Siku tano baada ya raia wawili wa Uingereza kumwagiwa tindikali visiwani Zanzibar, Serikali kupitia vyombo vyake vya uchunguzi imeibuka na kueleza kuwa bila wananchi kutoa taarifa za ushahidi wa uhalifu wa aina mbalimbali, ni vigumu kuwabaini wahusika. (HM)
Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja jana
na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, Mkemia Mkuu wa
Serikali, Profesa Samwel Manyele na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali
(DPP) Eliezer Feleshi, katika mkutano wao na waandishi wa habari,
uliolenga kueleza mikakati ya kupambana na matumizi yasiyo sahihi ya
tindikali nchini.
Katika ufafanuzi wao walisema, "Kutoa taarifa ya uhalifu wa jambo lolote siyo hiari, ni jukumu la kisheria na kikatiba," huku Feleshi akitolea mfano jinsi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk Steven Ulimboka alivyoshindwa kutoa ushahidi wa tukio lililomkuta la kutekwa, kupigwa na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, hivyo kufanya uchunguzi kuwa mgumu.