Siku
moja baada ya wabunge kuwataka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Waziri wa
Maliasili na Utalii, Khamis Kagasheki kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia
Operesheni Tokomeza Ujangili, pembe 706 za ndovu zimekamatwa jijini Dar
es Salaam.
Serikali ya Pakistan imetoa taarifa
kulaani vikali mashambulizi ambayo Marekani inafanya kwa kutumia ndege
zisizo na rubani, ikisema kuwa mashambulizi kama hayo yanakiuka uhuru wa
taifa hilo.
Shambulizi hilo lililofanywa siku ya Ijumaa, lililenga gari la Mehsud.
Afisaa mmoja mkuu wa ujasusi nchini
Marekani, aliambia shirika la habari la Associated Press kuwa Marekani
ilipokea taarifa muhimu kuthibitisha kifo cha Mehsoud.
Hata hivyo msemaji wa baraza la
usalama wa kitaifa la Marekani, alisema kuwa hawawezi kuthibitisha
taarifa hizo lakini ikiwa ni kweli basi ni pigo kubwa sana kwa Taliban.
Hakimullah Mehsud alijulikana sana
mwaka 2007 kama kamanda wa mwasisi wa kundi hilo Baitullah Mehsud,
alipowakamata wanajeshi 300 wa Pakistani .