Wednesday, May 29, 2013

Justin Bieber matatani tena,majirani wamtuhumu kuvuta bangi mbele ya watoto na kupiga kelele ovyo usiku wa manane


Siku chache baada ya kuondoa stress za mahusiano ya mapenzi juu ya Selena Gomez ‘The Beauty and beat singer’ Justin Bieber amekumbana na matatizo mengine ambayo yanaweza kuwa makubwa zaidi ya stress alizokuwa nazo, baada ya kuwa kero kwa majirani zake ambao wanajuta kukaa karibu na staa huyo kwa kuwa tabia zake zimeuharibu utulivu uliokuwepo katika ujirani huo huko Los Angeles.

Majirani hao wameiambia TMZ kuwa Bieber na marafiki zake wamekuwa wakisababisha kelele nyingi usiku wa manane wanaporudi kutoka viwanja na kuendesha gari lake aina ya Ferrari kwa fujo na wakati mwingine pikipiki yake, lakini pia hata wakifikika nyumbani huendeleza party huku wakiachia sauti juu na kuwanyima usingizi majirani hao.

Majirani hao walisema mida ya mchana Bieber hupita na gari lake taratibu mbele ya watoto wadogo huku akivuta marijuana a.k.a bangi waziwazi, na kwamba siku moja mwimbaji huyo alikuwa anaendesha akiwa na rafiki yake ambae pia alikuwa anavuta bangi.

Walisema hata bodi ya mmiliki wa nyumba hizo imewaambia majirani hao kuwa amepanga kuripoti polisi suala hilo kwa kuwa ni swala la kiharifu na linalovunja haki za msingi za majirani hao. Majirani hao pia wamesharipoti polisi tayari na polisi wamepanga kuzuia uendeshaji magari mida ya usiku sana katika maeneo hayo ili kuondoa kero hizo.

Mkasa huu uliompata wa kuchukiwa na majirani zake unaweza kufanana kidogo na ule wa Chris Brown kushtakiwa na majirani zake kwa kuwa alichora michoro iliyosemekana kuwatishia watoto wao. Lakini hii ya Bieber kuvuta marijuana mbele ya watoto wao itakuwa imetisha zaidi.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...