Wednesday, January 07, 2015

"KIWANGO CHA NGASSA KIMESHUKA, LAKINI NI MCHEZAJI MWENYE AKILI, LAZIMA ATARUDI KATIKA KIWANGO CHAKE" - PLUIJM

KOCHA mkuu wa Yanga SC, Mholanzi, Johannes Hans van der Pluijm anaamini Mrisho Ngassa atarudi katika kiwango chake cha zamani.
Pluijm alikiri wazi kuwa nyota huyo ameshuka kiwango kwa sasa  na ndio maana anaanzia benchi katika mechi mbalimbali, lakini anaonesha juhudi kubwa mazoezini kitendo kinachoonesha wazi ametambua alipo sasa.
“Kiwango cha Ngassa kimeshuka, lakini ni mchezaji mwenye akili, lazima atarudi katika kiwango chake”. Alisema Pluijm.
NGASSA-MRISHO
Kocha huyo anayependa soka la kushambulia aliongeza kuwa kwasasa kikosi chake kimesheheni nyota wa kiwango cha juu, hivyo inawalazimu wachezaji kufanya jitihada za kumshawishi.
Moja kati ya mechi kubwa ambayo Ngassa hakuanza chini ya Pluijm mwishoni mwa mwaka jana ni ile ya ligi kuu soka Tanzania bara dhidi ya Azam fc iliyopigwa desemba 28 mwaka jana uwanja wa Taifa ambapo timu hizo zilitoka sare ya 2-2.
Katika mechi hiyo, Ngassa alichezeshwa dakika 7 tu kitendo kilishoashiria mchezaji huyo kipenzi kwa Wana Yanga si mchezaji tegemeo tena katika kikosi cha Yanga. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

DROO YA KUPANGA MECHI KOMBE LA FA YAFANYIKA

Mabingwa watetezi wa kombe la FA, wakishangilia ushindi mwaka uliopita. 
 

Droo ya kupanga mechi za raundi ya 4 ya Kombe la FA imefanyika.
Katika mpangilio huo, vigogo Manchester United imepangwa kucheza na timu ya daraja la chini ya Cambridge United.
Mabingwa Watetezi, Arsenal, watakuwa Ugenini kucheza na Brighton au Hove Albion ambayo ipo Daraja la chini ya Ligi Kuu England.
Chelsea itakipiga na Mill wall au Bradford City. Manchester City itapepetana na Middlesbrough
Southampton/Ipswich na Crystal Palace
Blackburn Rovers na Swansea City
Michezo ya raundi ya nne inatarajiwa kupigwa Januari 24 na 25.
NAKO kwenye kombe la mapinduzi
Baada ya kutojulikana kuwa nani atacheza na Simba katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi, sasa kila kitu kiko wazi. Simba itaivaa Taifa Jang'ombe katika mechi ya michuano hiyo hatua ya robo fainali hii leo usiku.
Mechi hiyo itachezwa saa 2 usiku kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Siku inayofuata Alhamisi, mechi nyingine ya robo fainali itapigwa jioni, nayo ni kati ya Azam dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mechi hiyo inaaminika kuwa moja ya zile ngumu na safi za michuano ya Mapinduzi.
Yanga sasa itacheza mechi yake ya robo fainali dhidi ya maafande wa JKU.
Mechi hiyo itapigwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Yanga inakutana na JKU baada ya kumaliza vinara wa kundi A wakiwa na pointi 9. Walipata pointi hizo baada ya kushinda mechi zote tatu katika makundi kwa kujikusanyia mabao tisa, wakiwa hawajafungwa hata moja.
Walikamilisha pointi hizo tisa baada ya kuifunga Shaba kwa bao 1-0 katika mechi tamu na ya kuvutia jana usiku.
Bao la mchezo huo lilifungwa na Mbrazil Andrey Coutinho. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MATOKEO YA MECHI ZA JANA KOMBE LA FA ENGLAND HAYA HAPA… EVERTON YATOKA SARE

2475D89E00000578-0-image-a-88_1420581200502
 Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
England – FA Cup January 6
FT Everton 1 – 1 West Ham United
FT Scunthorpe United 2 – 2 Chesterfield

Tuesday, January 06, 2015

PROFESA SOSPETER MUHONGO AFANYA ZIARA SIMIYU KUKAGUA MIRADI YA UMEME

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akitoa maelekezo kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Symbion iliyopewa kazi ya kujenga miundombinu ya  umeme katika kijiji cha Nyamikoma kilichopo wilayani Busega Bw.  Steve Thomson (kushoto)
 Meneja wa Tanesco- Kanda ya Ziwa Mhandisi Joyce Ngahyoma, akifafanua jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na  wananchi wa kijiji cha Nyamikoma wilayani Busega (hawapo pichani)
 Mkazi wa kata ya Ijitu  iliyopo wilayani Busega ambaye  jina lake  halikupatikana mara moja akitoa hoja yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto  waliosimama mbele) mara Waziri alipofanya ziara katika kijiji hicho na kusikiliza kero za wananchi
Diwani wa Kata  ya  Ijitu iliyopo wilayani Busega Vumi Magoti  akielezea kero za umeme katika kata yake mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa pili kutoka kushoto), viongozi na wananchi  (hawapo pichani).
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokelewa na baadhi ya watendaji kutoka  Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) Kanda ya Ziwa na Nishati na Madini mara baada ya kuwasili katika  Uwanja wa Ndege wa Mwanza. Profesa Muhongo anafanya ziara  katika mikoa ya Simiyu, Tabora na Shinyanga lengo likiwa ni kukagua miradi  ya umeme vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Taneesco. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...