Friday, February 22, 2013

BREAKING NEWSZZZZZZZZ .... BABA MZAZI WA RAIS MSEVEN AFARIKI DUNIA

Baba wa Rais Museveni afariki dunia.

Mzee Amos Kaguta baba mzazi wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda amefariki dunia leo asubuhi huko jijini Kampala Uganda.

Mzee Amos Kaguta amefariki akiwa na umri wa miaka 96 na inasemekena alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya tumbo pia kichwa.East Africa Radio kwa habari zaidi.

LOWASSA ATOA OMBI KWA RAIS KIKWETE



Waziri mkuu aliejiuzulu Mh. Edward Lowassa, amemtaka rais Kikwete aunde tume kuchunguza kilichopelekea matokeo mabaya ya form IV mwaka huu. Amesema tume itasaidia kubaini ni nini chanzo cha tatizo.

Wakati huo huo Mh. Lowassa amemsifu kijana aliyemchora Messi na kusema kijana huyo ni intelligent. Amesifu uwezo wa kijana huyo kufanya hivyo!


Vilevile Mh. Lowassa, ameitaka serikali kuongeza uwekezaji katika elimu kwani amesema tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, Tanzania ndio ya mwisho kwa uwekezaji kwani inawekeza asilimia moja point something ya GDP katika elimu wakati Kenya ni asilimia tano na Rwanda kama sikosei amesema inawekeza mpaka asilimia 7 ya GDP katika elimu na hivyo ametoa wito kwa serikali kuongeza uwekezaji katika elimu.


Mh. Lowassa pia amemsifu Rais Kikwete kwa kufanikiwa katika maeneo mengine kama ujenzi wa barabara, hospitali, zahanati na kwenye maeneo mengine na kumtaka ajielekeze zaidi katika elimu. Mh. Lowassa amerudia kauli yake na kusisitiza kuwa msimamo wake utabaki kuwa ni elimu kwanza na sio kitu kingine.


Miongoni mwa viongozi waliohojiwa ni pamoja na Zitto Kabwe ambaye mbali na kushauri mambo mbalimbali pia amewataka waziri wa elimu na naibu wake pamoja na katibu mkuu wa wizara ya elimu kujiuzulu.


Source: Clouds FM mchana wa leo/jamiiforum

ASKOFU MDEGELA AFICHUA SIRI NZITO YA MAUAJI ZANZIBAR.


Askofu Dkt Mdegela
 

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi
yaIringa, Dk. Odernbarg Mdegela, ametoboa siri nzito kuhusu
uhalifu unaoendelea nchini, yakiwemo mauaji ya viongozi wa kidini na
uharibifu wa nyumba za ibada, kwamba upo nyuma ya vikundi kadhaa
vilivyopatiwamafunzo maalumu nje ya nchi kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.

Ingawa hakuvitaja moja kwa moja vikundi hivyo vinavyofadhiliwa
ilikutekeleza mkakati huo, Askofu Mdegela amedai kwamba vikundi
hivyo,vimepata mafunzo hayo na kwamba lengo ni kukamilisha mkakati
huo.

Mh. Membe kufungua Mkutano wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Cooperation), tarehe 24 hadi 25 Februari, 2013


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (Pichani) anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Cooperation), tarehe 24 Februari, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro) iliyopo Dar es Salaam.
Mkutano huo pia utahudhuriwa na Waziri anayeshughulikia Masuala ya Mambo ya Nje wa Oman, Mhe. Yousuf bin Alawi bin Abdullah anayetarajiwa kuwasili nchini Jumamosi tarehe 23 Februari, 2013 saa 11 kamili jioni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo mjini Dar es Salaam.
Mkutano huo unatokana na Makubaliano yaliyosainiwa tarehe 14 Oktoba 2009 kati ya nchi hizo mbili mjini Muscat, Oman.
Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo utajadili masuala ya ushirikiano baina ya Tanzania na Oman katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nishati na Madini, Viwanda na Biashara, Elimu, Afya, Uwekezaji, Utamaduni na Habari.
Imetolewa na:
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

RAIS MWAI KIBAKI WA KENYA AHITIMISHA ZIARA YAKE YA KISERIKALI NCHINI


 Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini akiagana na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali aliye pamoja na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda pamoja na viongozi wengine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini, wakisiliza taarifa ya pamoja ikisomwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini wakisimama kupokea heshima wakati nyimbo za taifa zikipigwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Rais Emilio Mwai Kibaki wa Kenya anayehitimisha leo Februari 21, 2013 ziara yake ya Kiserikali nchini katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Picha na IKULU

MONTAGE CHARITY BALL KUFANYIKA LEO NDANI YA SERENA HOTELI

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda akiongea na waandishi wa habari leo katika hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar Es Salaam
Teddy Mapunda Akifafanunua Jambo Mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo Picha) leo katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Serena Kulia ni Msanii kutoka Nchini Kenya Kidumu atakaye fanya makamuzi pamoja na Peter Msechu na Barnaba
Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda(katikati) Akiteta Jambo Na Msanii Kutoka Nchini Kenya Kidumu (kulia) wakati wa Mkutano na Wahandishi wa Habari uliofanyika katika Hoteli ya Serena Leo na Kushoto ni Msanii wa Bongo Fleva Peter Msechu
Mkurugenzi wa Montage Limited Teddy Mapunda akiongea na Waandishi wa habari (hawapo Pichani) wakati akiongelea Juu ya Tafrija ya Hisani ijulikanayo Kama Montage Charity Ball itakayofanyika Leo katika Hoteli ya Serena Kulia Kwa Teddy Mapunda Ni Peter Msechu na Kutoka Kushoto ni Msanii Barnaba na Kidumu kutoka Nchini Kenya
Pichani ni baadhi ya Wasanii  watakao tumbuiza kwenye tafrija ya Montage Charity Ball itakayofanyika jioni ya leo ndani ya Serena Hotel,jijini Dar.Kutoka kushoto ni Peter Msechu,Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band.
Pichani shoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda (katikati) akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kufanyika kwa tafrija maalum ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya afya hapa nchini kupitia mfuko wa Montage Charity Ball,itakayofanyika jioni ya leo, Februari 22 kwenye Hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam

Aidha Teddy ameeleza kuwa malengo hasa ni kukusanya kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 100 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya Wanawake wenye matatizo mbali mbali.Mgeni rasmi katika Tafrija hiyo anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA),Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Kulia kwake ni baadhi ya Wasanii watakaotumbuiza kwenye tafrija hiyo ambao ni Kidumu kutoka Kenya,Barnaba pamoja na Deo Mwanambilimbi ambaye ni kiongozi wa Kulunde Band na Peter Msechu ambaye hayupo pichani.

Maofisa wa FIFA wawasili Tanzania kukagua miradi ya maendeleo ya soka

Ashford Mamelodi. 
Ofisa Maendeleo wa Kusini mwa Afrika wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Ashford Mamelodi amewasili leo kwa ajili ya kufuatilia shughuli za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Mamelodi, ambaye amekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za maendeleo nchini Tanzania tangu alipoteuliwa kushika nafasi hiyo, pia amekuja kumtambulisha msaidizi wake, Patrick Onyango aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo hivi karibuni.
Wakiwa nchini, wawili hao wanatarajiwa kupata taarifa ya maendeleo ya mradi wa kuweka nyasi bandia kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza, baada ya FIFA kuipa Tanzania mradi wa nne (GOAL Project 4) wa kuweka miundombinu kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu.
Mwanza ilipata mradi huo baada ya Halmashauri ya Jiji hilo kukubali masharti ya mradi huo ya kulipia nakisi ya fedha zinazolipwa na FIFA, ambazo ni sh. milioni 700. Mradi huo wa kuweka nyasi bandia Nyamagana utagharimu sh. milioni 900, hivyo nakisi y ash. milioni 200 italipiwa na Jiji la Mwanza.
Pia Mamelodi na Onyango watapata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa Gombani uliowekwa nyasi za bandia kwa msaada wa FIFA katika mradi wa GOAL Project 3; na pia kupata mikakati ya maendeleo ya TFF kwa mwaka 2013, ikiwa ni pamoja na kozi na semina mbalimbali zitakazofanyika nchini mwaka huu.
Mamelodi na Onyango pia watapata taarifa ya maendeleo ya uboreshaji wa mashindano ya Copa Coca-Cola baada ya FIFA kuingia rasmi kwenye mashindano hayo mwaka jana kwa kuendesha kozi kwa walimu wa timu za kombaini ya mikoa na waamuzi.
Kwa sasa mashindano hayo yanashirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17, lakini FIFA inataka yahusishe umri mdogo zaidi ili kuendeleza soka ya vijana na kushirikisha kikamilifu shule. Maofisa hao wataondoka nchini Jumatatu asubuhi.

