Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umesema hautahusika na malipo ya matibabu kwa wanachama wao watakaoathirika na utumiaji wa dawa za kuongeza maumbile.
Akizungumza
kwenye kongamano la wadau wa mfuko huo mkoani hapa hivi karibuni, Kaimu
Mkurugenzi Tiba na Ushauri wa NHIF, Dk Mkwabi Fikirini alisema mfuko
hautatoa huduma kwa mwanachama aliyeathirika na dawa za kuongeza
maumbile ambazo zimepigwa marufuku na Serikali.
Dk
Fikirini alisema mfuko huo unatoa huduma ya matibabu kwa wanachama wake,
ila hauhusiki na waathirika wa dawa zilizopigwa marufuku na Serikali
ikiwamo za kuongeza maumbile maarufu kama dawa za Kichina.