Tuesday, October 01, 2013

VIJANA WANAVYOSAJILIWA KUPIGANIA AL SHABAAB

alshabaab-soldiers-in-training_495033_e5a43.png
Uchunguzi wa BBC umefichua ambavyo vijana husajiliwa kujiunga na kundi la kigaidi la Al Shabaab katika pwani ya Kenya.
Al Shabaab limekiri kufanya shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Westgate ambapo zaidi ya watu sitini waliuawa na mamia kujeruhiwa.
Uchunguzi wa BBC, unatizama ambavyo vijana wanafunzwa itikadi kali za dini katika kuwaandaa, kujiunga na kundi la Al Shabaab.
Vikao vya kuwasajili Vijana hao huanza na viongozi wa dini kutoa hotuba kwa vijana waisilamu wengi ambao wamesilimu.
Uchunguzi huo umebaini kuwa vijana hao ambao wanakuwa wamejitolea kupigania kile wanachosema ni dini, hupelekwa katika maeneo ya vijijini katika fuo za bahari kama sehemu ya kwanza ya safari yao kwenda Somalia.
Mmoja wa wahubiri hao kwa jina Makaburi, ametetea shambulizi lililofanywa dhidi ya Jumba la Westgate na kuwaua watu zaidi ya sitini akisema kwamba ilikuwa hatua sahihi.
Kulingana naye, ilikuwa sawa kwa sababu majeshi ya kigeni yanapigana nchini Somalia.
Jeshi la Kenya lilipeleka wanajeshi wake nchini Somalia,miaka miwili iliopita kupambana na kundi la Al Shabaab.
Wakati huohuo, maombi yanafanyika katika sehemu mbali mbali mjini Naiobi kuwaombea waathiriwa wa shambulizi hilo

Monday, September 30, 2013

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI MUTUNGI USO KWA USO NA VYAMA VYA UPINZANI VILIVYOUNGANA


MUUNGANO wa vyama vya siasa vya upinzani nchini, jana ulitinga ofisi za Msajili wa Vyama, Jaji Godfrey Mutungi, kwa nia ya kueleza dhamira yao ya kupinga Rais Jakaya Kikwete kuusaini Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
Vyama hivyo vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi, vinavyounda ushirikiano wa kisiasa wa kupinga Rais kusaini muswada huo, vilimfafanulia Msajili huyo kilichotokea bungeni hivi karibuni, kwa wabunge wa upinzani nje ya ukumbi wa Bunge, wakati wale wa CCM wakipitisha muswada huo pamoja na marekebisho yake.

Akizungumza na waandishi wa habari katika viunga vya viwanja vya Ofisi ya Msajili, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa ushirikiano huo, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema moja ya mapendekezo waliyompatia Msajili ni kutaka maridhiano ya kikatiba, hivyo Rais Jakaya Kikwete asisaini sheria hiyo.

“Tumefanya mazungumzo na Msajili, tulifika kumsabahi na kumweleza yaliyojiri bungeni kuhusu Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, mchakato ulianzia tume mpaka kura ya maoni ya katiba… Zanzibar haikushirikishwa, Serikali ilipeleka vipengele 6,” alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba alisema Oktoba 10 mwaka huu, ni siku ya kitaifa ya kupinga kusainiwa kwa Sheria hiyo na kwamba maandamano yatakayofanyika yatakuwa ya amani.

IJUE SABABU YA MKUU WA WILAYA YA MBULU KUWAPIGIA WANANCHI MAGOTI....!!!


Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya akiwa amewapigia wananchi magoti kwa maana ya kuonyesha unyenyekevu
Mbulu. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, Anatory Choya, amesema kuwa aliwapigia magoti wananchi wa Kijiji cha Hydom, ili kuonyesha unyenyekevu kwa wananchi hao aliodai walionekana kujazwa maneno ya uchochezi na wanasiasa ili wavuruge amani .

Alisema kutokana fujo zilizofanywa na baadhi ya wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika majuzi, kwa nafasi yake angeweza kuagiza hata Jeshi la Polisi kuwadhibiti watu, lakini misingi ya dini yake haimruhusu kumdhuru mtu zaidi ya kumwonyesha unyenyekevu.
 
 
Alisema hali hiyo ndiyo iliyomfanya kuamua kupiga magoti na kumshtakia Mungu.

MSIKILIZE MUIGIZAJI MAHIRI WA FILAMU NCHINI, LULU ALIVYOFUNGUKA KWENYE SEMINA YA FURSA KWA VIJANA JIJINI MWANZA

Angalia video hapo chini

ANGALIA NJIA RAHISI NA ZA KISASA ZA KUWAFUNDISHA WATOTO KUJUA KUSOMA NA KUANDIKA

 
Angalia video hapo chini

MAGAZETI YA LEO JUMATATU SEPTEMBA 30, 2013


DSC 0067 139a0
DSC 0068 4c367

ICC INAHARIBU MAHUSIANO YAKE NA AFRIKA - RAIS KIKWETE

zzzzzzzzzzzjk_f1554.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa mwenendo wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuhusu Bara la Afrika na viongozi wake, unainyima Mahakama hiyo nafasi kubwa ya kuungwa mkono na Bara la Afrika.
Rais Kikwete pia amelaani vikali mashambulizi yanayoongezeka dhidi ya vikosi vya kimataifa vya kulinda amani katika nchi mbali mbali duniani wakiwamo walinda amani wa Tanzania.

Rais Kikwete alitoa msimamo huo wa Tanzania mwishoni mwa wiki wakati alipohutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa (UNGA) mwaka huu, kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani.
Katika hotuba yake fupi na iliyowavutia wasikilizaji, Rais Kikwete alisema kuwa ni dhahiri kuanzishwa kwa ICC kutokana na Mkataba wa Rome kulikuwa ni hatua muhimu sana katika mfumo wa kimataifa wa kupambana na makosa ya jinai.
"Kwa hakika kuundwa kwa Mahakama hiyo kuliweka mfumo mzuri wa kuondokana na watu kutenda vitendo vya jinai na kuweza kuepukana na kuwajibika kwa vitendo hivyo na Mahakama hiyo ilianzishwa kwa kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na Afrika.
"Hata hivyo, muongo mmoja tu baada ya kuanzishwa kwa Mahakama hiyo, ni dhahiri kuwa mvutano umezuka kati ya ICC na Bara la Afrika. Sasa Mahakama hiyo inaonekana kama taasisi isiyojali maoni na msimamo wa Afrika, kwa mambo ambayo kwa maoni yangu, ni hofu halali ya Waafrika," amesema Rais Kikwete na kuongeza:
"Bado Mahakama hiyo inaendelea kupuuza maombi ya mara kwa mara ya Umoja wa Afrika. Ni jambo la kutia huzuni kuwa maombi ya kubadilisha muda wa kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Naibu Rais William Ruto yalipuuzwa na hata hayakujibiwa kabisa."

Sunday, September 29, 2013

TAARIFA YA ZITTO KABWE KUHUSIANA NA KUFUNGIWA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA

KUFUNGIWA MAGAZETI - WAHAFIDHINA SASA WANAONGOZA
Zitto Kabwe, Mb
Kwa mshtuko na masikitiko makubwa kuanzia jana jioni tumepokea taarifa za kufungiwa kwa magazeti mawili ya kila siku hapa nchini ya Mwananchi na Mtanzania. Serikali imechukua uamuzi huo kwa kutumia sheria ya kidikteta ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo Tume ya Jaji Francis Nyalali iliiorodhesha kama sheria kandamizi. Sababu zilizotolewa kuhalalisha uamuzi huu ni sababu zisizo na maana na ambazo Serikali ingeweza kufungua mashtaka ya kawaida kabisa mahakamani kushtaki magazeti hayo iwapo haikupendezwa na habari walizochapisha.

Moja ya sababu ya kufungiwa kwa gazeti la Mwananchi ni kuchapisha taarifa kuhusu mishahara ya Serikali. Serikali inasema habari hii ni siri. Serikali hii hii ambayo imesaini makubaliano ya kuendesha serikali kwa uwazi (Open Government Initiative) na kumwagiwa sifa na Rais Barack Obama wa Marekani inalifungia gazeti kwa kuandika habari za mishahara ya watumishi wa Serikali. Mishahara kuanzia mshahara wa Rais mpaka wa mtendaji wa Kijiji haipaswi kuwa jambo la siri.

ANGALIA VIDEO YA AUNTY EZEKIEL NA WEMA SEPETU WAKIPEANA BIRTHDAY LOVE NDANI YA HONG KONG.


ANGALIA VIDEO HAPO CHINI....
 

MTOTO ALIYEFARIKI NA KUZIKWA MIAKA MIWILI ILIYOPITA AONWA NA MAMA YAKE AKIWA HAI‏.

Mtoto Shabani Maulidi akiwa tayari melala kitandani katika hospitali ya wilaya ya Geita.
   Mama mzazi wa mtoto Shabani menye kilemba kichwani akiwa amepigwa bumbuazi  maeneo ya hospitali.




ROSE NDAUKA SASA KUZAA BILA NDOA, MAMA YAKE AGOMA

Staa wa filamu za Bongowood, Rose Ndauka ambaye ni mjamzito anadaiwa kuwa atazaa kabla ndoa mwezi Aprili, mwakani. Akizungumza na mwanahabari wetu, mchumbaa’ke, Malick Bandawe ambaye ni memba wa kundi la muziki la TNG alianika aya za Kurani kuwa katika Dini ya Kiislamu si ruhusa kufunga ndoa na mwanamke ambaye ni mjamzito kwani ni sawa na kufunga ndoa na watu wawili hivyo anamsubiri ajifungue kwanza. 
“Ni kweli mchumbaa’ngu hivi sasa ni mjamzito na anatarajia kujifungua mapema mwezi wanne, mwakani. “Kuhusu kufunga naye ndoa kwa sasa ni ngumu hadi ajifungue kwani kwa dini yetu (Uislam) si ruhusa kufanya hivyo lakini atakapojifungua tu tutafunga ndoa,” alisema Malick. Malick ambaye hivi sasa anatamba na Wimbo wa ‘Crazy Man’ alisema kuwa ana furaha kubwa kuitwa baba mtarajiwa na anamuomba Mwenyezi Mungu Rose ajifungue salama kwani anampenda kupita maelezo. Baada ya kuzungumza na Malick, gazeti hili lilimtafuta mama wa Rose Ndauka, Batuli kufungukia ishu ya mwanaye kubeba ujauzito kabla ya ndoa ambapo aligoma kuzungumza kwani hakubaliani na suala hilo.

