Huu
Wimbo Ameimba Producer wa mziki anayejulikana kwa jina la Mswaki
Kutoka Studio ya Black Curtains....Ameimba kama Marehemu Ngwear Akiimba
baada ya Kifo chake...Sikiliza Hapa chini: Big up Sana Mswaki
Katika
upekuzi wetu leo hii tuliweza kupata moja ya chat za mwisho mwisho ya
marehemu Albert Mangwea akiwa afrika ya kusini na mwanadada wa bongo
movies Wema sepetu. Katika maongezi hayo Ngwea alikuwa anapanga Kumtumia
mwadadada mwingine wa bongo movies Kajala Masanja kwenye video yake
mpya aliyokuwa anajiandaa kuifanya. Maongezi yao yalikuwa hivi.
Mangwea : kuku bandani..
Mangwea : Nataka Kajala…
Mangwea : Sikiza nyimbo then utanipa idea..
Mangwea : Nataka tukipiga hela kwa bro…
Mangwea : Tulipe na hela ya ticket ya Jux aje toka China tumalize huku kusini
Mangwea : #hugs
Wema Sepetu : Upo api?
Mangwea: Me nipo Pretoria now momo…
(Angalia screen shot ya maongezi hayo pichani)
Dah, inasikitisha sana. Maisha ya Msanii huyu yaliyokatika mapema. Mungu ailaze roho marehemu mahali pema peponi.
Mamlaka
ya Mawasilino Tanzania, TCRA, imesema watumiaji wa simu ambazo
hazikusajiliwa, watakatiwa mawasiliano ifikapo Juni Mosi mwaka huu.
Tamko
hilo lilitolewa jijiji Mbeya na Mkurugenzi wa Sheria na Leseni wa
mamlaka hiyo, Elizabeth Nziga wakati wa semina kuhusu utekelezaji wa
sheria mpya ya mawasiliano ya elektroniki na posta ya mwaka 2010 kwa
wadau mbalimbali.
Hiyo
ni awamu nyingine katika mipango ya TCRA, kwani awali ilikuwa na
kampeni za kuzima mitambo ya analogia nchi nzima na kuwataka wananchi
kuingia katika mfumo wa dijitali ulioanzia katika Mkoa wa Dar es Salaam
Desemba 31, mwaka jana.
Mikoa
mingine iliyoingia kwenye mfumo wa dijitali ni Arusha, Tanga, Dodoma,
Mbeya na Mwanza. Nziga alisema mamlaka hiyo inasisitiza kuwa hatua hiyo
ni utekelezaji wa makubaliano kati yake na watoa huduma za mawasilino ya
simu na kufikia usiku wa Juni Mosi, namba za simu ambazo hazikusajiliwa
zitakoma. Mmiliki wake hataweza kuitumia kupiga wala kupokea siku.
Alisema
kuwa ni muda mrefu umepita ambao ulitolewa kwa ajili ya kusajili namba
za simu lakini watu wengi hawakuweza kufanya hivyo kwa wakati na badala
yake wamekuwa wakitumia simu vibaya ikiwa ni pamoja na kufanya uhalifu
na kutoa lugha chafu.
Katika hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Abbas Kandoro, ilisema vyombo vya mawasiliano vimesaidia kukua kwa sekta mbalimbali
Siku
chache baada ya kuondoa stress za mahusiano ya mapenzi juu ya Selena
Gomez ‘The Beauty and beat singer’ Justin Bieber amekumbana na matatizo
mengine ambayo yanaweza kuwa makubwa zaidi ya stress alizokuwa nazo,
baada ya kuwa kero kwa majirani zake ambao wanajuta kukaa karibu na staa
huyo kwa kuwa tabia zake zimeuharibu utulivu uliokuwepo katika ujirani
huo huko Los Angeles.
Majirani hao wameiambia TMZ kuwa Bieber na
marafiki zake wamekuwa wakisababisha kelele nyingi usiku wa manane
wanaporudi kutoka viwanja na kuendesha gari lake aina ya Ferrari kwa
fujo na wakati mwingine pikipiki yake, lakini pia hata wakifikika
nyumbani huendeleza party huku wakiachia sauti juu na kuwanyima usingizi
majirani hao.
Majirani hao walisema mida ya mchana Bieber hupita
na gari lake taratibu mbele ya watoto wadogo huku akivuta marijuana
a.k.a bangi waziwazi, na kwamba siku moja mwimbaji huyo alikuwa
anaendesha akiwa na rafiki yake ambae pia alikuwa anavuta bangi.
Walisema
hata bodi ya mmiliki wa nyumba hizo imewaambia majirani hao kuwa
amepanga kuripoti polisi suala hilo kwa kuwa ni swala la kiharifu na
linalovunja haki za msingi za majirani hao. Majirani hao pia
wamesharipoti polisi tayari na polisi wamepanga kuzuia uendeshaji magari
mida ya usiku sana katika maeneo hayo ili kuondoa kero hizo.
Mkasa
huu uliompata wa kuchukiwa na majirani zake unaweza kufanana kidogo na
ule wa Chris Brown kushtakiwa na majirani zake kwa kuwa alichora michoro
iliyosemekana kuwatishia watoto wao. Lakini hii ya Bieber kuvuta
marijuana mbele ya watoto wao itakuwa imetisha zaidi.
