Saturday, May 18, 2013

DADA WA DIAMOND "ESMA" AZUNGUMZIA JUU YA HARUSI YA DIAMOND NA PENNY


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqauc854yv2PrYw-bH3bOCkwEGbb-8ERY5V3dCosbi_ICE5-UpO4U43B3LeqSrSiO4NSVr80ZZySDQv2QX2Vik0kITUUu3Bw8CBMmq31Snt4dIClzxcu912csTxh2z5C9Bx-EzdUQw-I0/s1600/diamond.jpg
Esma Abdul ambae ni dada yake staa wa Tanzania, Diamond Platnums, amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya harusi ya Diamond ambae anatarajiwa kumuoa mtangazaji wa TV aitwae Penny.

Esma ambae anaishi nyumba moja na kaka yake amesema, "Tumemkubali sana wifi yetu na tunampenda kwa sababu mtu yeyote mimi nitakaetambulishwa siwezi nikamkataa, manake nikimuingilia kwenye mapenzi yake na yeye ataniingilia kwenye mapenzi yangu."
Huu ni mwezi wa tano toka Esma amjue wifi yake ambae ni Penny, anasema nyumbani amekubalika na mipango ya harusi inaandaliwa japo hajui ni lini itafanyika, manake hiyo ni siri kwa sasa. 

Zaidi ya wiki tano zilizopita, Diamond aliongea na kusema ndoa yake imekaribia kufungwa na huyo mkewe mtarajiwa ambae ni mjamzito lakini pia akathibitisha kumnunulia gari la kutembelea aliloliagiza nchini Japan - Hyundai IX 35.

Mpaka sasa Diamond Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa Tanzania alieandikwa sana kwenye internet 2012, ameshaingia kwenye headlines za kuwa mapenzini na mastaa wa kike Tanzania kipindi cha nyuma kama Jokate, Wema Sepetu na wengine. 

KATI YA HAWA MMOJA ATATANGAZWA KWENDA BBA.


Jacqueline Pentzel ‘Jack wa Chuz’, Jacqueline Patrick ‘Jack Patrick’ (pichani) , Wema Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ na Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’  mmoja wapo ataungana na mwanaume kuiwakilisha Bongo kwenye Shindano la Big Brother Africa 2013 linalokwenda na kikolombwezo cha The Chase. 

 
Jack Pentezel
Kwa mujibu wa chanzo chetu (tunaficha jina lake), mastaa hao wa kike, mmoja ndiye ataibuka mshiriki kwa mwaka huu ambapo atakaa ndani ya mjengo kuanzia Mei 26, 2013 ambapo shindano litaanza rasmi. 
 
Jack Patrick
“Mimi nawamegea tu kwamba kati ya Wema, Baby Madaha, Jack wa Chuz na Jack Patrick  mmoja wao anakwenda Big Brother mwaka huu.
 
Wema sepetu
“Halafu ninachojua mimi, mshiriki ameshatumiwa taarifa kutoka Multi Choice, ila tatizo wale jamaa wanataka mtu msiri sana, mshiriki hatakiwi kumwambia mtu mpaka siku atakapoondoka,” kilisema chanzo chetu.
Risasi Jumamosi lilipiga kiguu hadi Ofisi za Multi Choice jijini Dar na kuulizia Mbongo anayekwenda, likakumbana na majibu haya:

Baby Madaha
“Sisi pia hatujui. Unajua ilivyo ni kwamba huwa tunatuma majina, sifa na anuani za watu kama watano kule Sauzi, halafu wao wanaangalia vigezo vyao, anayeshinda anataarifiwa kutoka kulekule bila sisi kujua,” alisema mtumishi mmoja ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Risasi Jumamosi juzi Alhamisi liliongea na Jack wa Chuz ambaye alisema aliwahi kuombwa kushiriki shindano hilo kwa sababu ya ushombe wake lakini hakuweka wazi kama alijaza fomu za maombi au la!
Aidha, Baby Madaha alipoulizwa alikiri kujaza fomu za kukusudia kushiriki siku za nyuma akiwa sambamba na Wema lakini akasema hajui nani kashinda ingawa lazima mshiriki ameshapatikana kati yao.
“Nasikia mshiriki anatakiwa kujijua wiki tatu au mbili kabla. Kwa hiyo atakuwa tayari anajijua, inakuwa siri ya mtu, hakuna anayeweza kujitaja kwa watu,” alisema Baby Madaha.
Simu ya Jack Patrick haikuwa hewani siku hiyo huku watu wake wa karibu wakisema yupo nje ya Bongo kibiashara zaidi. Simu ya Wema muda mwingi iliita bila kupokelewa hadi mpigaji akachoka.
Kwa upande wa wanaume, wanaotajwa kushiriki shindano hilo mwaka huu ni staa wa sinema za Bongo, Hemed Suleiman ‘PHD’, nyota wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’ na aliyewahi kuwa Mtangazaji wa Clouds TV, Rommy Jones ambaye ni ndugu na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’. 

