Upangaji
wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za
mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015
yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Mashindano hayo yataanza Januari 17, 2015.
Upangaji
wa makundi ulirudishwa wiki moja nyuma ili kuiwezesha Equatorial
Guinea, kujiandaa baada ya kuchukua nafasi ya Morocco, iliyokuwa iandae
mashindano hayo, lakini ilishindwa kufanya hivyo baada ya kutaka
mashindano hayo yasogezwe mbele kuhofia ugonjwa wa Ebola ambao
umeyakumba baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi, ambako zinatoka timu
nyingi zinazoshiriki michuano hiyo.
Mabingwa watetezi Nigeria ni
moja ya timu kubwa zilizoshindwa kufuzu kucheza fainali za mwakani,
pamoja na Misri na Angola ambazo zote kwa mshangao hazitaweza kushiriki.
Haya hapa makundi manne ya AFCON 2015:
Kundi B Zambia, Tunisia, Cape Verde, DR Congo
Kundi C Ghana, Algeria, South Africa, Senegal
Kundi D Ivory Coast, Mali, Cameroon, Guinea
Wenyeji
Equatorial Guinea na Congo zitacheza mechi ya ufunguzi wa michuano
hiyo. Kundi D ndilo linaloonekana kuwa gumu zaidi kutokana na timu
zilizopangwa kundi hilo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, ukitaka kuwa wa kwanza
kupata habari zetu Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz