Sunday, December 28, 2014

RUSHWA, NGONO TATIZO MISS TANZANIA


“Kwa sasa hana uamuzi wowote mpaka pale atakapokuwa amepewa barua rasmi.” Lundenga 

Serikali imesema imeyafungia mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandaaji kukiuka taratibu na kanuni huku pia yakitajwa kukithiri kwa rushwa ya ngono na upendeleo.
Mashindano hayo yalifunguliwa mwaka 1994, yamefungiwa kwa miaka miwili baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wananchi na washiriki.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Bazara la Sanaa Tanzania (Basata), Godfrey Mngereza alisema jana kuwa Kamati ya Miss Tanzania kupitia kampuni yake ya Lino Agency, imekiuka kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
“Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,” alisema Mngereza.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

YANGA, AZAM MWISHO WA UBISHI LEO

Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambako kutafanyika mchezo kati ya Azam na Yanga
Sehemu ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

YANGA leo itakuwa mwenyeji wa Azam FC katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Timu zote zinashuka dimbani zikiwa na pointi 13 kila moja zikitofautiana kwa uwiano wa mabao.
Mechi ya leo ni ya pili kukutana kwa timu hizo msimu huu, baada ya ile ya Ngao ya Jamii iliyofanyika mapema Septemba na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 yaliyofungwa na aliyekuwa mchezaji wao Geilson Santos ‘Jaja’ na Simon Msuva.
Katika historia ya kukutana kwao kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga wanaonekana kuwazidi Azam baada ya msimu wa mwaka 2012/2013 kuwafunga bao 1-0. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

FIFA YAMPA BEJI MWAMUZI WA SIMBA NA YANGA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara akijiandaa kuusaini mpira ulioshikiliwa na mwamuzi wa mchezo huo, Jonesia Rukyaa (kulia)

MWAMUZI aliyechezesha mechi ya Nani Mtani Jembe2
Jonesia Rukyaa ni miongoni mwa waamuzi wa kike sita waliopata beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

Jonesia alimudu vyema kuchezesha mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa Desemba 13, mwaka huu na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Wengine waliopata beji hiyo ni Florentina Zablon wa Dodoma na Sophia Ismail wa Mara (Waamuzi wa kati) na Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary wa Tanga, Grace Wamala kutoka Kagera na Dalila Jaffary wa Zanzibar (Waamuzi Wasaidizi).
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

KIONGOZI WA AL-SHABAAB AKAMATWA

 Kundi la wapiganaji wa Al shabaab
 
Maafisa nchini Somali wanasema kuwa kiongozi mkuu wa kundi la wapiganaji wa Alshabaab amekamatwa karibu na mji mmoja karibu na mpaka wa Kenya na Somali.
Kamishna wa Wilaya ya El Wak mjini Gedo ameiambia BBC Somalia kwamba vikosi vya usalama vilimkamata Zakariya Ismail Ahmed Hersi katika maficho yake ndani ya nyumba moja baada ya kupashwa habari.
Mwaka 2012 Marekani ilitoa zawadi ya dola millioni 3 kwa yeyote yule ambaye angeweza kutoa habari za Hersi. Kundi la Al Shabaab limejiondoa kutoka miji kadhaa nchini Somalia tangu uzinduzi wa mashambulizi makali dhidi ya kundi hilo yanayotekelezwa na vikosi vya AMISOM vikishirikiana na wanajeshi wa serikali ya Somalia.
Bwana Hersi alikuwa kiongozi wa kundi la Alshabaab upande wa Amniyat. Mapema mwaka huu alikosana na kiongozi wa kundi hilo Ahmed Abdi Godane ambaye aliuawa katika mashambulizi ya Marekani mnamo mwezi Septemba.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Na BBC 

WANAUME WALIOOANA WAPUNGUZIWA HUKUMU

 Wanaume waliooana Misri wapunguziwa hukumu jela
 
Mahakama moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto Nile huku wanaume wawili wakionekana wakivalishana pete na kukumbatiana.
Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja. Ushoga ni kinyume na utamaduni wa Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria. Wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri. 
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Friday, December 26, 2014

MAASKOFU WATAKA JK AENDELEZE FAGIO LAKE

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahi jambo na Fred Msongole aliyebeba mtoto wake, Jonathan Msongole (miezi 8) baada ya kukamilisha ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika kitaifa katika Kanisa la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam jana. (Picha na Fadhili Akida).
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Zanzibar, Michael Hafidh (kulia) akifurahia jambo na Fred Msongole.

MAASKOFU wa madhehebu mbalimbali ya Kikristo nchini, wamepongeza uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuwajibisha watendaji wake, huku wakimtaka asiishie kuchukua hatua kwa waliotajwa kuhusika na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow pekee, bali pia wazembe na wote wanaokutwa na tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
Aidha, wamesisitiza kamwe asicheke nao, kwani kitendo cha kuwavumilia kinaweza kugeuka shubiri katika utawala wake kwa kuwa watamharibia kazi. Walisema hayo kwa nyakati tofauti katika salamu zao za maadhimisho ya Sikukuu ya Krismasi, jana.
Weka pembeni Akiongoza mahubiri katika Ibada Kuu ya Krismasi katika Kanisa la Champlesy la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Askofu Michael Hafidh wa Zanzibar, alishauri Rais Kikwete aendeleze utaratibu wa kuwawajibisha viongozi wazembe na wasio waadilifu katika kazi zao.
 Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...