Vikosi vya uokoaji majini wakitafuta miili ya waliokuwa kwenye ndege iliyoanguka
Shirika
la uokoaji nchini Indonesia limesema hivi sasa miili 37 imepatikana
kutoka kwenye bahari ya Java ambapo ndege ya Air Asia iliangukia
mwishoni mwa juma lililopita.
Helikopta na Meli za kijeshi
zimekuwa zikifanya doria katika eneo la bahari hiyo ambapo vitu
vinavyoelezwa kuwa mabaki ya ndege vimeonekana.hali ya hewa ya eneo hilo
kwa sasa imetengemaa ingawa bado mikondo ya bahari ina nguvu. Vikosi
vya wapiga mbizi wa Indonesia na Urusi vina matumaini ya kupata vifaa
vya kurekodia mawasiliano ndani ya ndege, ambavyo vitasaidia kujua
sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Surabaya
kwenda Singapore. Air Asia ilikuwa imebeba Watu 162 ilipopata ajali. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Lebanon imepokea Wakimbizi zaidi ya Wakimbizi milioni moja kutoka nchini Syria
Masharti
mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia
nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea Wakimbizi wengi.
Kwa
mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo
vinavyoeleza kwa nini wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon. Masharti
haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya
nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa Raia
wa Syria lazima wawe na Viza. Hatua hii inaelezwa kulenga
kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa
sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni moja. Hatua hii ya
sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio
nchini Lebanon ambao hawajajiandikisha kuwa wakimbizi. Kabla ya
sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka miezi sita,
lakini sasa raia wa nchi hiyo watalazimika kutimiza vigezo kadhaa ili
kupatiwa Viza mpakani. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Michuano
ya kuwania Kombe la Mapinduzi Zanzibar, linalozishirikisha timu saba za
Zanzibar, nne za Tanzania Bara na KCCA kutoka Uganda imezidi kupamba
moto ikiwa katika hatua ya kukamilisha michezo ya makundi.
Timu ya
Yanga ya Tanzania Bara imezidi kutoa vipigo kwa timu za kundi lake
baada ya kuzicharaza timu za Taifa Jang'ombe na Polisi zote za Zanzibar
magoli 4-0 kila moja na hivyo kujikusanyia mabao nane na pointi sita
ikiwa haijaruhusu nyavu zake kutikiswa na timu pinzani na hivyo kuongoza
kundi A lenye timu za Taifa Jang'ombe, Polisi Zanzibar na Shaba pia ya
Zanzibar. Kwa matokeo hayo imefuzu kucheza hatua ya robo fainali. Wapinzani
wao wakubwa pia kutoka Bara, Simba imekuwa na mwendo wa kusuasua ambapo
katika mchezo wake wa kwanza katika kundi C ilicharazwa na Mtibwa Sugar
bao 1-0 kabla ya kuzinduka na kujipatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Mafunzo ya Zanzibar. Katika kundi hilo Simba ina timu za Mtibwa Sugar ya
Tanzania Bara, Mafunzo ya Zanzibar na JKU Zanzibar. Kundi B lina timu za KCCA ya Uganda, Azam ya Tanzania Bara, KMKM na Mtende zote za Zanzibar. Januari saba michuano hiyo itaingia hatua ya robo fainali kwa timu sita kutoka makundi yote matatu yenye jumla ya timu 12. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Heka heka katika lango la Hull wakati Arsenal ilipoibuka na ushindi wa 2-0
Mechi kadha zimechezwa kuwania kombe la FA kwa vilabu vya ligi kuu ya England na vile vya madaraja mengine.
Mabingwa
watetezi Arsenal waliweza kuwacharaza Hull City 2-0 ambao wameshindwa
kulipa kisasi baada ya kushindwa katika fainali za mwaka jana timu hizo
zilipokutana. Magoli ya Arsenal yalifungwa na Per Mertesacker pamoja na
Alexis Sanchez.
