Sunday, September 01, 2013

MECHI ZA LEO JUMAPILI LIGI KUU UINGEREZA...!!!

prediksi-liverpool-vs-manchester-united-epl-2013-14_b42ff.jpg
15:30 Liverpool vs Manchester United

West-Brom-v-Swansea-1727337_33482.jpg
15:30 West Bromwich Albion vs Swansea City

18:00 Arsenal vs Tottenham Hotspur

Saturday, August 31, 2013

TAZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA ''FOOLISH AGE'' YA ELIZABERTH MICHAEL (LULU) MASHABIKI WAMTUNZA CHUNGU CHA PESA


 


 
 
 
 
 
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .

DIAMOND NA LINAH WANASWA WAKICHOMBEZANA NDANI YA GARI...!!!






Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.

WADAU WA BLOG YA JAMBO TZ, PENDEKEZA BLOG YAKO HII IINGIE KATIKA SHINDANO LA TANZANIA BLOGS AWARDS LEO


Jambo Tz Blog tunapenda kuwashukuru wasomaji wetu wote kwa kufuatilia habari zetu za kila siku pia kwa kutoa maoni yenu mara kwa mara ili kuboresha zaidi blog hii kwa maslahi ya jamii yetu ya kitanzania. Pia tunapenda kuwataarifu kuwa:-

Tanzanian Blog Awards wamefungua shindano la kutafuta blog bora 2013 ambazo zimewekwa katika makundi mbalimbali, lakini tunaomba uipendekeze blog hii ili iingie katika tuzo hizo katika vipengele vifuatavyo:-

Best General Blog
Best News Blog
Best Educational Blog
Best Creative Writing Blog
JINSI YA KUPENDEKEZA
Mapendekezo yote yatatumewa kwa E:mail peke yake kwa kufuata hatua zifuatazo.
Nenda eneo la subject utaandika jambotz8.blogspot.com
Nenda eneo la uwanja wa ujumbe utaandika vipengele ambavyo blog hii inashindania ambavyo ni   Best Newcomer Blog,
                         Best News Blog,
                         Best General Blog,
 Best Educational Blog,
 Best Creative Writing Blog
Andika zote kwa pamoja na Baada ya hapo tuma kwenda nomination@bloggersassociationoftanzania.com au tanzanianblogawards@gmail.com

Shindano hili limeanza tangu tarehe 17.08.2013 na litaisha tarehe 02.09.2013
**************************************************************************



NOMINATE JAMBO TZ  BLOG FOR THE 2013 TANZANIAN BLOG AWARDS
How to nominate(E.mail)

Subject: jambotz8.blogspot.com Body:  
            Best Newcomer Blog,
            Best News Blog,               
            Best General Blog,
Best Educational Blog,
Best Creative Writing Blog
Send your nomination to Tanzanian Blog Awards Emal nomination@bloggersassociationoftanzania.com  or to tanzanianblogawards@gmail.com

·        Please include a genuine email address (spam free), just in case they need to confirm identity the link to your nominations post.
·        Nominations will be accepted from August 17, 2013 at  12:01AM  until to September 2nd, 2013 1:59pm Eat Africa Time 

Tunatanguliza shukrani za dhati kwa wale wote watakaopendekeza na kuipigia kura blog hii ili iweze kushinda katika shindano hili. 
Jambo Tz, Blog Bomba Ya KiTanzania

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI AGOSTI 31, 2013

DSC 0114 8c385
DSC 0115 9c65f
DSC 0116 3ab89

SERIKALI YASALIMU AMRI YA WABUNGE

bunge_802dc.jpg 
Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa mwaka 2013, jana ulipita kwa mbinde bungeni mjini Dodoma, huku Serikali ikisalimu amri kwa wabunge na kukubali kurekebisha baadhi ya vifungu vyake.Bila kujali tofauti zao za kisiasa, wabunge jana walisimama kidete na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, wakitaka sheria hiyo imlinde mzawa badala ya mwekezaji.

Moto huo wa wabunge uliwalazimisha Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kusalimu amri na kukubali mapendekezo ya wabunge.

Msimamo wa wabunge hao katika kuibana Serikali, pia ulililazimisha Bunge kutengua kanuni zake na kuendelea na shughuli za kupitia muswada huo hadi saa 7:35 mchana, badala ya kusitishwa saa 7:00 kwa ratiba ya kawaida.
Serikali ilikubali mapendekezo ya wabunge hao na kurekebisha vifungu ambavyo sasa vinampa mmiliki wa ardhi itakayotangazwa eneo la umwagiliaji kuwa mwanahisa na kulipwa fidia.

M23 YATANGAZA KUSITISHA MAPIGANO KURUHUSU UCHUGUZI

m23_2fb74.jpg
Kundi la waasi wa M23 katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa linasimamisha mapigano mara moja, kuruhusu uchunguzi juu ya makombora yaliyovuka mpaka na kuanguka katika nchi jirani ya Rwanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.


Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.

