Sunday, May 26, 2013

MAPACHA WATANO WALIOZALIWA WAKATI MMOJA WAFARIKI DUNIA

 Mwalimu Sofia Mgaya akiwa amelala na watoto wake wote watano  kitandani baada ya kujifungua
...............................................................................
Na Nathan Mtega,Songea

 WATOTO watano waliozaliwa kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kwa wakati mmoja kwa mwanamke aliyejulikana kwa jina la Sophia Mgaya(28) mkazi wa Ruhuwiko mjini Songea mkoani Ruvuma wamefariki dunia baada ya kuishi hai kwa muda wa masaa kumi.
 Akizungumza kwa njia  ya simu mganga mkuu mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma Dkt Benedict Ngaiza alisema kuwa watoto hao watano ambao walizaliwa kwa njia ya upasuaji wakiwa na umri wa miezi nane tofauti na inavyotakiwa  umri wa mtoto kuzaliwa kuwa ni miezi tisa.

DIAMOND ATOA SIRI YA MUZIKI WAKE....!!!


Mengi yamekuwa yakisemwa juu ya msanii ambae inaaminika ndiye mfalme wa muziki wa bongo fleva Wapo wanaosema anatumia nguvu za giza ikiwemo ushirikina na wapo wanaosema yuko powered na Imani ya Free mason ingawa TEENTZ tunaamini juhudi na kujituma ndiyo njia pekee ya mafanikio kwa chochote TEENTZ ilipiga story na Diamond na kueleza moja ya sababu kubwa why yuko juu na  na kila siku ananendelea kuwa juu tofauti na baadhi ya wanamzki wengine


1-"Mungu ndio kila kitu kwa maisha ya binadamu,so napenda kumtanguliza Mungu kwa kila nikifanyacho"
2-"Sipendi starehe,kutumia pesa vibaya,naiheshimu sana pesa yangu,matumizi yake makubwa ni chakula,pengine mafuta kwa ajili ya gari matumizi mengine ya mhimu kwa binadamu na zaidi naitumia pesa yangu kufanya kitu kitakachoendelea kumantain muziki wangu"

3"-Sibani pesa kwenye swala la kujijenga kimziki,niko tayali nitumie milioni kadhaa kufanya kitu kitakachojenga status yangu vizuri,mfano kugharamikia mavazi ya shows n.k"

VIKONGWE WATATU WACHINJWA KAMA KUKU NA KUCHOMWA MOTO

Matukio kama haya ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwauwa wenzao kwa kuwachoma moto yamekithiri katika jamii na ndiyo yaliyosababisha ajuza watatu kuuwawa kikatili usiku wa kuamkia leo huko Bunda, Mara

MAUAJI ya kikatili yametokea usiku wa kuamkia leo wilayani Bunda, mkoani Mara baada ya watu wenye hasira wa kijiji cha Kasaula kuwauwa kwa kuwachinja kama Kuku kisha kuwachoma moto ajuza watatu kwa kuwatuhumu wanajihusisha na vitendo vya kishirikina.
Pia watu hao mbali na kuwaua kikatili vibibi hivyo kwa tuhuma kwamba walimuua kijana mmoja aitwaye Sale Ligolo, walichoma moto na kuteketeza nyumba walizokuwa wakiishi wazee hao pamoja na kupora kuku waliokuwa wakiwafuga na kuatafuna kumaliza hasira zao.
Kwa mujibu wa wa taarifa ya mwandishi Masau Bwire aliyepo Bunda kwa sasa, tukio hilo limetokea usiku wa kumakia leo baada ya watu hao wenye hasira kuwasaka ajuza hao baada ya kuwepo tuhuma kwamba walishirikiana kumuua kijana huyo hivi karibuni.

Saturday, May 25, 2013

LADY JAY DEE NAYE AMSHANGAA MWANA FA. KUTOKANA NAYE KUANDAA SHOW TAREHE MOJA NA KUAMUA KUMCHUKUA LINNAH.

