Nape Moses Nnauye,
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala
mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua
uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa
Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf
Himid ni pamoja na:-
1.
Kushindwa
kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.
Kushindwa
kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.
Kuikana
Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma
dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)
imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa
kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor
Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.