Tuesday, December 03, 2013

WAATHIRIKA WA VVU MAKETE WASUSA KUNYWA DAWA ZA ARV


Mkuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani katika kata ya Mbalatse wilaya ya Makete 
 Wakazi wa Mbalatse wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Makete akitoa hotuba yake

BOKO HARAM WASHAMBULIA NGOME YA JESHI

Wapiganaji wa Boko Haram

Wapiganaji wa Boko Haram wameshambulia ngome ya Jeshi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali wamesema.

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia mapema asubuhi siku ya jumatatu.

Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.

Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.

Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka 2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.

MAGAZETI YA LEO JUMANNE DESEMBA 03, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

.

.

CHADEMA KIGOMA WATOA TAMKO KUHUSU ZIARA YA DR SLAA NA TISHIO LA USALAMA....!!!



chadema 
Hii ni taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Dec 2 2013 likiwa ni tamko la kikao cha mkoa Chadema Kigoma.
Ni kuhusu Kikao kilichofanyika ofisi ya Mkoa Ujiji kilibeba AGENDA ya Kujadili na Kuboresha ujio wa ziara ya Katibu Mkuu (T) Dr. P. Slaa Mkoani Kigoma 5/12/2013 ambapo atatembelea majimbo yote 8 ya mkoa Kigoma kwa mikutano si chini ya miwili kwa kila jimbo na baadae mkutano wa mwisho, jioni Mkutano ufanyike makao Makuu ya Jimb lengo likiwa ni kuangalia uhai wa chama.
Mambo makuu na muhimu yalizingatiwa ambapo usalama kwa Kiongozi huyo kufutia sakata la Maamuzi ya kamati kuu dhidi ya Mhe.Zitto na mapokeo ya wanachama wetu.
Kutoa taarifa rasmi kwa majimbo na kupokea hali ilivyo au inavyoonekana katika maeneo yao.
Baada ya Tafakuri ya kina na ya Hekima na Busara pevu katika ujio huo iliazimiwa ifuatavyo
 i.Mkoa uliomba Taifa lihairishe na kusogeza mbele tarehe ya ziara hiyo muhimu kwa mkoa wetu ili Mkoa kama ngazi ya chini ya Kanda na Taifa uweze kwenda katika majimbo hayo na kuwaelimisha wanachama na wapenzi wetu juu ya kuheshimu na kuwa na nidhamu na maamuzi yatolewayo na ngazi ya juu yetu hata kama yanamaumivu ….katiba ifuatwe katika kutatua tatizo – Maoni ya Wengi Mkoani na Viongozi wa Chama ni kuudhiwa na maamuzi ya k/kuu ambayo dhahiri yalilenga Zitto – Kisiasa.
ii.  Mkoa ulitishika na vitisho baada ya kupokea taarifa toka kwa baadhi ya viongozi wa majimbo ya mkoa kwamba hali ya usalama si nzuri kwa ujio wa kiongozi Dr. Slaa kufika Kigoma kwa kipindi hiki wakati wanachama na wapenzi wakitafakari na kwa kauli tofauti zisizolenga kuwepo usalama.
 iii.           Kwa hekima ya kikao kilijiridhisha kwa kupata maoni toka katika majimbo 6 kuwa hali ni mbaya kabisa wakishauri Katibu mkuu asogeze mbele ziara yake kupisha mtafaruku huu na kwa usalama wa Chadema na viongozi wake Kitaifa.
iv.          Hivyo Mkoa kupitia kikao hicho ikaonekana ni bora kuzuia kuliko kutibu, tayari sintofahamu zimeonekana, viongozi na hasa wa majimbo kutofautiana mitazamo ni HATARI katika hali hiyo, mkoa ulijiridhisha usalama hautakuwepo kwa ujumla hata kama baadhi ya majimbo yakisema wao wapo salama tu.
v.            HOFU/TAHADHARI -   Endapo hali haitokuwa salama Mungu apishe mbali.
Mkoa hautokwepa lawama na uzembe wa makusudi kwani wajibu wa ngazi ya chini ni kutoa ushauri kwa ngazi ya juu hivyo mkoa unatoa ushauri kwa Makao Makuu (T) Chadema kusogeza mbele ziara hiyo hadi hali itulie na mkoa upite majimboni kujiridhisha na usalama kwa viongozi wake na hasa wa Taifa.
 LENGO KUU:   NI KUHAKIKISHA CHADEMA TUNAPITA SALAMA KATIKA WAKATI HUU MGUMU KWETU – CHADEMA
 ALHAJ. JAFARI KASISIKO                                           MSAFIRI WAMALWA
M/KITI MKOA                        01/DEC.2013                KATIBU MKOA