UNA UHAKIKA NA MBAVU ZAKO? HEBU ANGALIA VIDEO HIZI UCHEKE PEKE YAKO

Chek nyingine kwa kubofya hapa.............. http://jambotz8.blogspot.com/p/vichekesho_5190.html

ANGALIA ALICHOFANYA NAY WA MITEGO WAKATI CHID BENZ YUPO JUKWAANI


Friday, August 30, 2013

MAGAZETI YA LEO IJUMAA AGOSTI 30, 2013


DSC 0078 77901
DSC 0079 4f4bd
DSC 0080 cea9f
DSC 0081 8f173

DIAMOND AMKABIDHI MZEE NGURUMO GARI AINA YA FUNCARGO

DIAMOND SHOW 020-1 8998c
Msanii Diamond Platnum amefanya kufuru usiku huu kwa kutoa zawadi ya Gari kwa Mzee Ngurumo Mwanamziki wa miaka mingi na mkongwe nchini aliyestaafu majuzi kufanya kazi za mziiki.
Tukio hilo limetokea usiku huu ndani ya ukumbi wa SERNA HOTELkatikati ja jiji la DSM ambapo Diamond Platnum anazindua video yake ya wimbo wa #one fun.
DIAMOND SHOW 025 b03d6
Mzee Ngurumo amesema"Haamini macho na masikio yake,hanachakusema zaidi ya ASANTE kwa msanii huyo"Lakini pia amesema hajui hata mke wake atasemaje baada ya kumwona akiingia na gari ndani ya nyumba yake.
Mzee ngurumo amekuwa na matatizo ya kiafya siku za karibuni nakupelea kustaafu mziki kabisa.Wazee wa msondongoma ndio wanajua makali ya Mzee Ngurumo.

"KAJALA NDIO KILA KITU KWANGU KWA SASA, YEYE NI ZAIDI YA MUME KWANGU"......WEMA


KASUMBA ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa, bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea mtupu.
Wema Sepetu na Kajala Masanja.
Wema alifikia hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her everywhere with me. I hope that’s how they out each other.”
Aliandika kimombo, alimaanisha nini?

Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu wawe wote.
Kajala amjibu
Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa, kama ni hivyo yeye hana la kusema.
Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.


Kwa nini Wema aseme hivyo?

Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.

KATIBA YATAKIWA IRUHUSU WAFUNGWA KUSHIRIKI TENDO LA NDOA NA WENZA WAO ILI KUPUNGUZA USAGAJI NA USHOGA GEREZANI

BAADHI ya wadau wa masuala ya jinsia wamependekeza kuwa ili kukabiliana na masuala ya ushoga na usagaji, Katiba Mpya iruhusu wafungwa kukutana kimwili na wenza wao, kwani vitendo hivyo chanzo chake ni gerezani hasa kwa vijana wanaokula 'unga' na kuvuta bangi.




Hayo yalisemwa juzi kwenye kikao cha maboresho ya Rasimu ya Katiba Mpya, kilichofanyika siku tatu kwenye Kijiji cha Makaburini kwa kuratibiwa na asasi ya Tanzania Environment Relatives Organization (TERO) ya mjini Korogwe kwa ufadhili ya Shirika la The Foundation for Civil Society la jijini Dar es Salaam. 

"Mfungwa akubaliwe kukutana kimwili na mume au mke wake. Kitendo cha kuwakatalia wafungwa kukutana kimwili na wake au waume zao kunachochea vitendo vya kufanya mapenzi ya jinsia moja na vijana wengi wameharibikia gerezani na kujikuta vitendo hivyo vinaingia mitaani"

RAIS KIKWETE AMUOMBA RAIS WA UGANDA AONGEE NA KAGAME ILI KUMALIZA UGOMVI ULIOPO


RAIS Jakaya Kikwete, amewasiliana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ili azungumze na Rais wa Rwanda, Paul Kagame kwa nia ya kumaliza mvutano wa maneno kati yao kwa busara.
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alisema hayo jana bungeni, alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Upinzani bungeni, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema).
 
“Tunataka suala hili limalizike kwa njia ya busara, ili watu waendelee kuchapa kazi, ninaamini busara zitatumika kumaliza tatizo hilo,” alisema.

Akiuliza swali katika kipindi cha maswali ya Papo kwa Hapo kwa Waziri Mkuu jana, Mbowe alitaka kujua kauli ya Serikali na mikakati iliyopo kupata suluhu katika mvutano wa maneno uliojitokeza kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame.
 
Pia Mbowe alitaka Serikali kuunda jopo la ushawishi wa kimataifa, kutokana na Rwanda kuonekana kushawishi nchi za Uganda na Kenya, jambo ambalo linaashiria kuitenga Tanzania katika shughuli mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
 
Kwa mujibu wa Mbowe, kitendo cha marais wa Kenya, Uganda na Rwanda kukutana katika mikakati ya kuanza kutumia bandari ya Mombasa ambayo ingekuwa ya nchi za Afrika Mashariki, ni dalili kuwa Tanzania imeanza kutengwa.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...