MAMA SHARO... AAMBULIA PATUPU KWENYE AKAUNTI YA MWANAYE.


Maskini! Mama mzazi wa aliyekuwa msanii maarufu wa vichekesho na muziki Bongo, Marehemu Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufunga safari kutoka Tanga hadi Dar kwa ajili ya kushughulikia fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya mwanaye na kuambulia patupu.


Akizungumza na Risasi Jumamosi juzi kwa njia ya simu, mama huyo alisema kwa kuwa tayari ameshafungua mirathi, ilibidi aanze kushughulikia suala la benki ambapo alianzia kwenye akaunti za marehemu lakini alipofuatilia hakukuta hata senti tano.

“Namshukuru Mungu kwa yote maana nimerudi Tanga kama nilivyotoka na nauli yangu kwani sikukuta fedha yoyote kwenye akaunti zote za Sharo ila inawezekana alichukua fedha zote kwa ajili ya manunuzi yake kabla ya kifo.
“Huwezi jua kwani alikufa kwa ajali hivyo ni lazima vitu vyake vingi vibaki gizani,” alisema mama Sharo na kuongeza:
“Sioni haja ya kumlaumu mtu zaidi ya kumuachia Mungu ambaye ndiye muweza wa yote, hapa duniani sote tunapita.”
Sharo Milionea alipatwa na umauti Novemba mwaka jana kwa ajali ya gari katika eneo la Songa- Maguzoni wilaya ya Muheza mkoani Tanga wakati akiwa safarini akitokea Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao, Kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

NEY WA MITEGO KUITWA BABA SOON, HUYU NDO MAMA KIJACHO WAKE.


So much is happening in the Bongo Flava scene!! TID anataka kuoa, Nurah anatarajia kufunga ndoa June 8 na sasa Nay wa Mitego naye anategemea kuitwa baba, basi raha tupu!!

b89c11b6b7ab11e286be22000a9f139c_7

0bb7758abce711e2935222000a1fb825_7
Kupitia Instagram Nay aka True Boy ambaye hivi karibuni amekuwa dhahabu kwenye show za promotion za makampuni ya simu, amekuwa akishare picha za msichana ambaye kwa mujibu wake ni ‘Mama Kijacho Wake’. “Mic u mama kijacho wanguuuuuuuu…” aliandika hivi karibuni kwenye picha ya msichana huyo.

NISHA AMKIMBIZA WEMA KWA KUMILIKI NYUMBA YA KIFAHARI, HII NDO NYUMBA YA NISHA YENYE THAMANI YA MILIONI 95.

Unakumbuka zile habari za Wema Isaac Sepetu kununuliwa jumba la kifahari na bilionea mmoja Kijitonyama, Dar? Sasa zimegeukia kwa staa wa sinema za Kibongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ambaye naye kuna madai mazito ya kuhongwa nyumba.
Ilikuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo gazeti hili lilipokea ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ‘sms’ kutoka kwa chanzo chake.
HABARI ILIVYOANZA
Chanzo: Hivi ninyi mna habari?
Risasi Jumamosi: Nyingi tu lakini kama una ya kwako itatufaa sana.
Chanzo: Kwa taarifa yenu Nisha kanunuliwa bonge la mjengo hapa Kijitonyama karibu kabisa na Kituo cha Polisi cha Kijitonyama ‘Mabatini’.
Risasi Jumamosi: Nani kamnunulia?
Chanzo: Nasikia ni bilionea mmoja mwenye fedha zake hapa Dar es Salaam, kainunua kisha kamhonga Nisha kwa sababu ni mpenzi wake.
Risasi Jumamosi: Tunashukuru kwa taarifa, kaa mkao wa kula itaruka hewani mara moja baada ya upelelezi wetu.

RISASI LATUA KIJITONYAMA
Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilisaga soli hadi maeneo hayo na kuanza kugonga geti moja baada ya lingine hadi lilipofanikiwa kuinasa nyumba hiyo huku Nisha akiwa ndani kapumzika.
Msichana aliyejitambulisha kuwa ni dada wa kazi au hausigeli kwa lugha laini ndiye aliyetoboa siri kuwa ni kweli staa huyo yupo ndani na amehamia mahali hapo muda si mrefu.