The
Medical report from Helen Joseph hospital,Dr Shirley Radcliffe
confirming that albert Mangwairdied from “alcohol toxicity” after
drinking toomuch,Over-exhaustion and drugs overdose....The inquest heard
that Albert 28, collapsed in the his friends home had been more
thanfive-times the legal S.A drink-drive limit with 416mgof alcohol per
100 millilitres of blood in hissystem....
Radcliffe
described thereasons for ICU admission included hypoxemia and one of
his friend found “two empty vodka bottles[found] on the Car” and he
hadbeen suffering from the eating disorder Bulimiafor several months
before his death and endless partying session with little or no
resting...sample taken from his stomach showed poly-drug cocktail and he
overdosed Heroin,Cocaine 'crack' and cannabis 0.08gms was also found in
his blood...and his death was caused by massive heart attack and
respiratory failure followed by sudden Heart stop...and end up dead
within seconds! R.I.P Mangwear!
JINA
LAKE HALISI NI ALBERT KENETH MANGWAIR,NI MTU WA RUVUMA
MNGONI...,,,,MNGONI,LAKINI ALIZALIWA MBEYA TAREHE 16 NOVEMBER,MWAKA
1982.YEYE NI MTOTO WA MWISHO KWAO,KWA BABA AKIWA MTOTO WA 10,KWA MAMA
AKIWA MTOTO WA 6.
NGWAIR
ASILI YAKE NI RUVUMA,YAANI MNGONI, ALIZALIWA MBEYA,A KIWA MIAKA 5
WALIHAMIA MOROGORO AKASOMA SHULE YA MSINGI BUNGO HADI DARASA LA 5,BABA
YAKE AKAPATA UHAMISHO AKAHAMIA DODOMA,SO AKAHAMA NA BABA YAKE AKAENDA
AKAMALIZA SHULE YA MSINGI MLIMWA DODOMA.BAAADAE MAZENGO SEC,THEN CHUO
CHA UFUNDI MAZENGO
Muda
mfupi uliopita nilipokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo
anajulikana kwa jina la P Funk Majani na kuniomba nipokee msg hii hapa
chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.
Baba
Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi,
amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa
Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika
Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi
Beach.
Ingawa
bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo
amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake
alizikwa.
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu.
Kuhusu
mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema
kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna
ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na
ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.
Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.
VIDEO Queen wa Bongo Fleva, Agness Jerald ‘Masogange’
anasumbuliwa na tatizo la kuota ndoto mbaya usiku na kuamka kisha
kutoka nje na kutimua mbio, jambo ambalo kwa wengi linaweza kuonekana
kuwa ni maajabu.
Agness Jerald ‘Masogange’.
Habari kutoka kwa sosi wetu, zinasema kuwa katikati ya wiki iliyopita,
Masogange akiwa ndotoni, aliamka na kufungua milango na geti la nje
kisha kutimua mbio umbali mrefu akiwa na nguo za kulalia na miguuni
hana viatu.
“Bahati nzuri ni kwamba, wakati anahangaika
kufungua geti, rafiki yake aliyekuwa amelala naye alishtuka na kushangaa
kukuta milango iko wazi. Alipotoka nje, akakuta Masogange ndiyo
anamalizia kufungua geti kubwa na kuanza kukimbia hivyo akamkimbiza,”
kilieleza chanzo chetu. Akaongeza: “Lakini pia aliwapigia simu
marafiki zake wengine na kuwajulisha juu ya tukio hilo, maana mwenyewe
ilikuwa mara ya kwanza kumuona katika hali hiyo.” MASOGANGE ANASEMAJE? Risasi
Mchanganyiko kama ilivyo kawaida yake ya kutokukurupuka, lilimsaka
Masogange kwa simu na kufanikiwa ambapo alithibitisha tukio hilo na
kufafanua kwamba liliwahi kumtesa kwa muda mrefu huko nyuma, likaisha.
“Ilikuwa
hatari sana lakini namshukuru rafiki yangu kwa kunisaidia. Unajua hili
tatizo liliwahi kunitesa sana wakati nikiwa mdogo lakini nilikwenda
Mbeya nikapewa dawa tatizo likapotea kabisa hadi juzi liliporudi tena,”
alisema.
Akiongea kupitia kipindi cha Amplifire cha Clouds FM, kutoka mkoani
Morogoro, mama mzazi wa msanii Albert Mangwair aliyefariki dunia leo
akiwa nchini Afrika Kusini, amesema kuwa mara ya mwisho kuwasiliana na
marehemu ilikuwa wiki mbili zilizopita ambapo Mangwair alimwambia kuwa
mzima na anaendelea vizuri na kwamba angerejea nchini Ijumaa iliyopita.
Aliongeza kuwa taarifa za kifo cha mwanaye amezipata jioni hii kwa
masikitiko. Wakati Mangwair anaelekea Afrika Kusini hakumuaga mama yake
japo akiwa huko alikuwa anawasiliana naye. Kuhusu taarifa za mazishi
mama Mangwair amesema bado anasubiri shemeji zake wafike ili wapange.
Mungu ampumzishe Mangwair mahali pema peponi. Amen!