Thursday, January 01, 2015

RAIS KIKWETE ATOA SALAMU ZA MWISHO ZA MWAKA AKIWA MADARAKANI

Rais Kikwete 

Mwaka wa uchaguzi umeingia. Usiku wa kuamkia leo, Watanzania wameupokea mwaka mpya 2015 huku tafakari kubwa ikiwa ni matukio makubwa yatakayotokea mwaka huu, ukiwamo Uchaguzi Mkuu na kura ya maoni ya Katiba Inayopendekezwa.
Mbali na uchaguzi wa rais wa awamu ya tano, wananchi wataamua ama kuipitisha au kuikataa Katiba Inayopendekezwa, mambo ambayo wasomi, wanasiasa na wanaharakati wameonya kuwa yanatakiwa kuendeshwa na kusimamiwa kwa weledi na umakini mkubwa.
Vilevile, kutokana na matukio hayo kugharimu fedha nyingi, wataalamu wa uchumi wanatabiri kuwa mwaka huu utakuwa mgumu na itakaowalazimu Watanzania kufunga mikanda zaidi.
Pia, macho na masikio ya wananchi yako kwa vyama vya upinzani ambavyo vimeungana na kuzaa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuona kama vitasimamisha mgombea mmoja wa urais na katika nafasi za ubunge na udiwani kama vilivyokubaliana, ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MUUMINI MBARONI KWA KUFANYA FUJO KANISANI

Leonard Paul
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo
POLISI mkoani Morogoro linamshikilia Jackson Mnyilemi (20), ambaye ni muumini wa Kanisa la Moravian Tarafa ya Malinyi wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuhusika kufanya fujo kanisani.
Fujo hizo zilisababisha kujeruhiwa kwa waumini wawili kwa kukatwa sehemu za usoni na mikononi na kitu chenye ncha kali.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema jana kuwa tukio hilo ni la Desemba 28, 2014 majira ya saa 10 : 40 asubuhi katika kijiji cha Makelele na kuwataja waumini waliojeruhiwa kuwa ni Maria Silumbwe (47) na Aron Silumbwe (20), wote wakazi wa Kijiji hicho kilichopo Tarafa ya Malinyi wilayani Ulanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MWAKYEMBE AFUKUZA KAZI VIGOGO 6 WA RELI

Dk Harison Mwakyembe.
 Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ameagiza wafanyakazi sita wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), wafukuzwe kazi na polisi wawakamate na kuwalaza rumande kuanzia jana kutokana na tuhuma za wizi.
Pia, ameagiza mali za watuhumiwa hao, zichunguzwe na ikibainika ni zaidi ya kipato chao cha kawaida, zipigwe mnada na Bodi ya Wakurugenzi ikae na kuangalia hatua zaidi za kuchukua.
Dk Mwakyembe alitoa maamuzi hayo jana baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa TRL na kuonekana kutoridhishwa na vitendo vya wizi, vinavyoendelea katika shirika hilo.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Stanley Makunja, Stanley Andrew, Edward Benedicto, Lucy Mtinya, B. Ruoga na Jackson Moses.
Hata hivyo, Mwakyembe alipoombwa na waandishi wa habari, kufafanua vituo vya kazi vya watuhumiwa hao, alidai kwamba wote ni wa TRL na wamewajibishwa kama wafanyakazi wa TRL. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO SIKU YA KWANZA YA MWAKA 2015

.
.
.

Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

ZITTO: NITAMUUNGA MKONO MBOWE


HAKI SAWA: Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba (kulia) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Zitto Kabwe wakiwasili kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara jana, ambako walihutubia mkutano wa hadhara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe amesema atamuunga mkono Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe pale atakapowasilisha hoja yake bungeni kuhusu ufisadi wa zaidi ya Sh1 trilioni katika mradi wa bomba la gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Zitto aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa mkoani hapa uliandaliwa na Chama cha Wananchi (CUF) kuwashukuru wakazi wa mkoa huo kwa kuwachagua viongozi wa chama hicho katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Najua bado mnalia kuhusu bomba la kupeleka gesi Dar es Salaam, machozi yenu yatafutika kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa bomba hili zimeanza kuchomoza. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

WATU 20 WAFARIKI HARUSINI

Mmoja ya watoto waliojeruhiwa wakati bomu liliporushwa katika nyumba moja iliokuwa ikifanya sherehe ya harusi mkoani Helmand nchini Afghanistan.Takriban watu 20 waliaga dunia 
 
Sherehe moja ya harusi nchini Afghanistan, imeshambuliwa kwa mzinga uliorushwa na roketi na kusababisha mauaji ya watu 20 na kuwajeruhi wengine zaidi ya kumi na mbili.
Kisa hicho kilitokea wakati wa makabiliano makali kati ya walinda usalama wa Afghanistan na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Helmand.
Mmiliki wa jumba lilofanyiwa harusi hiyo amesema kuwa wageni walikuwa wanajikusanya nje kumkaribisha bi harusi,na kuongezea kuwa watoto wake tisa wametoweka.
Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Lashkar Gah,mji mkuu wa mkoa huo.
Shambulio hilo limetokea wakati wa siku ya mwisho kwa ujumbe wa wanajeshi wa Marekani na wale wa shirika la kujihami la NATO wanaoondoka nchini Afghanistan. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...