Monday, December 02, 2013

MKUU WA MKOA WA MOROGORO MH. JOEL BENDERA NA NAIBU WAZIRI MEDEYE WATUNUKIWA PHD YA HESHIMA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia) mara baada ya kumtunukisha Shahada ya Uzamivu ya Heshima ( PhD) katika Masuala ya Falsafa ya Jamii ya Chuo Kikuu cha Califonia State Christian kilichopo nchini Marekani, kwa mamlaka aliyopewa na Bodi cha Chuo Kikuu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akivishwa kofia ya udaktari wa Heshima .
Naibu Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Dk Joel Goodluck Ole Medeye ( kushoto) akipongezwa na Makamu wa Rais na Mkurugenzi wa Mahusiano wa Masuala yote ya Afrika ya Kielimu ambaye pia ni Kamishina wa Tume ya Haki za Binadamu yenye kutetea matatizo ya Haki za Binadamu Kimataifa , Profesa Edward Lazaro Nasioki, ( kulia).kati kati kati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Innocent Kalongeris.

TABIA ZA MSICHANA ANAYEKUPENDA KIMAPENZI LAKINI HAWEZI KUSEMA

1. Atakutega kupata attention yako. Hufanya mambo ambayo yatamfanya kuona kama unampenda au lah! Mf wa mambo hayo ni kujifanya anaumwa na kuangalia respond yako kwake ni kiasi gani unamjali na kiasi gani utahangaika kwa ajili yake au
2. Haoni aibu kugusa sehemu yako ya mwili. Msichana anayependa haoni aibu kukushika mkono ama kukutomosa au hata kukumbatia. Kwa kufanya hivyo hujua kuwa kwa asilimia kubwa hisia za kushikana kwenu kutamrahisishia kazi ya kuwa na wewe

3. Kucheka kwa nguvu hata kwa kitu kisicho chekesha endapo wewe umezungumza. Mara nyingi ataonesha uso wa furaha hata kama si furaha ya kweli

4. Wivu.
Hujisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Ukiwa unachart nao na ukiwaita majina ya kimahaba. Hapendi.

5 anakumbuka siku zako muhimu. Hukumbuka kama vile siku yako ya kuzaliwa hatowez kuisahau kufanya ipite bila kukutakia heri ya siku ya kuzaliwa kama sivyo ukifaulu mtihani au chochote katika maisha yako atakuwa mbele kukupongeza

6. Eye contact anapenda kukuangalia machoni muda wote ambao mtakuwa mkizungumza pamoja akidhani kuwa utaelewa ni kiais gani anakupenda kupitia vile ambavyo anakuangalia.
Ila wengine huona aibu kuwatazama wavulana wanaowapenda si wote wana ujasiri wa kuwatazama wapenzi wao.

7. Hupenda kukaa mmuda mwingi na wewe. Hawezi kupoteza hata sekunde ukimuhitaji kwa mazungumzo. Anajisikia furaha kukaa na wewe muda mrefu bila kuchoka. Anaweza akaacha kila kitu anachokifanya ili ajumuike na wewe.

8. Yupo tayari kuangamiza. Kama msichana anakupenda yupo tayari kusacrifice. Ni kitu ambacho hakuna mtu ambaye anaweza akafanya kwa mtu mwingine. Utaona vipi huyo msichana alivyo kwako na wa wengine. Yaani yupo tayari yeye akose lakini wewe upate na kwa mwingine anaweza akamwamba hana alichoombwa lakini akakupa wewe kama pesa na vitu vingine.

9. Anachukulia matatizo yako kama ni yake. Unapomueleza kuwa ana tatizo anajali tatizo lako kama vile ni lake na hujisikia vibaya sana na kuhuzunika na atafanya lolote ili aweze kukusaidia utoke katika hilo tatizo.

10. Mikwaruzano ikitokea katika urafiki wenu hayupo tayari kukupoteza kabla hajakuambia anakupenda. Kwa kuwa anakupenda endapo ikatokea mikwaruzano basi atafanya juu chini kuyaweka mambo sawa ili asikukose

UZINDUZI WA AZAM TV HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA...!!!

Mambo yalikuwa kama hivi kwenye uzinduzi wa Azam TV jijini Dar..
Mtangazaji wa Televisheni ya Azam TV Wasiwasi Mwabulambo akiwa kwenye Red Carpet kabla ya mahojiano na Mkurugeni wa Kajunason Blog Cathbert Angelo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa METL na Mbunge wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji alikuwa ni miongoni mwa wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Azam TV. Pichani akifanya mahojiano na Mtangazaji wa Azam TV Wasiwasi Mwambulambo.