NAY WA MITEGO AMTUPIA KIJEMBE CHA NGUVU DIAMOND PLATNUMZ

Katika hali ya Amani kimuziki Msanii Nay wa Mitego amemrushia
vijembe Msanii mwenzake
Diamond Platnumz Jionii ya Leo......''
Niliamua kumwendea hewani Nay wa Mitego Kujua kajianda vipi
kuhusiana na Show ya kesho
Usiku Darlive......Na Mnukuu Nay wa Mitego akifunguka
 baada ya swali aliloulizwa,
Nay''Napenda kumwambia bwana mdogo Diamond kuwa kesho
akae tayari kwa kuwa naenda kuandika
Historia Mpya Darlive,Nataka watanzania wote wajitokeze waje
 kuona navyomkalisha mbana pua
na wavaa nguo za dada zao wanaojidai kwenda sawa na utandawazi......''
Nay alizidi kufunguka kuwa kesho ndo utakuwa mwisho wa
Diamond na kumthibiishia
kuwa Hip Hop ndo muziki unaolipa na wenye maana zaidi......!!

Hayo ndo maneno aliyoyatoa Nay dakika chache zilizopita
alivyopigiwa na Mwandishi wa This Is Diamond
Kuhusiana na Show kubwa kesho Darlive......

Stay Tuned Nitamuenda Hewani The Kid From Kigoma baada ya
kumfikishia ujumbe huu wa Nay...
Je maneno hayo kakubaliana nayo....?
 Stay here kusubiria jibu la Diamond Juu ya ujumbe huu.....!!

SIMBA NA YANGA LEO NDIO LEO.... UPO UPANDE GANI....???


Ubabe ubabe tu. Usemi huu unaweza kutumika leo wakati miamba ya soka Tanzania, Simba na Yanga itakaposhuka dimbani kuumana katika pambano la kuhitimisha Ligi Kuu litakalopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo baina ya mahasimu hao una sura tatu tofauti, kwanza kila timu inahitaji kuvuna pointi tatu ili kulinda heshima yake, kulipa kisasi na kuendeleza rekodi.

Yanga inasaka ushindi ili kunogesha ubingwa wake wa Ligi Kuu msimu huu, pia kulipa kipigo cha mabao 5-0 ilichokipata kutoka kwa Simba katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye uwanja huo Mei 5, 2012.

Nao Wekundu wa Msimbazi, baada ya kupokonywa taji na kuambulia nafasi ya tatu, sasa wana kiu ya kutaka kuboresha rekodi yao ya kumtundika mpinzani wake Yanga mabao mengi zaidi katika mechi mmoja.

Kocha wa Yanga, Ernie Brandts akizungumzia matarajio yake kuelekea mtanange huo alisema:

“Bila kuifunga Simba ubingwa hauwezi kunoga, ndiyo maana tumejidhatiti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri Jumamosi.”

Kwa upande wake Liewig alisema: “Tunajua Yanga ni Bingwa, lakini sisi pia tuna mipango yetu kama Simba ambayo ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa mwisho na hilo nina uhakika litafanikiwa.”

Ubora wa vikosi:
Yanga itaingia uwanjani ikijivunia kikosi chenye wachezaji wazoefu katika mechi za ligi, lakini Simba itawategemea chipukizi wake walioitakatisha vyema mzunguko wa pili wa ligi Kuu, hususan Haruna Chanongo na Rashid Ismail.

Kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima atakuwa ‘mpishi’ mkuu wa mabao ya Yanga kwenye kipute hicho, kama itakayokuwa kwa Amri Kiemba wa Simba ambaye kiwango chake cha juu msimu huu kimewaacha wengi midomo wazi.

Rekodi za jumla:
Yanga na Simba zimekutana mara 100 katika mechi mbalimbali za Ligi Kuu, kati ya hizo Yanga ilishinda mara 37, Simba mara 32, huku mara 31 zikitoka sare.

Zaidi ya hapo, Yanga imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara 23 wakati Simba imefanikiwa kunyakua taji hilo mara 18.

SERIKALI YAAHIDI KUWACHUKULIA HATUA KALI VIONGOZI WA WIZARA YA ELIMU WALIOSABABISHA UBOVU WA MATOKEO YA FORM FOUR...!!

Serikali imeahidi kuwajibisha watendaji watakaobainika kwenda kinyume katika uingizaji wa mfumo mpya wa usahihishaji mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012, ambao matokeo yake yamefutwa. 


