Saturday, November 02, 2013

JELA MAISHA KWA UBAKAJI

kana_mbakaji_512x288_bbc_nocredit_fc7c2.jpg
Johannes alikiri kumbaka Anene lakini alikanusha madai ya kumuua
Mwanamume mmoja nchini Afrika Kusini aliyepatikana na hatia ya ubakaji na mauaji ya msichana mwenye umri wa miaka 17 amepewa hukumu mbili za maisha jela na mahakama moja viungani mwa mji wa Cape Town.
Viongozi wa mashitaka walitaka mshukiwa Johannes Kana afungwe jela maisha bila dhamana.
Marehemu Anene Booysen alifariki mwezi Februari , masaa kadhaa baada ya kuuawa kinyama katika kesi ambayo imewaghadhabisha wengi.
Afrika Kusini ni nchi mojawapo yenye visa vingi vya ukatili wa kijinsia duniani.
Mwandishi wa BBC Nomsa Maseko aliyefika katika mahakama ya Swellendam, umbali wa kilomita 220 kutoka mji wa Cape Town, anasema kuwa mjombake Kana alishanga kwa kupiga makofi na hata kuangua kicheko jaji alipotoa uamuzi wake.
" Hiki ni kichekesho ," alisema huku akiongeza kuwa mfumo wa sheria hauna haki
Lakini wengi waliohudhuria kesi hiyo walihisi kama haki imetendeka
Bi Booysen alitendewa ukatili na mwili wake kutupwa karibu na nyumba yake Bredasdorp lakini alifariki baadaye hospitalini mjini Cape Town
Wakati huohuo, Rais Jacob Zuma alitaja mauaji hayo kama ya kushtua na ya kinyama.
Ametoa wito kwa majaji kutoa adhabu kali sana kwa wanaofanya vitendo vya uhalifu wa kijinsia.
Wakati wa kesi dhidi ya Kana, madaktari waliomtibu Bi Booysen walisema kuwa majereha aliyoyapata yalikuwa mabaya zaidi kwake kuwahi kuyashuhudia.
Kabla ya kifo chake alisema kuwa karibu wanaume watano au sita walihusika na shambulizi dhidi yake , lakini washukiwa watatu walikamatwa baadae ingawa ni mmoja tu aliyehukumiwa.
Kana alikiri kosa la ubakaji ingawa alikana kuwa alimuua.

Friday, November 01, 2013

YANGA SC YAIPIGA JKT 4-0


3_17e1c.jpg
Ngassa alifunga bao la kwanza kwa shuti kali la umbali wa mita 20, baada ya kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa JKT Ruvu, wakati bao la pili alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kurushwa na beki Mbuyu Twite.
Pamoja na kumaliza dakika 45 za kwanza wakiwa nyuma kwa 2-0, lakini JKT Ruvu ndiyo waliocheza soka ya kuvutia ya pasi za hapa na pale, huku Yanga wakitumia mashambulizi ya haraka kwa mabeki kupeleka mipira pembeni, ambako mawinga wanatia krosi washambuliaji wagombanie goli.
Kipindi cha pili, Yanga SC waliendelea na staili yao kushambulia kutokea pembeni, huku JKT Ruvu wakionekana kuanza kupoteza mwelekeo na kutoa mwanya zaidi wa kushambuliwa.
Beki Oscar Joshua aliipatia Yanga bao la tatu dakika ya pili ya kipindi cha pili, akiunganisha kona maridadi iliyochongwa na kiungo Simon Msuva.

Kona hiyo ilitokana na kazi nzuri ya kipa wa JKT Ruvu, Sadick Mecks aliyepangua shuti kali la kiungo wa Yanga, Frank Domayo.

VIWANGO VIPYA VYA ALAMA ZA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI HIVI HAPA.....!!!


a_97eff.jpg
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalasesa.
b_3754b.jpg
_ Baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome (hayupo pichani).
c_5b2ab.jpg
Waandishi wa habari na maafisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome(hayupo pichani).
Picha zote na Eliphace Marwa (MAELEZO)
UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU
UTANGULIZI
Wizara imekusanya maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika Mitihani ya Kuhitimu Kidato cha Nne na cha Sita pamoja na Matumizi ya Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment ama CA) kwa ajili ya kuamua kiwango cha ufaulu wa mwanafunzi.

MUGABE ANAWZA 'KUTUSIWA' AU KUKOSOLEWA

120927121136_mugabe_un_304x171_reuters_nocredit_35956.jpg
Mahakama ya kikatiba nchini Zimbabwe imebatilisha sheria inayosema kuwa ni uhalifu kumtusi Rais wa nchi.
''Viongozi wa mashitaka hawapaswi kuwa na tamaa sana ya kuwashitaki watu wanaomkosoa Rais Mugabe katika kumbi za ulevi na maeneo mengine ya kijamii,'' iliamua mahakama ya kikatiba.
Angalau watu 80 wameshitakiwa chini ya sheria hiyo katika miaka ya hivi karibuni.
Mnamo mwezi Mei, mwanaharakati Solomon Madzore alikamatwa baada ya kudaiwa kumuita Mugabe 'Punda anayechechemaa.'
Alikanusha kosa la kumtusi Rais.
Chini ya kifungu cha 33 cha sheria ya uhalifu nchini Zimbabwe, mtu anaweza kufungwa jela hadi mwaka mmoja au kutozwa faini ya dola 100 kwa kumtusi Rais.
Sheria hiyo ilipingwa na watu kadha nchini humo akiwemo mkaazi mmoja wa mji wa Bulawayo Kusini mwa nchi, Tendai Danga, aliyekamatwa miaka miwili iliyopita kwa madai ya kumtusi Mugabe wakati alipozozana na polisi ndani ya baa.
Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC mjini Harare, Brian Hungwe, majaji tisa waliotoa uamuzi huo, walikubaliana kwa kauli moja kuwa sheria hiyo inahujumu uhuru wa kujieleza na kuifanya vigumu kwa serikali kukata rufaa dhidi ya uamuzi wao.
Hata hivyo, mahakama hiyo ilimpa waziri wa sheria, Emmerson Mnangagwa hadi tarehe 20 Novemba kukata rufaa.
Mwezi Agosti mahakama ilimwachilia huru mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 26 Takura Mufumisi, aliyeshitakiwa kwa kuwa na nia ya kutumia bango la karatasi lenye picha ya Mugabe kama karatasi ya kujipangusia chooni ndani ya baa moja.
Katika kura ya maamuzi iliyofanyika mwezi Machi, wananchi walipitisha katiba mpya ambayo inawapa uhuru zaidi wa kujieleza.
Watu wengi wamepongeza uamuzi wa mahakama wakiamini kuwa sheria ilikuwa imemlinda rais dhidi ya kukosolewa.

MAMA RWAKATARE ATENGWA NA MAKANISA KWASABABU YA KUFUNGISHA NDOA YA MBUNGE ALIYEOLEWA NA KIJANA MDOGO...!!!


MBUNGE wa Viti Maalumu, Mchungaji Getrude Rwakatare (CCM) wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Mikocheni B, jijini Dar es Salaam, ametengwa katika Ushirikiano wa Makanisa baada ya kanisa lake kulalamikiwa kufungisha ndoa inayodaiwa kukiuka taratibu za kikanisa, kisheria na kimaadili, Tanzania Daima Jumatano limejulishwa.Ndoa inayolalamikiwa kufungishwa na kanisa hilo ni ile iliyoibuliwa na gazeti hili wiki iliyopita ambayo inamhusisha Mbunge  wa Viti Maalumu, Rosweeter Kasikila (CCM) mwenye umri wa miaka 60 na kijana Michael Christian wa miaka  26.


Ndoa hiyo ambayo ilifungwa katika kanisa hilo Septemba Mosi mwaka 2011, imebaki kuwa gumzo na kuwaacha hoi baadhi ya mawaziri, wabunge pamoja na majirani wanaoishi jirani na mbunge huyo mjini Bagamoyo, Pwani.
Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na Haki za Jamii ya makanisa hayo, Mchungaji William Mwamalanga, alisema uamuzi wa kulitenga kanisa la Mama Rwakatare umetokana na kikao cha Kamati ya Maadili iliyokutana jana jijiji Dar es Salaam.

LULU MICHAEL AMWAGA MATUSI YA NGUONI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU....!!!


  Elizabeth Michael ‘Lulu’.

MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.
Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).

TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.

MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).

Thursday, October 31, 2013

WAPINZANI KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA 2015

mbatia-k1 596f0
UPEPO wa mabadiliko ya kisiasa unaovuma kuelekea kambi ya upinzani, sasa unaonekana kuwaamsha viongozi wa vyama hivyo baada ya kutolewa kwa taarifa kuwa wanafikiria kusimamisha mgombea mmoja wa urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.


Taarifa zilizolifikia gazeti hili kabla ya kuthibitishwa na mmoja wa viongozi hao, zilieleza kuwa hatua ya vyama hivyo imekuja baada ya ushirika wao waliouunda kupinga upungufu uliokuwemo kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kuzaa matunda.
Pamoja na hilo, inaelezwa kuwa maamuzi hayo magumu ya wapinzani yametiwa chachu na kauli aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete ya hivi karibuni ya kukitabiria anguko Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi wa mwaka 2015 au ule wa 2020, kutokana na kile alichodai kuwa viongozi wa chama hicho kuendekeza rushwa.
Mmoja wa viongozi wanaounda ushirika huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia alithibitisha taarifa hizo huku akisisitiza kuwa nia ya kufanya hivyo ni kuhakikisha wanaiondoa madarakani CCM mwaka 2015.
Kwa mujibu wa Mbatia, walichokifanya kwenye Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba si nguvu ya soda na badala yake wataendeleza hadi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

ANGALIA PICHA ZA MAZISHI YA BABA YAKE WEMA SEPETU YALIYOONGOZWA NA RAIS WA ZANZIBAR DR ALI MOHAMMED SHEIN



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akiuaga Mwili wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani, Mnazi mmoja Mjini Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimpa pole Mjane wa Marehemu Balozi Isaac Sepetu,Mama Miriam Sepetu,alipofika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani,Mnazi mmoja Mjini Unguja, kuuaga mwili wa Marehemu.
Ibada ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Sepetu  ikiendelea kwenye Kanisa la Minara Miwili Zanzibar
Baadhi ya watoto wa marehemu Balozi Sepetu wakisikiliza neno la mungu
Wema Sepetu(Aliyesimama Kushoto) akiwa kanisani kwenye maombezi ya baba yake mzazi 

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS OKTOBA 31, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.

Q-CHILA "NIMEOTESHWA NDOTO YA USHINDI KUWA PAPII KOCHA ATARUDI URAIANI"

Muimbaji wa Beautiful, Q-Chilla amesema ameota ndoto kuwa Papii Kocha na baba yake Nguza Viking aka Babu Seya wataachiwa huru.

Leo, Jumatano, jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania limeipitia upya hukumu yao.

“Nimeota ndoto ya ushindi, nimemuona Papii Kocha Sinza anakatiza barabara. Naotaga mara chache sana na huwa vitu vinatokea. Iko wazi kaka yangu anarudi uraiani. Nimemuona, welcome home, dunia ilikumiss, vita imekwisha,” Q-Chilla ameimbia Bongo5.

“Let the world know that the beloved kid is coming home.”

Katika rufaa hiyo leo wakili wa Babu Seya na Papii Kocha ameiomba mahakama hiyo ifute ushahidi na waachiwe huru lakini serikali imepinga. Kutokana na hatua hiyo, leo mahakama ya rufaa haijafanya uamuzi wowote imewapiga kalenda.

Nguza Viking na Papii Kocha wanatumikia kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto wadogo wa shule ya msingi.

Wednesday, October 30, 2013

KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZ​I WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

PIX 1 f3694
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto) akimpokea Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi cha siku tatu kinachofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. 
Katika Hotuba yake ya ufunguzi, Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo.
PIX 2 8e6ee
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza na wajumbe wa baraza hilo kabla ya kufungua kikao cha siku tatu kinaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. 
Wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Edson Nyinyimbe. 
Wa pili kushoto ni Venance Ntiyalundura, Katibu wa tawi hilo. Katika kikao hicho Ntunguja aliwaomba watendaji wakuu wa wizara hiyo washirikiane vizuri na watumishi wao ili kuleta mafanikio zaidi ndani ya wizara hiyo.
PIX 3 abd9f
Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariam Ntunguja (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba ya kufungua mkutano wa wafanyakazi wa siku tatu unaofanyika katika Hoteli ya Paradise jijini Mbeya. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WEMA SEPETU AFUNGUKA JINSI BABA YAKE ALIVYOTESEKA MPAKA MAUTI ILIPOMCHUKUA

Staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu akielezea kuhusu msiba wa baba yake mzazi Balozi Abraham Isaac Sepetu alipoongea na GLOBAL TV. Balozi Sepetu alifariki asubuhi ya Jumapili Oktoba 27, 2013 katika hospitali ya TMJ jijini Dar na mwili wake jana nyumbani kwake Sinza-Mori jijini Dar es Salaam tayari kwa mazishi yatakayofanyika leoVisiwani Zanzibar.

Tuesday, October 29, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMANNE OKTOBA 29, 2013

.
.
.

ASKARI ALIYEUAWA DRC ALIKUWA MBIONI KUFUNGA NDOA DESEMBA



Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), aliyeuawa kwa kupigwa risasi kwenye mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani, katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (Monusco), Luteni Rajab Ahmed Mlima, alikuwa katika hatua za mwisho za kufunga ndoa.

Askari huyo aliuawa katika  uwanja wa mapambano na vikosi vya wapiganaji wa Kundi la Waasi la M23, katika Milima ya Gavana, karibu na Goma, DRC- Congo wakati akitekeleza jukumu la ulinzi wa amani

Akizungumza na gazeti hili, kaka wa marehemu Dk Aziz Mlima, alisema kuwa ndugu yake alikuwa tayari amekamilisha mipango yote na kilichokuwa kikisubiriwa ni siku ya kufunga ndoa hiyo.

“ Alikuwa yuko mbioni kufunga ndoa, lakini kwa sasa sitapenda kutaja jina la mchumba wake kwa kuwahayupo hapa lakini naye ni askari,” alisema Dk Mlima.

MWIGAMBA AZIDI KUANIKA MADUDU YA CHADEMA


*Awaonya wanaomwita msaliti
*Dk. Slaa aibua mapya

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, aliyesimamishwa uongozi asema atakichafua chama hicho kama ataendelea kuitwa msaliti.

Hatua hiyo, imekuja baada ya Mwigamba kukiri hadharani kusambaza waraka unaowatuhumu viongozi wa chama hicho katika mtandao wa Jamii Forum (JF), akitumia jina la Maskini Mkulima. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Arusha jana, Mwigamba aliwaonya viongozi wa Chadema wanaomwita msaliti. 
 
Alisema kama wanataka awe msaliti, yupo tayari kumwaga mambo yote hadharani, tena kwa ushahidi usio na shaka hata kidogo.

Mwigamba, aliyejiunga na Chadema mwaka 2004, akiwa mwanachama wa kawaida, alisema akiwa makao makuu mjini Dar es Salaam kama mhasibu mkuu wa chama, ndipo alipoanza kutambua udhaifu mkubwa wa kiuongozi ndani ya chama chake.

“Niliondoka pale makao makuu kwa mizengwe, kiongozi mmoja mkubwa kabisa alinifukuza kazi kwa kunipigia simu, tena baada ya kuwasiliana na Mkurugenzi wa Fedha,Anthony Komu akiwa nje ya Dar es Salaam na kumwagiza anifukuze,” alisema Mwigamba.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...