kijana wao kwani alikuwa ni mtaratibu, hivyo maamuzi aliyoyachukua yalikuwa magumu.

“Kijana wetu enzi za uhai wake alikuwa ni mtaratibu, hivyo maamuzi aliyoyachukua yalikuwa ni magumu mno na mwenye siri hiyo ni mzazi mwenzake Ufoo, tuna imani ataeleza,” alisema Mushi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...