TANZANIA YATINGA KWENYE KUMI BORA NDANI YA LONDON FASHION WEEK

=

 Wabunifu mitindo Jackline Kibacha na Anna Lukindo wakisindikizwa na Mama Balozi Joyce Kallanghe na Mama Rose Kiondo
 Nje ya Jumba la Somerset
 Wanamitindo wa Kitanzania kwenye London Fashion Week 2013. Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha
 Anna, Jack na Duane kutoka Jamaica
 Anna Luks
Mama Rose Kiondo, Samson Soboye, Mama Joyce Kallaghe, Anna Lukindo, Christine Mhando, Jacquline Kibacha
 Barabara ya The Strand copy
London Fashion Week 2013.Picha zote za Urban Pulse
Imeandikwa na Urban Pulse na Freddy Macha

Jumapili mchana  wilaya ya Westminster jijini  London ilikuwa na mashindano ya ubunifu na urembo katika maonyesho  ya kimataifa ya London Fashion Week. Mashindano haya yalifanyika jumba la Somerset lililosimama imara  kwenye upembe wa  kaskazi ya mto Thames.
Maonyesho ya London Fashion Week, bado yanaendelea jumba hili  la Somerset toka tarehe 14 hadi tarehe 28. Wiki hizi mbili nzima zitakutanisha kila mtu anaye husika na biashara ya mavazi na urembo. Magwiji na mapapa wa mitindo, wabunifu, walimbwende, watafuta vipaji, wafanya biashara, wazalishaji mali ghafi na wamiliki viwanda.  Wote hukutana katika maonyesho haya. Hapa si vipaji tu vinavyojionyesha, bali pia watu wa biashara.
Siku hii Tanzania ilikuwa moja ya nchi mbili tu za Kiafrika zilizochaguliwa na British Council na LFW kushiriki kwenye mashindano  ya kutafuta vipaji chipukizi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi na urembo.  Watanzania Anna Lukindo, Jacqueline Kibacha na  Christine Mhando ndio wasanii waliobeba bendera ya taifa letu na kutuwakilisha katika mashindano haya ya kimataifa yanayofanyika kila mwaka kwa zaidi ya miaka 27 sasa.
Katika kuunga mkono maendeleo ya Tanzania na Watanzania,  Ubalozi wetu  Uingereza na Bodi ya Utalii Tanzania, nao pia walichukua nafasi hii kuwasaidia wananchi hawa kufanikisha mahitaji yao ya ushindani. Ubalozi umetoa Ukumbi wa Nyumba Ya Tanzania ulioko Bond Street ili wasanii hao waweze kuonyesha nguo na sanaa zao kwa juma zima kama sheria za London Fashion Week zinavyoamuru. Vile vile Bodi ya Utalii ya Tanzania imesaidia katika mchango  wa mali ghafi zilizotumika katika shughuli hizi  ili kuiuza Tanzania kimataifa.
Mshindi wa tukio alikua Estonia. Ingawa  Tanzania haikuwa mshindi wa mwanzo- ilichaguliwa kati ya Kumi Bora jambo ambalo limetikisa nyoyo na vichwa vya  waandaaji, wabunifu,wafanya biashara na watafuta vipaji vya kimataifa. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa letu kushiriki katika shughuli na  wote wameguswa na kupumbazwa na usanii wa hali ya juu ulioonyeshwa na wasanii  watatu wa Kitanzania.   Lukindo, Mhando na Kibacha wamechukua nafasi waliyopewa kwa mikono miwili na wote wameisogeza Tanzania hatua moja zaidi ndani ya ulingo wa kimataifa na katika biashara hii ya mavazi na urembo ambayo inasemekana ina thamani ya  Pauni Billioni 10  ama  shilingi Trillion 25 za Tanzania.

