Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Monday, August 26, 2013
MSICHANA AMEJIKUTA AKIZOMEWA NA KUCHAPWA VIBOKO BAADA YA KUVAA NGUO FUPI...!!!
Msichana mmoja ambaye jina lake halikujulika amejikukuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na kuchapwa viboko na kundi la watu katika eneo la soko la nmc jiji arusha kwa madai ya kuvaa nguo fupi hali iliyowalazimu wasamariawema kuingilia kati na kutumia nguvu kubwa ili kumwokoa na kumsitili kwa kumfunika na nguo zingine.
Mwandishi wetu Halfani Lihundi
kutoka arusha alikuwapo katika sakata hilo na ametuma taarifa hii
iliyosema, watu walio shuhudia tukio hilo wamesema wamechukizwa na aina
ya nguo alizizovaa msichana huyo ambazo haziendani na maadili ya
Kitanzania, ndiyo maana wameamua kumwadabisha ili kukomesha tabia hiyo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Kwa upande wao wanawake waliyo msitili msichana
huyo kwa kumpa nguo za heshima na kumhifadhi katika Gareji ya jirani
kabla ya
kumkimbiza kwa gari aina ya Toyota Hiace wamesema hawaridhishwi na tabia
hiyo inayowazalilisha wanawake na kuwataka wasichana kuavaa nguo za
kujisitili ili kujenga heshima katika jamii.
Source ITV
AHUBIRI ZAIDI YA MASAA MATATU BILA WAUMINI...!!!
Mhubiri wa injili akitoa neno pembeni ni viti kwa ajili ya waumini japo hakuna aliyejitokeza.
...Akizidi kumwaga injili.
...Akielezea umuhimu wa kumtukuza bwana.
CHAZ BABA AFUNGA NDOA, ATINGA UKUMBI WA ‘TWANGA’ KUJINAFASI AKIWA PEKE YAKE
Rehema akikubali kuolewa na Chaz.
Chaz akimvisha pete mkewe.
CCM KWAWAKA MOTO MMOJA ATIMULIWA UANACHAMA
Nape Moses Nnauye,
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya
Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyomalizika leo imejadili kwa kina Masuala
mbalimbali likiwemo pendekezo la Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi - Zanzibar la kumvua
uanachama Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa
Kiembesamaki.
Baadhi ya tuhuma za Ndugu Mansoor Yussuf
Himid ni pamoja na:-
1.
Kushindwa
kusimamia malengo ya CCM na kutekeleza masharti ya uanachama.
2.
Kushindwa
kutekeleza wajibu wa mwanachama na kukiuka Maadili ya Kiongozi wa CCM.
3.
Kuikana
Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010-2015 na kuisaliti CCM.
Baada ya kujiridhisha vya kutosha na tuhuma
dhidi ya Ndugu Mansoor Yussuf Himid, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)
imeridhia uamuzi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Magharibi Zanzibar wa
kumfukuza uanachama. Kwa uamuzi huo wa kumvua uanachama wa CCM Ndugu Mansoor
Yussuf Himid, yeye kwa sasa sio Kiongozi tena wa CCM.
Imetolewa na:
Nape Moses Nnauye,
KATIBU
WA NEC ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
26/08/2013
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
DILLISH TOKA NAMIBIA AIBUKA MSHINDI WA BIG BROTHER AFRICA 2013
Fainali za Big Brother zimefikia tamati usiku huu zikiwa na washiriki watano ambao ni Beverly, Melvin, Cleo, Elikem na Dillish.
Mshiriki wa kwanza kutolewa alikuwa ni Beverly akifuatiwa na Melvin huku Elikem akiwa ni mshiriki wa tatu kutolewa..
Mchujo huo uliwafanya Cleo na Dillish waingie katika masaa ya fainali za mwisho ambapo Cleo alielemewa na kutolewa huku akimwacha Dillish akichekelea $300,000 za ushindi wa shindano hilo....
Agalia jinsi kura zilivyopigwa:
Angola: Dillish
Botswana: Cleo
Ghana: Elikem
Kenya: Dillish
Ethiopia: Beverly
Malawi: Cleo
Namibia: Dillish
Nigeria: Melvin
South Africa: Cleo
Sierra Leone: Elikem
Tanzania: Dillish
Uganda: Dillish
Zambia: Cleo
Zimbabwe: Elikem
Rest of Africa: Melvin
Total:
Dillish = 5, Cleo = 4, Elikem = 3, Melvin = 2, Beverly = 1.