HUYU NDIYE JOSEPH OMOG KOCHA MPYA AZAM FC


 Kocha mpya wa Azam FC Joseph Omog akiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Ndugu Said Mohammed.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU DESEMBA 02, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.


WANAWAKE WENGINE WANASWA NA DAWA ZA KULEVYA KIA ...!!!

Jeshi la Polisi  Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), linawashikilia wanawake wawili ambao ni wafanyabiashara wa kigeni kwa tuhuma za kukutwa wakisafirisha kilo 12.7 za dawa za kulevya maarufu kama 'unga'.

Hilo ni tukio la pili katika muda usiozidi siku saba kwa raia wa kigeni kukamatwa na dawa hizo katika uwanja huo, ikiwa ni wiki mbili  tangu Waziri wa Uchukuzi, Dk.

Harrison Mwakyembe, atishie kuwafukuza kazi maofisa wa idara za usalama watakaobainika kujihusisha na biashara hiyo  kupitishwa katika uwanja huo.


Watuhumiwa hao waliokamatwa ni jana alfajiri katika uwanja huo ni Josiane Dede Creppy (25), raia wa Togo na Grace Teta (34), raia wa Liberia ambao kwa nyakati tofauti, mmoja akijiandaa kuelekea jijini Accra, Ghana na mwingine nchini Afrika Kusini.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, aliiambia NIPASHE jana kwamba mtuhumiwa  Grace alikamatwa akiwa na kilo 10.5 za dawa hizo wakati  akisafiri kwa ndege ya Shirika la Precision Air kutoka KIA kwenda Captown nchini Afrika Kusini kupitia Nairobi, Kenya.

“Huyu alikamatwa na unga unaoaminika kuwa ni dawa za kulevya alfajiri ya saa 10:45 akitumia hati ya kusafiria yenye namba 1039080 ikimuonyesha ni mfanyabiashara na raia wa Liberia. Josiane    alikamatwa saa 8:50 alfajiri akiwa na kilo 2.2 za dawa hiyo akiwa anataka kuondoka na ndege ya Shirika la Ethiopia kelekea Ghana,” alisema Kamanda Boaz

Sunday, December 01, 2013

CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA


UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi; Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea. Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya; 1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

CHADEMA YAZIDI KUPUKUTIKA .... KATIBU WA WILAYA CHADEMA AJIUNGA NA CCM

 Katibu wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya, Bwa. Bryson Mwasimba akionesha kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya kuachia ngazi, kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. 
Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama, kukagua miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha CCM, Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya, Bwa. Bryson Mwasimba aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM, huku umati mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa mayowe na miluzi, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 Bwa. Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
 Bwa. Bryson Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo. CHANZO MICHUZI JR

MH. ZITTO AELEZA MAMBO YANAYOMMALIZA KISIASA...!!!


Zitto-Kabwe_46197.jpg
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.
"Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, .... nadhani hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto... wanajua siwezi kusemea nje maana sina kinga..., hivyo wanataka kuniondoa bungeni..." alisema.

Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika kipindi chake chote cha kisiasa.
Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 01, 2013

.
.



Saturday, November 30, 2013

MPANGO WA SARAFU MOJA WA EAC KUJADILIWA LEO JIJINI KAMPALA

 Wakuu wa Nchi Tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo Novemba 30, wanatarajiwa kutia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa EAC, Richard Owora aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa kuwa sherehe za kutia saini mkataba huo utakaoanzisha mchakato wa miaka kumi hadi kufikia lengo la kuwa na sarafu moja ya EAC, zitafanyika katika Viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Marais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya wanatarajiwa kuwa jijini hapa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi za EAC.
Umoja wa sarafu ni moja kati ya mambo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC. Masuala mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imesainiwa na kuanza kutekelezwa, ingawa kwa kasi isiyotosheleza kutokana na vikwazo kadhaa.
Hatua ya mwisho na juu kabisa katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni shirikisho la kisiasa linalolenga kuwa na nchi moja, hatua itakayozihakikishia nchi za ukanda huo nguvu ya soko, biashara, majadiliano na uamuzi katika ngazi ya ndani na kimataifa.
Huu ni mkutano wa kwanza kuwakutanisha wakuu wote wa EAC tangu kuibuka kwa migongano ya kimawazo na mtazamo miongoni mwao kuhusu utekelezaji wa makubaliano na miradi iliyo katika mipango ya EAC pamoja na njia bora na sahihi ya kumaliza vita na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya baadhi ya nchi wanachama.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...