Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamedi Mpinga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.
JESHI la Polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa
Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), limewaadhibu wamiliki wa magari zaidi ya
21.
Mawakala wao wa kukata tiketi, wamesombwa na kuburuzwa mahakamani,
ambao baada ya kesi zao kusogeswa mbele, sasa wanasota mahabusu,
watakakokuwa hadi baada ya shamrashamra za kuukaribisha Mwaka mpya 2015.
Wakati mabasi mengi yakinaswa Morogoro, mawakala wa tiketi ambao pia
ni maarufu kama wapigadebe, wamekamatwa katika kikuo kikuu cha mabasi
yaendayo mikoani cha Ubungo, Dar es Salaam.
Hayo yamethibitishwa na Ofisa Mfawidhi wa Sumatra Mkoawa Morogoro,
Allen Mwanri aliyesema mabasi zaidi ya 21 yalikamatwa kwa makosa ya
mbalimbali, likiwemo kubwa la kuzidisha nauli na kutoza nauli kubwa.
Hata hivyo, alisema kila mmiliki wa basi lililokamatwa kwa kuzidisha
nauli na nauli kubwa, alitozwa adhabu ya kiasi cha Sh 250,000. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz,
ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali
na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715
221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.








