Monday, December 29, 2014

ASKOFU "WANAWAKE ACHENI KUWAZENGEA MAKASISI"

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi

ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi amewataka akina mama kuacha kuwazengea makasisi, hatua inayoweza kuwafanya kukacha kiapo chao cha useja.
Kwa mujibu wa Askofu Mkuu Ruwa’ichi, pamoja na baadhi ya akina mama ‘kuwazengeazengea’, kumekuwa na msukumo kutoka kwa baadhi ya waumini, kuwashawishi makasisi kuasi kiapo cha useja walichoapa ili wakaoe.
Akizungumza kabla ya kuwaweka wakfu mafrateli watano kuwa makasisi, ambayo ni hatua ya mwisho kabla ya kuwa mapadri kamili, Ruwa’ichi alisema akina mama mnatakiwa kukaa mbali na watumishi hao wa Mungu.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 29, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

NDEGE ILIYOPOTEA WAENDELEA KUITAFUTA

Airasia iliotoweka 
 
Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda.
Watu 162 walikuwa kwenye ndege hiyo wakati ikipoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia. Shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung.
Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

WATOTO WAZUIWA KUITEMBELEA ISRAEL

Watoto waliotekwa Gaza ndani ya Basi
Kundi la Hamas limewazuia kundi la watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.
Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.
Wanaharakati wa masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini wakabadili msimamo wao baadae. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

YANGA NA AZAM ZASHINDWA KUTAMBIANA

Hamisi Tambwe na Msuva wakishangilia bao leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Afrika mwakani, Azam na Yanga zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare 2-2 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es salaam.
Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofunga na Didier Kavumbagu dakika 6, Yanga walisawazisha kupitia Amiss Tambwe (7) na kupata la pili lililofungwa na Simon Msuva (57), kabla ya John Bocco aliyeingia akitoa benchi alisawazisha Azam dakika 65.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

MTIBWA SUGAR CHUPU CHUPU KWA STAND

TIMU ya soka ya Mtibwa Sugar ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania bara jana ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Stand United ya Shinyanga katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani Morogoro jana asubuhi.
Mchezo huo ilikuwa uchezwe juzi lakini ulivunjika katika dakika ya sita baada ya mvua kubwa iliyosababisha maji kujaa kwenye uwanja wa Manungu na kuamuliwa uchezwe jana saa mbili asubuhi.
Katika mchezo huo wa jana wachezaji wa Stand United walionesha mpira wa kuvutia hasa kipindi cha kwanza na kuwawezesha kupata bao la kuongoza katika dakika ya 22 ya mchezo.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...