YANGA
SC imeirejea historia yake ya kuwatimia makocha wake muda mfupi tu
baada ya kula kichapo kutoka kwa watani zao Simba ambapo tayari uongozi
wa Yanga umelivunja benchi la ufundi la timu hiyo lililokuwa likiongozwa
na makocha Wabrazil,
Marcio Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Neiva na kuwarejesha Mholanzi,
Hans Van der Pluijm na Charles Boniface Mkwasa 'Master'.
Maximo anaondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu Simba SC Jumamosi katika mchezo wa Nani Mtani Jembe, wakati Pluijm anawasili usiku huu na kesho atasaini Mkataba na kuanza kazi. Mkwasa tayari alisaini Mkataba wiki kadhaa zilizopita na ameridhika kufanya kazi chini ya Pluijm tena.
Maximo
na Leonardo walitua Yanga SC Julai mwaka huu kurithi mikoba ya Pluijm
na Mkwasa ambao walipata kazi Uarabuni. Hata hivyo baada ya muda
usiozidi mwezi mmoja, Pluijm na Mkwasa waliacha kazi Uarabuni, wakidai
kukerwa na kuingiliwa na viongozi wa klabu yao katika masuala ya
kiufundi.
Pluijm
alirudi Ghana wakati Mkwasa alirejea nyumbani Tanzania kabla ya
kuajiriwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kama Mkufunzi Mkuu. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.