Hongera sana Dillish
TANGAZO LA USAILI NAFASI ZA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA
TANGAZO TANGAZO TANGAZO TANGAZO
KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA DIWANI ATHUMANI – ACP ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE YA KUWA ORODHA YA
MAJINA YA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 NA CHA SITA MWAKA 2013
NA KUCHAGULIWA KUFANYA USAILI WA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI INAPATIKANA KWENYE
TOVUTI YA POLISI www.policeforce.go.tz.
MUHIMU.
i.
MWOMBAJI ANARUHUSIWA KUFANYA USAILI
KWENYE KITUO CHOCHOTE CHA USAILI KILICHO KARIBU NAE KULINGANA NA TAREHE
ZINAVYOONYESHA KWENYE TANGAZO LA USAILI.
ii.
KWA MKOA WA MBEYA NA IRINGA KITUO CHAO
NI MBEYA NA USAILI UTAFANYIKA KUANZIA TAREHE 16/09/2013 HADI 19/9/2013 SAA
2:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KATIKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
iii.
MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI
AJE NA VYETI VYOTE VYA MASOMO(ACADEMIC
CERTIFICATES),RESULTS SLIP(S) NA LEAVING CERTIFICATE(S), NAKALA HALISI YA
CHETI CHA KUZALIWA(ORIGINAL BIRTH CERTIFICATE). HATI YA KIAPO CHA
KUZALIWA HAITAKUBALIWA.
iv.
MWOMBAJI AWE NA NANMBA YA SIMU
AMBAYO ITAMJULISHA ENDAPO ATAKUBALIWA.
v.
KILA MWOMBAJI ALIYEITWA KWENYE USAILI
ATAJIGHARAMIA USAFIRI, CHAKULA, NA MALAZI KWA MUDA WOTE WA ZOEZI LA USAILI.
NI MUHIMU SANA KILA MWOMBAJI
KUZINGATIA MUDA WA KUANZA USAILI.
Saturday, August 24, 2013
KUWA WAKWANZA KUSIKILIZA NA KUDOWNLOAD WIMBO WA MSANII MPYA WA HIP HOP CHATTA RYMES KUTOKA SHY TOWN
Ujio mpya katika mziki wa kizazi kipya katika miondoko ya
hiphop.. Anaitwa ISSA ALLY a.k.a CHATTA
RYMES ni kijana mdogo mwenye uwezo wa
kushangaza katika mziki Anakuja na wimbo wake mpya aliofanya na KING DIZZO unaitwa SEMA NAO
ameufanyia katika Studio za SHY TOWN REC
pande za SHINYANGA Tz
Kwa muonekano ni mdogo lakini kiuandishi ni hatari sana na
anaplan ndefu ya kuhakikisha mziki unaweza kumlipa na kumfanya aendeshe maisha
yake kupitia mziki na hatimae kuitangaza Tanzania kimataifa zaidi.
SUPORT YAKO NDIO ANAYOIHITAJI
ARTIST: Chatta Rymes Ft King Dizzo
TRACK:Sema nao
STUDIO:Shy Town Recs
PRODUCER: Hance Q
Friday, August 23, 2013
MADAM RITA: "NAY WA MITEGO HANA PESA ZA KUNILIPA HATA NIKIMFUNGULIA KESI"
Mratibu wa shindano la Epic Bongo Star Search(EBSS) Rita Paulsen (Madam Rita ) ameshangazwa na taarifa zilizoenea katika vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii ,kuhusiana na yeye kutaka kumfungulia mashtaka msanii Nay Wa Mitego ambaye anadaiwa kumchafua (defamation) katika wimbo wake mpya unaotamba sasa (Salamu Zao). Amesema hana mpango
wa kumfungulia mashitaka kwa kuwa hatakuwa na pesa za kumlipa kwa maana itakuwa kesi ya kumchafua na inaweza kumgharimu pesa nyingi.
.
