Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe amesema
uchovu ndiyo sababu iliyomfanya kuugua ghafla jana na kulazwa katika
Hospitali ya Taifa, Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Akiwa
katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,
Edward Lowassa, kuchukua fomu jana, Mbowe aliugua ghafla eneo la
Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili ambako amelazwa
hadi leo.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo
ambaye anawania ubunge katika jimbo la Hai kupitia Chadema
amewahakikisha wanachama na wafuasi wa Ukawa kuwa afya yake ni njema na
huenda akaruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 48.
Akizungumza
na Mwananchi jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminieli Aligaesha
pamoja na kukiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo, hakutaka kuweka hadharani
kilichokuwa kinamsumbua Mbowe. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
MAKAMU wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal amekanusha taarifa za uzushi
ziliposambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anakihama Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Akizungumza jana, Katibu wa Makamu wa Rais, Zahor Mohammed Haji kwa
niaba ya Dk Bilal, alisema taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa aina
yake. Zahoro alisema, Dk Bilal yupo nchini Uingereza katika shughuli za
ujenzi wa taifa na kwamba hana mpango wa kuondoka CCM na wanaoeneza
uzushi huo wana lao jambo.
Katibu huyo amemnukuu Dk Bilal akisema; “Ndugu zangu wa CCM, na
Watanzania kwa ujumla, napenda kuchukua fursa hii kuwa taarifu kwamba
kuna taarifa inayoenezwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo
facebook na whatsApp kuwa nitaitisha mkutano na vyombo vya habari ili
kujitoa CCM.
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara nje ya ofisi ya CCM jana. Picha na Ofisi ya CCM
Waziri wa Ujenzi na
mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu
wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata
ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara
itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa
kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote
za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji
yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe
wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni
lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze
katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa,
kata majimbo, wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja
huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni
wa tsunami,” alisema Dk Magufuli. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vingine
vitatu vya upinzani vinavyounda umoja unaofahamika kwa jina la Ukawa,
Edward Lowassa jana alichukua fomu za kuwania rasmi nafasi hiyo kutoka
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Lowassa, Waziri Mkuu wa zamani aliyejiunga Chadema hivi karibuni
baada ya kushindwa katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi
ya CCM, sasa ameungana na wagombea wengine kujitokeza NEC kuchukua fomu
za kuwania urais.
Ametanguliwa na mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ambaye pia ni Waziri
wa Ujenzi na Mwenyekiti wa UPDP, Fahmi Dovutwa. Wengine ni Mchungaji
Christopher Mtikila wa DP, Mac-Millan Lyimo wa TLP, Hashim Rungwe wa
CHAUMMA, Chifu Lutasola Yemba wa ADC na Dk Godfrey Malisa wa CCK. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Kiongozi
wa mashtaka nchini Burundi amesema kuwa watu kadhaa wanaoshukiwa
kutekeleza mauaji ya jenerali Adolphe Nshimirimana wamekamatwa. Hata hivyo Afisa huyo anasema kuwa viongozi waliopanga njama ya kumua jenerali huyo wangali wanasakwa.
Kufuatia mauaji ya kiongozi huyo wa kikosi
cha ulinzi wa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, Mwanaharakati maarufu
wa haki za kibinaadamu nchini humo alipigwa risasi na kujeruhiwa vibaya
na watu waliokuwa katika pikipiki .
Pierre Claver Mbonimpa alishambuliwa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mapema wiki hii. Mbonimpa amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.
Hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.
Wakati
huohuo taharuki imetanda katika mji mkuu wa Bujumbura baada ya milio ya
risasi kusikika katika maeno kadha ya mji huo usiku wa kuamkia leo.
Hakuna taarifa zaidi ila habari zinasema huenda wanajeshi kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa. Inaelezwa milio hiyo ya risasi ilisikika baada ya gari moja kutoka ofisi ya Rais wa nchi hiyo kuchomwa moto.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu. Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.
Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.
Mbunge wa Bariadi Magharibi,
Andrew Chenge amekiri mbele ya Baraza la Maadili kupokea Sh1.6 bilioni
kutoka Kampuni ya VIP Enginering and Marketing Limited, zikiwa ni malipo
ya kutoa ushauri.
Pia, alihoji kama kuna tatizo kutumia taaluma yake ya sheria kuzishauri kampuni binafsi na kujipatia fedha.
Chenge
ambaye alitoa utetezi wake jana saa 7:30 mchana, alisema hakulipwa
fedha hizo kwa sababu ni kiongozi wa umma, bali kwa kutoa ushauri.
Alisema
aliingia mkataba na kampuni hiyo wa kutoa ushauri wa kisheria dhidi ya
Kampuni ya Mechmer ambazo ni kampuni binafsi zilizokuwa na mgogoro. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akiaga waandishi wa
habari baada ya kuwatangazia kujivua wadhifa huo katika mkutano
alioufanya Dar es Salaam jana.
Hakuna neno jingine linalofaa
kuelezea hali ilivyo ndani ya Ukawa zaidi ya “mtikisiko” baada ya
Profesa Ibrahim Lipumba kuamua kujivua uenyekiti wa Chama cha Wananchi
(CUF) wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kutaka kushika
dola ukiwa umeshika kasi.
Uamuzi wa Profesa Lipumba,
mmoja wa waasisi wanne wa Ukawa-Umoja wa Katiba ya Wananchi unaoundwa na
vyama vinne vya Chadema, CUF, NCCR Mageuzi na NLD-,unamaanisha
anapoteza wadhifa wake wa mwenyekiti mwenza wa umoja huo ambao umeamua
kushirikiana kwenye Uchaguzi Mkuu kwa kusimamisha mgombea mmoja kuanzia
ngazi ya urais hadi udiwani atakayeungwa mkono na vyama hivyo.
Wengine
walioongoza harakati za kuasisi Ukawa ni Freeman Mbowe, ambaye ni
mwenyekiti wa Chadema, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Emmanuel Makaidi
wa NLD. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Miamba ya soka la Ujerumani Bayern Munich wametwaa ubingwa wa michuano ya Audi mwaka 2015.
Bayern wakicheza katika uwanja wao Allianz Arena Jijini Munich, wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya klabu ya Real Madrid ya Hispania.
Bao la ushindi la Bayern lilifungwa Dakika ya 88 na mshambuliaji Robert Lewandowski,alieunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Douglas Costa.
Katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu Tottenham Hotspur waliwachapa AC Milan kwa mabao 2-0 kwa mabao ya Nacer Chadli, Dakika ya 8, na Thomas Carroll, Dakika ya 71.
Klabu ya soka ya Fiorentiana ya Italia imewachapa mabingwa wa ligi ya England Chelsea kwa bao 1-0.
Bao pekee la ushindi la Fiorentina ama maarufu kama Viola liliwekwa kimiani na beki Gonzalo RodrÃguez raia wa Argentina katika Dakika ya 34 baada ya Kipa wa Chelsea Begovic kutema Shuti la Alonso Mendoza.
Mchezo huu ni wa mwisho wa kirafiki kwa klabu ya Chelsea inayonolewa na Kocha Jose Mournho kabla ya kuanza kwa kipute cha ligi kuu ya Engalnd hapo Augusti 8.
Ambapo wataanza utetezi wa ubingwa wao kwa kucheza Mechi yao ya kwanza dhidi ya timu ya Swansea City.
Rais Barack Obama wa Marekani hatimaye amefika nchini Ethiopia katika ziara yake ya pili ya nchi za Afrika.
Ni mara yake ya kwanza tangu aongoze taifa la Marekani akiwa rais kuhutubia wanachama hamsini na mbili wa umoja wa Afrika katika makao makuu yake yaliyoko Addis ababa.
Mazungumzo yao yakiwa yamelenga kutafuta suluhu ya kutokomeza migogoro ya vita za wenyewe kwa wenyewe sudan ya kusini.
Rais Obama, aliwasili nchini Ethiopia akiwa anatokea mjini Nairobi ambako aliwaambia wakenya kuwa amna kikomo cha kile wanachokihitaji na kusisitiza kwa kutoa angalizo katika athari za ukabila na rushwa.
Tamaduni mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia, ndoa za kulazimishwa, tohara kwa watoto wa kike na kutopeleka watoto shuleni.
Bobbi Kristina Brown, mtoto wa marehemu Whitney Houston ambaye alikuwa gwiji wa muziki wa R&B, amefariki dunia baada ya kupoteza fahamu kwa muda wa miezi sita tangu alipokutwa taabani kwenye bafu lake na pindi alipofikishwa hospitalini na kukutwa na matatizo kwenye ubongo.
Bobbi amekufa akiwa na umri wa miaka 22,huku akivutiwa kuwa muigizaji na muimbaji mahiri na mwenye ubora wa aina yake.
Msemaji wa familia Kristen Foster amesema Bobbi amefariki akiwa amezungukwa na familia yake, ''hatimaye yuko salama sasa kwenye mikono ya Mwenyezi Mungu,tunawashukuru wote walioungana nasi katika maombi na kuonesha upendo kwa miezi michache iliyopita''.
Bobbi ambaye alikuwa amepoteza fahamu tangu akutwe ameanguka kwenye bafu lake panapo tarehe 31 januari mwaka huu na kuwekwa kwenye matibabu huku akiwa amekosa ufahamu na mpaka kifo chake kumkuta alikuwa hajapata fahamu bado.
Inakumbukwa kuwa miaka mitatu iliyopita mama yake Bobbi,alikutwa pia kwenye bafu lake amepoteza fahamu baada ya kupitliza kiwango cha dawa za kulevya na pombe mwishowe kufa.
Bobbi alikuwa mtoto pekee wa Whitney Houston na Bobby Brown,magwiji wa muziki wa miondoko ya R &B.
Takriban watu 10 wameuawa kufuatia mlipuko mkubwa uliotokea katika hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.
Mwandishi wa BBC katika mji huo anasema kuwa lori moja lilitumiwa kushambulia hoteli ya Jazeera karibu na uwanja wa ndege wa taifa hilo.
Wajumbe wa kimataifa wamekuwa wakiishi katika hoteli hiyo ambayo imelengwa katika siku za nyuma.
Ripota wetu anasema kuwa ni moja ya mashambulizi mabaya kuwahi kushuhudiwa mjini Mogadishu.
Anasema kuwa magari ya ambulansi yameanza kuokota miili.