Thursday, February 21, 2013

Kongamano la nane la Wanahabari na Wadau wa NHIF lafunguliwa leo Mkoani Mtwara

 Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid (kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia (katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Mh. Wilman Kapenjama Ndile (kushoto) wakiwasili kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara leo,tayari kwa ufunguzi wa Kongamano hilo ambalo ni la siku mbili.
Mwenyekiti wa Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),John Bwire akitoa utambuliwa wa Wanahabari waliohudhulia kongamano hilo toka sehemu mbali mbali hapa nchini,linaloendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.
Mgeni Rasmi katika Kongamano la Nane la Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dkt. Seif Rashid akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Benjamin Mkapa uliopo ndani ya Chuo cha Ualimu Mkoani Mtwara.Kauli mbiu ya Kongamano hilo kwa mwaka huu ni “Matumizi Sahihi ya Fedha za Uchangiaji Katika Halmashauri ili kuboresha huduma katika vituo vya matibabu”.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Mh. Joseph Simbakalia akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuhutubia na kufungua Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa yote Nchini,Mh. Abbas Kandoro akitoa salamu kwa Wanahabari na Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wanaoshiriki Kongamano hilo.

Simanzi yatawala, Waziri azomewa


Na: Elias Msuya, Zanzibar 
SIMANZI na vilio vilitawala mazishi ya Padri Evarist Mushi yaliyofanyika Kitope Zanzibar jana huku Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud akipata wakati mgumu baada ya kuzomewa na waombolezaji kutokana na kukerwa na hotuba yake.Padri Mushi aliuawa kwa kupigwa risasi, Jumapili iliyopita wakati akijiandaa kwenda kuongoza misa katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili mjini hapa. Ibada ya mazishi iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ilianza saa nne asubuhi katika Kanisa la Mt. Joseph Minara Miwili na kuhudhuriwa pia na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein. Baada ya misa hiyo iliyomalizika saa 6.30 mchana, msafara wa mazishi ulielekea Kitope yalipo makaburi ya viongozi wa Kanisa Katoliki. Baada ya kufika makaburini, ibada ya mazishi ilianza saa 7.30 mchana na mwili wa Padri uliwekwa kaburini saa moja baadaye. Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa. Waziri Aboud alizomewa kutokana na kauli yake aliyotoa katika salamu za Serikali kuwa kifo cha Padri Mushi ni kazi ya Mungu, ambayo haina makosa. “Serikali imepokea msiba huu kwa
huzuni na masikitiko makubwa. Maumivu ya familia ya marehemu ni maumivu ya Serikali. Padri Mushi ametuachia pengo kubwa lakini kazi ya Mungu haina makosa,” alisema Waziri Aboud kauli ambayo ilipokewa kwa waomboleza kuguna wengine wakizomea hali iliyowafanya baadhi ya viongozi kuwatuliza.
Mmoja wa waombolezaji alisikika akisema: “Kazi ya Mungu ndiyo imewatuma hao wahalifu kuua kwa risasi?”

Mwakilishi wa familia, Francis Mushi alijibu kauli ya waziri huyo alipopewa nafasi ya kutoa salamu kwa kusema: “Tumeupokea msiba huu kwa masikitiko makubwa hasa kwa kuwa Padri hakuugua… Alikuwa kiungo kikubwa katika familia yetu.” Maneno ambayo yaliibua simanzi na vilio kutoka kwa waombolezaji wengi.

Hata Askofu wa Jimbo Katoliki Zanzibar, Augustino Shao aliyekuwa amekaa karibu na Rais Dk Shein alipopewa nafasi naye alisema waziwazi: “Naomba kusema kuwa, kauli hii ya mapenzi ya Mungu haipo… Hili ni suala la uovu na tusikubali kushindwa na uovu.” Kauli hiyo ilionekana kuungwa mkono na waumini.

Ibada hiyo ilihitimishwa kwa sala iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga, Antony Banzi.
Wanasiasa waomboleza
Akizungumza baada ya kumalizika kwa msiba huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema wananchi wamechoshwa na kauli za Serikali za kuwatuliza huku watu wakiendelea kuuawa.