Tume ya Uchunguzi inayotarajiwa kukamilisha maelezo yake hivi karibuni, ilipewa hadidu za rejea ambazo ni kubainisha sababu za matokeo hayo mabaya, kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua. 
Akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu, Magdalena Sakaya (CUF), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alisema kinachosubiriwa sasa, ni maelezo ya kina ya Tume ya Taifa aliyoiunda kuchunguza matokeo hayo.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu, Tume hiyo haijakamilisha kazi yake,  lakini muda si mrefu itakuwa imekamilisha na kuwasilisha maelezo ya kina yatakayoipa Serikali majibu kwa maeneo yote.
 
“Tusubiri kidogo, muda si mrefu tutakuwa tumekamilisha kazi …na kama wapo watu waliosababisha jambo hili, wala haitakuwa tatizo hata kidogo kuchukua hatua za kuwawajibisha. Ni dhahiri kwamba suala hili si dogo,”alisema Waziri Mkuu.

Majibu hayo ya Pinda yalitokana na maswali ya Mbunge Sakaya, ambaye alisema uamuzi wa Serikali wa kufuta matokeo hayo kutokana na kubainika kulikuwa na mabadiliko ya upangaji wa alama bila kuandaa wanafunzi, si jambo dogo.

ELIMU YA SHULE ZA MSINGI ITAKUWA NI MIAKA 10 BADALA YA 7...!!

RASIMU ya Sera ya Elimu na Mafunzo nchini inapendekeza kuunganisha elimu ya msingi na sekondari ya kawaida ya sasa ili kuunda elimu-msingi itakayotolewa kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2018, imefahamika. 
Rasimu ya kwanza ya Sera hiyo imeshakamilika na sasa wadau mbalimbali wanatoa mapendekezo yao kuiboresha, kabla ya kupelekwa bungeni ili kutungiwa sheria.
Aidha, mikakati hiyo itakayotekelezwa ni kuhuisha muundo na utaratibu mpya wa elimu na mafunzo kwa kuhakikisha kila mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na mitano anapitia elimu ya awali kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja kabla ya kujiunga na elimu-msingi.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alithibitisha kwa gazeti hili wiki hii mjini hapa kuhusu kukamilika kwa rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2013.
“Ni kweli Sera hiyo imekamilika baada ya kuandaliwa kwa miaka mitatu. Imepita kwa wadau mbalimbali, mashuleni, vyuoni na katika taasisi mbalimbali nchini ambao wametoa maoni yao. “Jumapili (kesho) tunatarajia kuwa waheshimiwa wabunge nao watapata fursa ya kuijadili na kutoa maoni yao katika semina iliyoandaliwa maalumu kwao,” alisema Mulugo katika Viwanja vya Bunge.
Alisema baada ya maoni hao ya wabunge, watapeleka Rasimu hiyo kwa mamlaka husika kwa ajili ya andiko la mwisho kabla ya kupelekwa katika Bunge lijalo ili itungwe sheria kuhusu Sera ya Elimu na Mafunzo.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 18.05.2013

DSC 0261 1a54f

DSC 0262 5766d

SUGU, PROPESA JAY, ROMA MKATOLIKI WAPIGIWA DEBE KUALIKWA KATIKA SHOW YA LADY JAYDEE KUFUATI, BAADA YA MATONYA NA WENGINE KUMTOSA.


 Joseph Mbilinyi aka "Sugu"
 Joseph Haule aka Proffessor Jay"
 R.O.M.A Mkatoliki

 Lady Jay Dee mwenyewe
 K na D wa Maujanja Saplayaz (Kulwa na Dotto)
WAKATI wapenzi wa muziki wa kizazi kipya nchini wakisubiri kwa hamu kubwa show kali ya Mwanadada Judith Wambura "Lady Jay Dee" ya kuadhimisha kutimiza miaka 13 katika game ya Muziki huo na kutokana na hali ambayo imeendelea kwa baadhi yawasanii mbalimbali waliokuwa wametajwa kushirikiana naye katika show hiyo kujiengua na kutoa sababu kadhaa za kutoshiriki katika Show hiyo (TID, Linah, Barnaba na Matonya)

DIAMOND ATOA SABABU ZA YEYE KUWA KICHECHE......!!!

 KWA mara ya kwanza nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond' ameacha gumzo London, Uingereza baada ya kueleza sababu za kwa nini ni kiwembe?
Akifunguka katika mahojiano maalum wiki iliyopita na Kipindi cha Sporah Show cha runingani alipokuwa kwenye ziara ya kimuziki nchini humo, Diamond alizungumza ishu kibao za kimapenzi hasa juu ya msururu wa wanawake ambao tayari ametoka nao.
ASISITIZA ANASUBIRI MTOTO

Kabla ya yote, staa huyo alisisitiza kuwa muda si mrefu anatarajia kupata mtoto kutoka kwa mpenzi wake wa sasa, Peniel Mungilwa ‘Penny’ akimaanisha kuwa ni mjamzito, kinyume na msichana huyo ambaye hivi karibuni alimshangaa Diamond kueneza habari hizo.
KWA NINI ANAPENDA KUBADILISHA WANAWAKE?

