Wednesday, April 03, 2013

LOWASSA AMTOA KAFARA PINDA

WABUNGE WAUNGANISHA NGUVU KUTAKA KUMSULUBU BUNGENI





RIPOTI ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa mwaka 2006 kuchunguza ujenzi wa maghorofa katika Jiji la Dar es Salaam, imemweka mahala pabaya na inaweza kumtoa kafara, Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.
Pinda anatolewa kafara katika sakata la jengo la ghorofa 16 lililoporomoka katikati ya Jiji la Dar es Salaam wiki iliyopita na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 40.

Kutokana na janga hilo, Pinda analalamikiwa kukalia ripoti ya Tume ya Lowassa ambayo ilikuja na mapendekezo ya kukabiliana na maghorofa yaliyojengwa chini ya kiwango.

KANGAMOKO WATIA AIBU TENA MKOANI KAGERA HEBU ANGALIA PICHA HIZI




SUMATRA YATANGAZA KUPANDA KWA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU NA DALADALA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM

IMG_6840Kaimu Mkurugenzi wa SUMATRA Athman Kilima akizungumza na waandishi wa habari leo katika makao makuu ya taasisi hiyo wakati akitangaza kupanda kwa viwango vya nauli ya mabasi ya mikoani na Daladala.
………………………………………………………………..

 Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekamilisha mchakato na kuridhia viwango vipya vya nauli kwa ajili ya usafiri wa mijini na usafiri wa kwenda mikoani. Viwango hivi vipya vimefikiwa baada ya kufuata taratibu za kisheria na za kiutendaji ambazo SUMATRA kama msimamizi na mdhibiti wa sekta ya usafiri wa barabara inapaswa kuzifuata kabla ya kuridhia viwango hivyo. Viwango vipya vya nauli vitaanza kutumika kuanzia tarehe 12 Aprili, 2013.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...