Thursday, April 04, 2013

SHILOLE, Q-CHILLAH WAFUMWA LAIVU WAKIWA KATIKA MAHABA

Aibu hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya shoo siku ya Pasaka.
Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa.


Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana: Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17. 

Katika mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel. 

Airtel inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya vifaa vya kisasa vya elektoniki.

Chadema wamtuhumu Mwakyembe kutoa zabuni kinyume cha sheria

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume cha sheria za ununuzi. Chadema walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine. 
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema: “Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo waache mimi niongoze Serikali.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...