Kutokana na JIDE kuwa na show yake kubwa mnamo tarehe 31 mwezi huu pale nyumbani lounge ,Sasa rafikiye wa karibu sana MwanaFA inaonyesha naye ameanda show yake siku hiyohiyo  ya Tarehe 31,Zaidi ya yote mwana FA akawachukua  wasanii walio jitoa katika show ya JIDE kama Linnah  sa kutokana na sitofahamu hiyo mtandao huu wa thechoicetz uliweza kumtafuta JIDE kupitia twitter na kumuu liza juu ya hili swala naye aliweza kutoa yake anayo yafikiria,pia mtandao huu wa thechoicetz ulimtafuta  MwanaFA lakini mwanaFA hakuweza kutujibu swali tulilo muuliza hadi muda huu
 

Hivi ndivyo jide ALIVYO TUJIBU


MUONEKANO MPYA WA WEMA SEPETU HUU HAPA.....!!!


  
Huu ndio muonekano mpya wa bidada Wema, Vipi mzuri au mbaya? Comment

"MWANAMKE MCHAWI ADONDOKEA KANISANI AKIWA NA BIBLIA MKONONI, WAUMINI WAHAHA, YEYE MWENYEWE ANENA MAZITO "...!!

Wakati Mtwara kukilipuka kwa vurugu za gesi na kusababisha maafa, jijini Dar kumeibuka taharuki ya aina yake baada ya mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Anna kudaiwa kuwa ni mchawi na kudondokea kanisani.


Tukio hilo lililochukua saa kadhaa lilitokea katika Kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi na Uponyaji linaloongozwa na Nabii Flora Peter lililopo Mbezi Beach Salasala, Dar hivi karibuni.
Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni waumini wa kanisa hilo inadai kuwa mwanamke huyo, mkazi wa Bunju, Dar alifika kanisani hapo saa 4:45 asubuhi huku akiwa amebeba Biblia na pochi lake akionekana kuwa sawa waumini wengine.

Baada ya Mahakama Kumruhusu Dr. Slaa Kuoa, Ridhiwani Kikwete Amponda Facebook







What is your Take ? Je ni kweli ni discussion ya Kidini ama ?

Picha za mwanasheria aliyebambwa akifanya ukahaba. Ashitaki mawakili kwa kusambaza picha zake za uchi


Mwanasheria mmoja wa Illinois ambaye alipatikana na hatia ya kufanya ngono na mwanaume mmoja kwa malipo ya Dola za Marekani 100 anamshitaki aliyekuwa wakili wake wa utetezi na mawakili wengine wawili kwa madai ya kusambaza picha zake za utupu.

Reema Bajaj, mwenye miaka 27, anasema wakili wake wa zamani Timothy Johnson, mwendesha mashitaka wa zamani Calvin Campbell, na mwanasheria aliyeorodheshwa kwenye hati ya mashitaka kama ‘John Doe’ walitoa hadharani picha zake za siri sambamba na taarifa kumhusu yeye.

Huyu Ndio Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania kwenye BBA “The Chase”

 
 

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kwenye mitandao mbalimbali nchini Tanzania, mrembo huyu, mwanamuziki Feza Kessy, ndiye atakayeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2013 (BBA “The Chase.” Well, hizi ni baadhi ya picha zake. Get familiar

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 25, 2013 HARD NEWS, UDAKU ,MICHEZO NA BURUDANI

.
.
.

MTOTO ALIYEZALIWA JELA AREJEA NA KUMTOA MAMA YAKE GEREZANI...!!!


 
Kanhaiya Kumari (kushoto) akiwa na mama yake, Vijaya mara baada ya kuachiwa huyu.

Mtoto mdogo wa kiume wa mwanamke ambaye amedhoofika  jela kwa takribani miaka 20 nchini India kwa upungufu wa Pauni za Uingereza 119 katika pesa za dhamana hatimaye amehakikisha kuachiliwa huru kwa mama yake. 


Kanhaiya Kumari, mwenye umri wa miaka 19, alizaliwa ndani ya gereza na Vijaya, mwenye miaka 48, ambaye alikamatwa mwaka 1993 kwa kuhusiana na kesi inayohusisha mauaji ya mmoja wa majirani zake katika wilaya ya Aligarh nchini India.


Alipatiwa dhamana mwaka 1994 lakini - ilitupwa na mumewe - hakuwa na uwezo wa kulipa Rupia 10,000 iliyokuwa ikihitajika kuhakikisha uhuru wake. Sasa ameungana tena na mtoto wake wa kiume, baada ya mtoto huyo kuwa amefanya kazi kupata pesa hizo za dhamana na kuishawishi Mahakama Kuu kwa ajili ya kuachiliwa mama yake.

