| Aibu
hiyo ilitokea Machi 29, mwaka huu ambayo ilikuwa Ijumaa Kuu ambapo
wasanii hao walikuwa wakitoka Dar kwenda Mwanza kwa ajili ya kufanya
shoo siku ya Pasaka. Akilisimulia gazeti hili, shuhuda wetu aliyekuwemo ndani ya ndege hiyo (jina tunalo) alisema aliwaona Shilole na Q-Chillah wakiwa katika ‘malovee’ ambapo mara kwa mara walikuwa wakipigana mabusu kitendo kilichowafanya abiria wengine kuwakodolea macho yenye kuwashangaa. |
Thursday, April 04, 2013
SHILOLE, Q-CHILLAH WAFUMWA LAIVU WAKIWA KATIKA MAHABA
Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana: Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu

Kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel inayofanya kazi pamoja na kampuni ya
Samsung zimesaini makubaliano ya kushirikiana kudhamini mashindano
makubwa Afrika kwa vijana wa chini ya miaka 17.
Katika
mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji rasmi wa
vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu kama
Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel.
Airtel
inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20 barani
Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni makubwa ya
vifaa vya kisasa vya elektoniki.
Chadema wamtuhumu Mwakyembe kutoa zabuni kinyume cha sheria

Chama
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtuhumu Waziri wa Uchukuzi,
Dk Harrison Mwakyembe kwamba alitoa zabuni ya ujenzi wa bandari ya
nchikavu kwa kampuni inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinyume
cha sheria za ununuzi. Chadema
walisema jana kwamba, kampuni hiyo ni Jitegemee Trading Company ambayo
ilipewa zabuni ya ujenzi wa bandari katika Viwanja vya Sukita pasipokuwa
na mchakato wa kushindanisha kampuni nyingine.
Mkurugenzi
wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Benson Kigaila alisema:
“Mwakyembe aseme alitoa zabuni hiyo kwa Jitegemee kwa kuzingatia vigezo
gani? Kampuni ngapi zilishindanishwa katika mchakato huo na asipofanya
hivyo hastahili kukaa wizarani hapo bali alipelekwa Segerea gerezani
kwani ni kosa kubwa kutoa zabuni kinyemela.”
Hata
hivyo, Dk Mwakyembe, ambaye yuko jimboni kwake Kyela mkoani Mbeya
alipoulizwa kuhusu madai hayo alijibu na kukata simu; “Mimi nina kazi ya
kuongoza wizara na wao Chadema wana kazi ya kuchonga mdomo, hivyo
waache mimi niongoze Serikali.
Subscribe to:
Comments (Atom)