Diamond: Mimi ni binadamu kama binadamu wengine wa kawaida. Nampenda mwanamke anayenipenda na kuniheshimu. Ikitokea mikwaruzano huwa mimi nakaa pembeni, natafuta sehemu nyingine. Wakati mwingine mimi ndiye huwa naachwa.
KWA NINI MSURURU NDANI YA KIPINDI CHA MIAKA MITATU?

Diamond: Nikiwa na mtu nikiachana naye naonekana nina matatizo kwa sababu wakati mwingine nakuwa na wanawake wenye majina. Siwezi kukaa bila uhusiano na nakuwa wazi kwa sababu lazima itajulikana tu na kuandikwa kwenye magazeti. Kuna kipindi nilikaa miezi sita bila kufanya kitu chochote (mh!). Lakini nikianza (uhusiano), nikihama naonekana msumbufu.

UWT MBEYA WAMJIA JUU MCHUMBA WA DKT SLAA.


Dkt Slaa akiwa na mchumba  wake Bi Bi.Josephine Mushumbusi Kushoto
Na Esther Macha, Mbeya
UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa
mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri .
Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya
Vwawa Mkoani hapa.

Friday, May 17, 2013

WANAFUNZI WA CBE, VETA, UDSM WAJIUZA......!!!

Wanafunzi wa kike wa chuo kikuu cha Dar es salaam [UDSM],Chuo cha elimu ya biashara [CBE]na chuo cha mamlaka ya Elimu na ufundi  stadi [VETA],Dar es salaam ,wamefikishwa katika mahakama ya jiji samora wakidaiwa kufanya biashara ya kuuza mili yao.

Washitakiwa hao waliokamatwa  katika eneo la kona Baa Ambiance Sinza wilayani kinondoni ambao ni miongoni mwa wanawake 35 wanaodaiwa kufanya biashara hiyo na wote walifikishwa mahakamani hapo.

Kesi hiyo ilikuwa chini ya hakimu Willian Mtaki ambapo muendesha mashitaka,bwana John Kijumbe,alisema wasichana hao walikamatwa katika mazingira tofautitofauti.

Wanafunzi hao ni Yasinta Kilimo mwenye miaka 21 CBE mkazi wa upanga,Morin Masatu miaka 19 UDSM,mkazi wa kinondoni na mwanafunzi wa VETA aliyefahamika kwa jina moja la Khadija.

“Nilikwenda pale baa kuchukua simu yangu ambayo ilipotea hivyo waliniita nikaichukue ndipo askari wa jiji wakanikamata,”Alisema Khadija akijitetea.

Kwa mujibu wa bw. Kijumbe washitakiwa  hao wamekosa dhamana baada ya kushindwa kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili au kulipa faini ya kulipa sh. 200,000.

POLISI YAWATIA MBARONI KANGAMOKO ..... RIPOTI KAMILI HII HAPA

JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni, linalishikilia baadhi ya wanenguaji wa kundi maarufu kwa kucheza maungo yakiwa wazi ‘Kanga Moko na Laki si Pesa’, gazeti la Tanzania Daima la leo lina hatimiliki ya hii habari.
Watuhumiwa hao wamekamatwa sambamba na watu wengi wanaofanya biashara ya kuuza miili yao, kufanya mapenzi hadharani na vitendo vya kishoga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa kundi hilo sambamba na watu hao walikamatwa katika maeneo ya Hoteli ya Travertine, Ambiance Club, Kinondoni Makaburini, Coco Beach na Barabara ya Tunisia.“Tumewakamata hao wanaofanya mchezo maarufu wa Kangamoko na Laki si Pesa na tayari wanafikishwa mahakamani muda wowote na msako bado unaendelea ili kudhibiti vitendo hivyo na michezo hiyo ya kangamoko au baikoko ambayo watu wengi wameilalamikia kutokana na mtindo wanaoutumia,” alisema.
Kundi la kangamoko limekuwa likilalamikiwa mara kwa mara kutokana na kucheza wakionesha maungo ya miili yao wazi na kuvaa nguo nyepesi wanazozimwagia maji.
Kukamatwa wasanii wa kundi hilo kumekuja siku chache tu tangu walalamikiwe katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kwamba wamekuwa wakipotosha jamnii.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...