WANAWAKE 8000 NCHINI NIGERIA WAANDAMANA KUISHINIKIZA SERIKALI IWASAIDIE WAOLEWE

  Nigeria ina upungufu wa wanaume wa kuoa kiasi kwamba wanawake wanaotamani kupata wenza na kutengeneza familia wameamua kuchukua hatua.  
Zaidi ya wanawake elfu 8 walio single jana wameandamana kutokana na upungufu wa wanaume wa kuwaoa.  
Lengo la maandamano yao ni kuishinikiza serikali kuwasaidia waolewe, kivipi? (Ndio swali hata mimi nimejiuliza!)  
Wanawake waliojikusanya na kuandamana ni mkusanyiko wa 5380 waliopewa talaka, 2200 ni wajane 1200 yatima, na 80 wengine.  
Wanawake hao wamedai kuwa hawana uwezo hata wa kununua chakula cha siku kwa sababu hawana wanaume wa kuwasaidia ndio maana wanahitaji wanaume wa kuwaoa na kuwasaidia mahitaji yao.  
  SOURCE: NAIJA GISTS

MATOKEO YA LIGI KUU YA UINGEREZA LEO JUMAPILI

Stoke-City-Vs-Norwich-City_81e66.png
Stoke City 0 - 1 Norwich City
Timu ya Norwich City imeweza kupata goli hilo katika dk ya 34 na mfungaji alikuwa ni Jonathan Howson. mchezo huo ukiluwa mzuri lakini mpaka mpira unamalizika matokeo yaliendelea  kuwa Stoke City 0 - 1 Norwich City.
Endelea kuifuatilia mjengwablog kwa matokeo ya mchezo baina ya Sunderland na Liverpool ambao mpaka sasa bado hawajafungana na ni kipindi cha kwanza.

KENYA: MAAFISA WALIKUWA NA TAARIFA

westgate 34bc1
Mawaziri wa serikali walipokea taarifa kuhusu tisho la mashambulizi ya kigaidi kabla ya kundi la Al Shabaab kushambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.


Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi zilizofichuliwa, zilionyesha maelezo ya mipango ya mashambulizi hayo kufanyika Nairobi au mjini Mombasa.
Taarifa zinazohusianaKenya
Mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walikuwa wamefahamishwa kuhusu tisho la kufanyika shambulizi la kigaidi.
Watu 67 walifariki na mamia kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi ambalo Al Shabaab walikiri kulifanya Septemba 21 mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la Daily Nation, mawaziri walipokezwa taarifa za kati ta yarehe 13 na 20 kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulizi kadhaa ya kigaidi mjini Mombasa na Nairobi.

TAMKO LA SERIKALI LA KUYAFUNGIA MAGAZETI YA MWANANCHI NA MTANZANIA

DSC_0068_b4d0a_d830f.png
DSC_0066_048af_a3496.png
Serikali imeyafungia kutochapishwa Magazeti ya MWANANCHI na MTANZANIA kuanzia 27 Septemba, 2013 kutokana na mwenendo wa magazeti hayo kuandika habari na makala za uchochezi na uhasama kwa nia ya kusababisha wananchi wakose imani kwa vyombo vya dola hivyo kuhatarisha amani na mshikamano ulipo nchini.
Gazeti la MWANANCHI limefungiwa kutochapishwa kwa siku kumi na nne (14) kuanzia 27 Septemba, 2013. Adhabu hii imetangazwa kwa Tangazo la Serikali (Government Notice) Namba 333 la tarehe 27 Septemba, 2013.


Gazeti la MWANANCHI limepewa adhabu hiyo kutokana na hivi karibuni kuchapisha habari zenye mwelekeo wa
uchochezi na uvunjifu wa amani, mfano tarehe 17 Julai, 2013 katika toleo Namba 4774 ilichapisha habari isemayo "MISHAHARA MIPYA SERIKALINI 2013" kwa kuchapisha waraka uliozuiliwa kwa matumizi ya vyombo vya habari waraka huo ulikuwa wa Siri haukupaswa kuchapishwa Magazetini.
Aidha, katika toleo la Jumamosi, tarehe 17 Agosti, 2013 lilichapisha habari yenye kichwa kisemacho "WAISLAM WASALI CHINI YA ULINZI MKALI" habari hiyo ilikolezwe na picha ya mbwa mkali mwenye hasira.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...