Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepo
na mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayo www.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html
Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayoinamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.

Matapeli
hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa
Mtanzania yeyotemwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip
a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA
WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE
TOVUTI HIYO.
Kwa
taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na
Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama
ambavyo inadai.
IMETOLEWA NA
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013
IDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKI
BENKI KUU
YA TANZANIA
DAR ES SALAAM.
29/5/2013