Tuesday, April 02, 2013

KIJIJI CHA MISUKULE CHAGUNDULIWA NCHINI

Msukule.


Msukule.
Msukule.



Na Makongoro Oging', Bagamoyo


INATISHA na hofu kubwa imetanda katika Kijiji cha Kimange, Wilaya ya Bagamoyo  mkoani Pwani kufuatia baadhi ya viongozi  wa dini kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ili wapelekwe kanisani.

Uchunguzi umebaini kuwa nia ya viongozi hao wa dini kuteua kijiji hicho na kuwatumia vijana wa hapo kama misukule ni kuwalaghai waumini kwamba wana uwezo wa kufufua watu wanaodaiwa kufa na kuchukuliwa kimazingara.
Imebainika kuwa viongozi hao wa dini wamekuwa wakifanya udanganyifu huo lengo lao likiwa ni kupata waumini wengi katika makanisa yao ambao wamekuwa wakiamini kwamba kweli misukule inarejeshwa katika maisha ya kawaida.

AGNES MASOGANGE AWEKA PICHA INSTRAGRAM AKIWA KATIKA POZI ZA KIMAHABA

Ni miezi michache imepita tangu video queen wa bongo Agnes Masogange aadhirike baada ya video yake chafu kusambaa ikionesha waki**** na jamaa yake.
 
Lakini sasa inaanza kuonekana kuwa dada huyu hii ni michezo yake baada leo kupost picha zinazomuonesha wakiwa kimahaba na mpenzi wake katika mtandao wa instragram.JE HIVI TUKIONA VIDEO NYINGINE AKIWA NA HUYU MCHIZI TUTASHANGAA AU TUTASEMA NDIO KAZI YAKE?

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI ZANZIBAR ALIGOMBEA UBUNGE TIKETI YA CUF 2010

IMEELEZWA kuwa, mtuhumiwa Omar Mussa Makame (35) anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumuua Padri Evaristus Mushi ni mwanachama wa CUF ambaye aligombea nafasi ya uwakilishi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 katika Jimbo la Rahaleo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF).
Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Hamad Masoud alithibitisha jana kuwa, mtuhumiwa huyo ni mwanachama wao na alishiriki katika mchakato wa uchaguzi mkuu na kusimamishwa na chama katika kampeni za Uwakilishi Jimbo la Rahaleo.
“Ni kweli mtuhumiwa anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padri Mushi ni mwanachama wetu na alishiriki katika mchakato wa kuwania Uwakilishi Jimbo la Rahaleo mwaka 2010.
Hata hivyo, Hamad alisisitiza na kusema suala la Omar kamwe lisihusishwe na CUF na kusema suala hilo watalitolea tamko baadaye.
Kwa mujibu wa kumbukumbu za Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ripoti ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Jimbo la Rahaleo, mgombea wa CCM, Nassor Salim Ali maarufu kama Jazirra aliibuka na ushindi kwa kupata kura 3,952 sawa na asilimia 63.10, wakati mgombea wa CUF, Omar Mussa Makame alipata kura 2,310 sawa na asilimia 39.9 na kushika nafasi ya pili.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...