Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF leo tarehe 31 Januari 2014 limeupa kibali cha kuchezea mashindanoya kimataifa yanayoandaliwa na CAF uwanja wa Azam Complex Chamazi na kuufanya uwanja wa kwanzaunaomilikiwa na klabu Afrika Mashariki kuruhusiwa kuandaa (ku-host) mashindano makubwa ya vilabu
Kwa mujibu wa barua pepe iliyotumwa leo na CAF kupitia kwa naibu mkurugenzi wa mashindano Bwana Khaled
Nassar, Uwanja wa Azam Compex Chamazi umepita vigezo vyote vinavyohitajika na CAF
kuchezewa mashindano ya
kimataifa hivyo kuanzia tarehe ya leo, uwanja huu unaruhusiwa “kuchezewa
mechi za CAF
Bwana Khaled ameandika katika taarifa yake ya barua pepe kwenda TFF na Azam FC kuwa CAF ilimtuma mkaguziwake toka nchini Zimbabwe Bwana Wilfried Mukuna kuja kukagua uwanja huu. Bwana Mukuna aliwasilisha ripoti
CAF iliyopelekea shirikisho hilo kutoa kibali kwa Azam FC na TFF kuruhusiwa kuutumia uwanja huu kwa mechi
zinazoandaliwa na CAF
Uongozi wa Azam FC umetoa
shukrani kwa mkaguzi wa CAF Bwana Mukuna, Uongozi wa TFF chini ya Rais Jamal
Malinzi, na uongozi wa CAF Cairo Misri hasa Bwana Khaled Nasser kwa kuwezesha zoezi hili kufanyika kwa uwazi
na uweledi wa hali ya juu uliopelekea uwanja wetu kupata kibali cha kutumika kwenye michezo ya kimataifa.
Azam FC sasa imewatangazi wapenzi wake kuwa kuanzia msimu huu mechi zake za CAF zitachezwa Azam Complex Chamazi.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz