JAMAL Emil Malinzi, usiku
huu ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kupata
kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye
ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa
kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib
Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
Huyu ndiye Rais wenu mpya TFF; Rais
aliyemaliza muda wake TFF, Leodegar Tenga kushoto akimtambulisha Jamal
Malinzi kuliakuwa Rais mpya wa shirikisho hilo usiku nwa kuamkia leo
ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam
Katika nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13;
kiungo wa zamani wa Simba SC Wilfred Kidau amepata kura 60 na kuwashinda
Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura
nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davisa Mosha aliyepata kura 54.
Kanda ya 11 Geoffrey Nyange
'Kaburu' amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir
Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya
10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba
akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Mhagama
aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya
nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.
Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi
aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati
Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. Eley
Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63,
amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano
aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha
Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo
Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.