“Watanzania tusiendekeze kauli za Serikali za kila siku, eti Bwana ametoa Bwana ametwaa! Kifo cha Padri Mushi hakikutokana na ugonjwa wala Serikali, lakini haiwezekani kila siku Serikali iendelee na ahadi za maneno matupu.
“Haiwezekani Katibu wa Mufti, Fadhili Soraga ajeruhiwe kwa tindikali, Padri ajeruhiwe kwa risasi, kule Geita mchungaji ameuawa na mwaka jana mwandishi wa habari aliuawa na Jeshi la Polisi, tusidanganyane… tuseme ukweli,” alisema Slaa.

Akizungumzia kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kulitaka Jeshi la Polisi kushirikiana na vyombo vya nje katika upelelezi, alisema: “Suluhisho siyo kuleta ‘Scotland Yard’ hapa, tatizo letu tunashughulika na matawi wakati mzizi ukiwa bado haujakatwa. Tung’oe mzizi wa tatizo.”

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alivilaumu vyombo vya usalama kwa kushindwa kudhibiti mauaji hayo na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwajibika kwa mauaji yanayoendelea nchini.

“Rais anapoingia madarakani anaapa kuwa mtiifu kwa Katiba na raia wake, lakini haya matukio ya umwagaji damu yamekuwa kawaida sasa. Damu ya mtu ni ya thamani huwezi kuinunua hata uwe tajiri.”

Wananchi watakiwa kwenda kutibiwa Hospitali na siyo kwa waganga wa jadi – Mama Salma Kikwete.



 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasili eneo la mkutano wa hadhara, uliofanyika Kata ya Ndoro, Lindi mjini, Feb 20, 2013.
Kina Mama wa Kata ya Ndoro Lindi Mjini, Amina Ali na Saida Ali wakimzawadia kuku, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika, Februari 20, 2013 katika kata hiyo.
 
Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara wa Mama Salma Kikwete, Kata ya Ndoro, Lindi mjini wakishangilia wakati wa mkutano huo.
Wasanii Karim Suleiman ambaye ni mlemavu wa mguu na Mohamed Ali wakionyesha umahiri wao wa kucheza Kiduku katika mkutano wa hadhara uliofanywa na Mama Salma Kikwete kwenye Kata ya Ndoro, Lindi mjini Februari 20, 2013.
Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kuwakabidhi kadi wanachama wapya katika mkutano wa hadhara uliofanyika mtaa wa Matopeni, Lindi mjini Feb 20, 2013. (Picha zote na Bashir Nkoromo).
Na Anna Nkinda, Maelezo  Lindi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa wilaya ya Lindi mjini  kujenga mazoea ya kwenda hospitali kupima afya zao mara kwa  mara na kuachana na tabia ya kwenda kutibiwa kwa waganga wa jadi na kushikana uchawi kutokana na maradhi yanayowasumbua.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais alitoa rai hiyo  jana alipokuwa  akiongea kwa nyakati tofauti na wakazi wa kata za Matopeni na Wailesi zilizopo wilaya ya Lindi mjini wakati wa ziara yake ya kichama ya siku saba katika wilaya ya Lindi mjini ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC.
Aliwasihi watu wenye tabia ya kutopenda kupima afya zao wakati wanaumwa na wale wenye tabia za kukimbilia kwa waganga wa jadi huku wakijua fika kuwa ni wagonjwa waache kwani wanaweza kupoteza maisha kwa magonjwa ambayo wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na kupona.
“Hakuna mtu asiyejua kuwa kuna Ugonjwa wa Ukimwi, muache suala la kushikana uchawi katika hili kwani ugonjwa huu haupatikani kwa kurogwa. Mtu mwenye virusi vya ukimwi  anapimwa  kinga za mwili za kupambana na magonjwa ( CD4) kama zipo chini atapewa dawa za kuongeza na akitumia dawa atakuwa na nguvu na kuweza kufanya kazi zake kama zamani jambo la muhimu asipitishe muda wa kuzitumia” , alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa NEC alisema kuwa jamii nzima inahusika katika ulezi wa watoto lakini jambo la kusikitisha ni kuwa hivi sasa watu wamebadilisha mienendo ya maisha kila mtu anahangaika kulea mwanawe. Na kuwasihi wakazi wa Lindi kufuata maadili ya  zamani ya kuwalea watoto  kwani mtoto wa mwenzako ni wako .
“Ni jukumu la jamii nzima kuwalea watoto wao kwa kufuata  mila za kitanzania , wazazi ambao wakiambiwa kuwa watoto wao wanamienondo mibaya na kuja juu badala ya kuzifanyia kazi taarifa hizo waache tabia hiyo kwani watoto wakilelewa vizuri hata shuleni watakuwa na maadili mazuri na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao”, alisema.
Kuhusu ufanyaji kazi kwa ushirikiano Mama Kikwete aliwataka wananchi hao kuachana na  mambo ya siasa kwani uchaguzi umeshapita hivyo basi wafanye kazi za maendeleo kwa na kujenga tabia ya kujitolea kufanya kazi.
Mama Kikwete alihoji,  “Hawa wazungu manaowaona wanakuja Lindi kufanya kazi wamekuja kujitolea ni jambo la muhimu kujitolea kufanya kazi za maendeleo, ukiambiwa kuna ujenzi wa shule, Zahanati wewe nenda ukajitolee usiseme ile si kazi ya Serikali sasa Serikali ni nani kama si wewe mwananchi?”.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi 2010 – 2015 Diwani wa kata ya Matopeni Suleiman Namkoma alisema kuwa idadi ya watoto wanaoanza darasa la kwanza imeongezeka kutoka 45 hadi 60, kuongezeka kwa ufaulu wa wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba kutoka 20 hadi 43, kuongezeka kwa barabara zinazopitika kipindi cha masika na kiangazi na kuimarika kwa miundombinu na barabara za mifereji.
Namkoma alisema, “Tunakabiliwa na changamoto za uchache wa wataalam wa kada mbalimbali ngazi ya kata na jamii kukosa wataaluma wa huduma stahiki, ukosefu wa uwajibikaji kwa baadhi ya watumishi wa ngazi ya kata, ukosefu wa huduma ya maji safi na salama, kuchelewa kwa ruzuku ya Serikali kuu na makusanyo madogo ya Halmashauri na upungufu wa walimu wa shule ya msingi”.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Mikumbi Zahara Suleiman alisema kuwa katika kata hiyo kuna vikundi vingi vya maendeleo lakini kwa mwaka 2010/2013 hakuna vikundi vilivyokopeshwa na Seambavyo ni  Ayayoli na Mafundi Seremali.
Suleiman alisema, “Tunawashukuru wafadhili waliovikopeshwa baadhi ya vikundi vyetu vya maendeleo kwani  kikundi cha Mwambao Fishing Group kilipewa na Mama Salma Kikwete boti na vifaa vya kuvulia vyenye thamani ya shilini milioni 57  na kikundi cha Uganda kilipewa pesa kutoka MACEP  shilingi milioni 15”.
Katika mkutano wa kata ya Mikumbi   Mjumbe huyo wa NEC aliwapokea vijana 18  waliokuwa wanachama wa CUF na kujiunga  na CCM. Akiwa katika kata za Matopeni, Wailesi  na Mikumbi alikabidhi  kadi  kwa wanachama  wapya wa CCM 43 , Umoja wa vijana 60, Umoja wa Wanawake  22 na Jumuia ya Wazazi  59.

IKULU: Rais Mwai Kibaki awasili nchini kwa Ziara ya Kiserikali (State Visit) ya siku Mbili

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Mwai Kibaki wa Kenya muda mfupi baaada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili.
Rais Mwai kibaki wa Kenya akikaribishwa  kwa maua na Mwanafunzi Tazmina Rasul(6) muda mfupi baada ya kuwasili nchini kwa ziara ya kiserikali (State Visit) ya siku mbili huku mwenyeji wake Rais Dkt.Jakaya Kikwete akiangalia.Picha na IKULU

SIMBA 1 TZ PRISONS 0



KIKOSI CHA SIMBA

MASHABIKI WA SIMBA

KIKISI CHA TZ PRISONS
MASHABIKI WA PRISONS


WAANDISHI WA HABARI


WAANDISHI WENGINE WAKITUMA STORY ZA MCHEZO HUO KWA KUTUMIA SIMU





WAHUSIKA WA UWANJA HUU WA SOKOINE TUNAOMBA BARABARA HII IWE KATIKA HALI  NZURI HASA ZINAPONYESHA MVUA KWANI HAIFAI KABISA 




PICHA NA MBEYA YETU

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...