Madam Rita ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha burudani cha The Strengo Saturday kinachorushwa na Radio Victoria fm kupitia 90.6 kilichopo Musoma, Mara. Ambapo mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale alitaka kujua sababu kubwa ya EBSS kuhamishiwa katika kituo cha televisheni cha TBC1 ikitokea ITV na vipi kuhusiana na habari zilizopo za yeye (Madam Rita) kutaka kumfungulia Nay Wa Mitego kesi ya kumchafua .
JK AAPISHA MAKATIBU WAKUU NA NAIBU MAKATIBU WAKUU IKULU DAR ES SALAAM LEO
Rais Jakaya Kikwete na Katibu
Mkuu Kiongozi Mhe Ombeni Sefue wakiwa katika picha ya pamoja na
watumishi wa ofisi ya Sekretariate ya Baraza la Mawaziri ambako
watumishi wake wawili wameteuliwa kuwa manaibu Makatibu wakuu, ambao ni
Injinia Angelina Madete (kulia kwa Rais) na Mhe. Consolata Mgimba
(kushoto kwa Rais) mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu
Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa
Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu
wapya mara baada ya kuapishwa Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu
Ikulu jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa
Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue katika picha ya pamoja na Makatibu wakuu wapya mara baada ya
kuapishwa Makatibu wakuu hao na Manaibu Katibu wakuu Ikulu jijini Dar es
salaam leo.
HIKI NDICHO KILICHOMPONZA LULU MPAKA FILAMU YAKE YA FOOLISH AGE KUPIGWA STOP
Bodi ya ukaguzi wa filamu na michezo ya
kuigiza nchini imeipiga stop filamu ya Foolish age ya msanii wa kike
mwenye mvuto Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ baada ya kukuta picha zilizo
nje ya maadili ya Kitanzania katika filamu hiyo, filamu hiyo ambayo
ilipanga kuzinduliwa mwezi huu tarehe 30 katika ukumbi wa Mlimani City
inahitaji marekebisho.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.
Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.
Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.
Kikwazo kilichoikumba filamu hiyo ni nguo fupi zilizotumika katika waigizaji walioshiriki katika filamu hiyo ambayo inatabiriwa kufanya vizuri katika soko la filamu Bongo kama itafanikiwa kuzinduliwa na kuingia sokoni, juhudi zinafanyika kuhakikisha kuwa marekebisho yanafanyika ili kwenda na ratiba kama ilivyopangwa.
Hivi sasa baada ya urasimishaji wa filamu mamlaka na taasisi zinazohusika na masuala ya filamu zimekuwa makini na kuhakikisha kuwa filamu zinazoingia sokoni na zile zinazozinduliwa kukaguliwa kabla ya kufanyika kwa matukio hayo kama ilivyokuwa awali, kama filamu hiyo ya Foolish age itashindwa vigezo vya madaraja yanayotolewa na Bodi hiyo haitaonyeshwa.
Lulu ndio mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2013 kupitia tamasha la filamu la kimataifa la ZIFF katika kipengere cha tuzo za Bongo movie kilichopewa jina la Zuku Bongo movie Awards zilizotolewa katika ukumbi wa Ngome Kongwe.
TFF: YANGA WAMEONGEZA ADHABU YA MRISHO NGASSA
Mrisho Ngassa.
Na Khatimu NahekaIMEFAHAMIKA kuwa Klabu ya Yanga, ndiyo iliyochangia ukubwa wa adhabu aliyopewa kiungo wake mshambuliaji Mrisho Ngassa, Championi Ijumaa limebaini.
Taarifa hiyo inakuja wakati ambao Ngassa amefungiwa kucheza mechi sita za mashindano pamoja na kuilipa Simba jumla ya shilingi milioni 45, sababu kubwa ikiwa ni kusaini mikataba miwili, ule wa Yanga na ule wa Simba.
Boniface Wambura ambaye ni Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ameliambia Championi Ijumaa kuwa, adhabu ya kufungiwa michezo sita kwa Ngassa imewekwa maalum, kutokana na Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji kutaka mchezaji huyo apate uchungu wa makosa aliyoyafanya na siyo kutegemea kulipiwa na klabu.
Wambura alisema adhabu hiyo imetokana na kasumba ya klabu mbalimbali ambazo zimekuwa zikiamua kulipa faini wanazokatwa wachezaji wao kwa makosa mbalimbali, maamuzi ambayo yanasababisha wachezaji kurudia makosa hayo.
Subscribe to:
Posts (Atom)