Wachezaji wa Chelsea wakipongezana baada ya ushindi 3-0 dhidi ya Watford
Mechi nyingine zilikuwa kati ya
Chelsea na Watford, Chelsea ikiibuka na ushindi wa 3-0. Nayo Machester
United ikiishindilia Yeovil 2-0. Kwa upande wake Manchester City nao
waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Shef Wednesday. Crystal
Palace ilipata ushindi mnono dhidi ya Dover wa mabao 4-0, huku Stoke
City ikiicharaza Wrexham magoli 3-1. Sunderland nayo ilivuna goli 1-0
dhidi ya Leeds. Mechi kumi zimechezwa ambapo kwa ujumla vigogo wa soka England wameonekana kupata matokeo mazuri. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Wachezaji nyota wa ligi kuu ya Hispania, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid
Ligi
Kuu ya Hispania, La Liga imezidi kuleta ushindani mkubwa baada ya
vinara wa ligi hiyo, Real Madrid na Barcelona kupoteza katika mechi zao
za mwishoni mwa wiki.
Kikosi cha aliyekuwa kocha wa timu ya
Manchester United David Moyes ambaye kwa sasa anainoa timu ya Real
Sociedad ya ligi kuu ya Hispania, La Liga, imeiadhibu Barcelona kwa goli
1-0 alilojifunga mwenyewe mchezaji wa Barcelona Jordi Alba, mapema
katika dakika ya pili ya mchezo.
David Moyes kocha wa Real Sociedad ya Hispania
Kipigo Real Madrid cha 2-1
kutoka kwa Valencia mapema Jumapili kingewawezesha Barcelona kuelekea
mbele katika kinyang'anyiro cha ubingwa wa ligi hiyo endapo timu hiyo
ingeshinda. Lakini kocha Luis Enrique alianza mchezo huo kwa
kutowaanzisha wachezaji wake mashuhuri akiwemo Lionel Messi, Neymar na
Dani Alves. Barcelona ilishindwa kusawazisha goli walilojifunga wakati Moyes akipata ushindi wa pili akiwa meneja wa timu ya Sociedad. Messi,
Neymar na Alves walirejea katika mazoezi Ijumaa wiki iliyopita baada ya
mapumziko marefu ya Krismasi Amerika Kusini ambako ligi ilisitishwa ili
kusherehekea siku kuu hiyo. Enrique alifanya mchezo wa
kubahatisha kwa kutowapanga wachezaji hao katika mchezo wake na Real
Sociedad ambayo imekuwa kikwazo kwa Barcelona katika michezo ya nyuma.
Wachezaji wa Real Sociedad wakishangilia goli katika moja ya michezo yao ya ligi kuu ya Hispania
Na kwa hiyo imethibitika kwa
mara nyingine kwamba Barcelona hawana chao katika uwanja wa Anoeta sasa
ikiwa ni michezo sita, Barcelona ikipoteza kwa Real Sociedad. Kwa
upande wake Real Madrid ilijikuta ikipoteza mchezo wake dhidi ya
Valencia baada ya kucharazwa mabao 2-1 licha ya Real Madrid kuongoza
kipindi cha kwanza kwa bao la penalti lililofungwa na Cristian Ronaldo
dakika ya 14. Valencia ilijipatia magoli yake yote mawili kipindi cha pili yakifungwa na Barragán dakika ya 52′ na Otamendi dakika ya 65. Real
Madrid inaongoza msimamo wa ligi ya Hispania ikiwa na pointi 39 katika
michezo 16 ikifuatiwa kwa karibu na Barcelona yenye pointi 38 baada ya
kucheza mechi 17. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Asante kwa kutembelea Blog na pia ku-like page yetu ya facebook, endelea kuwa nasi siku zote ili upate habari nzuri na za uhakika kutoka kila kona ya dunia wakati wowote kila siku.
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.