KIONGOZI WA VURUGU ZA MTWARA AKAMATWA......!!!

vujo mtwara

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                     Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                    Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                           S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                        DAR ES SALAAM.
24 MAY 2013
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi Nchini linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi kwa tuhuma za kueneza ujumbe wa uchochezi na chuki kwa wananchi na viongozi wa serikali kwa njia ya simu ya mkononi akituma SMS kwa lengo la kuchochea fujo, vurugu na kutoa matusi kwa viongozi hao.

MWANAFUNZI WA CHUO APIGA PICHA YA "UTUPU" ILI AFANANE NA RIHANNA...!!!

Huyu ni mwanafunzi wa chuo(jina kapuni) aliyehamua kupiga picha ya utupu ili afanane na Rihanna Katika pozi...

Mwanafunzi Huyu ambaye yeye Binafsi anapenda kujifananisha na mwanamuziki asiyeishiwa na skendo Rihanna alifikia uhamuzi wa kujimulika na kamera na hatimaye kuficha....Ila ckuzote maovu ayajifichi.....

Picha hii ilisambaa mitandaoni hasa ya kijamii na hatimaye mdau wetu alitutonya na tukaipata...

Sio mbaya kama umefanana na mwanamuziki fulani ......ILA pia sio sahihi kuiga kila kitu ambacho mwanamuziki huyo anafanya...Kwa mtazamo tuu

TUNAJIFUNZA NINI...
Je ni sahii Kujimulika na katika picha za utupu ili tuuuu ujione umekamika na kufanana na mwanamuziki fulani........?

TANGAZO MUHIMU KUTOKA KWA JESHI LA WANANCHI TANZANIA(JWTZ) KWA WANANCHI WOTE...!!

 " Mtanzania yeyote: kaa makini usiokote kitu chochote ambacho una mashaka nacho, kuna bomu zimerushwa toka nchi jirani Malawi zaidi ya 30 zenye uzito usiopungua tani 100. Hivyo basi uonapo kitu kipo kama chupa la chai chenye rangi ya fedha "usikiguse" piga namba 0756000042. SMS hii tuma kwa watu uwezavyo: Imetolewa na JWTZ/ LSL5CAMRM: Asante. "
 Source: http://williammalecela.blogspot.com

Friday, May 24, 2013

ASILIMIA 31 YA WATANZANIA NI WALEVI

Asilimia 26.8 hadi asilimia 31.9 ya Watanzania wanatumia pombe na asilimia 27.4 kati ya hao ambao ni wanaume na wengine asilimia 13.4 ambao ni wanawake, ni walevi wa kupindukia. Bunge lilielezwa jana.


Takwimu hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid, ambaye alisema kuwa viwango hivyo vimetokana na utafiti uliofanywa kati ya Februari hadi Oktoba mwaka jana 2012.

Kwa mujibu wa naibu waziri, utafiti huo ulifanywa na Shirika la Afya Duniani (WHO).
Alikuwa akijibu swali la Abdallah Haji Ali (Kiwani–CUF) aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu utumiaji wa pombe ambao umethibitika kuwa ni hatari kwa afya za binadamu.
Pia alipendekeza pombe ipigwe marufuku kabisa hapa nchini kwa kuzingatia madhara yake.

Naibu waziri alisema tafiti zimeonyesha kuwa watu milioni mbili wanafariki dunia kila mwaka duniani kutokana na madhara ya matumizi ya pombe na asilimia nne ya matatizo ya kiafya yanatokana na matumizi ya pombe.
“Hali inazidi kuwa mbaya zaidi katika nchi zinazoendelea hasa kutokana na kukabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi na ustawi wa jamii inayochangiwa na magonjwa ya malaria, kifua kikuu na Ukimwi,” alisema Dk Rashid.

Naibu Waziri alisema kutokana na kuongezeka kwa athari zitokanazo na matumizi ya pombe hasa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza, Serikali inatekeleza mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya kuambukizwa unaoelekeza kutoa elimu kwa wananchi kupitia njia mbalimbali.
Kuhusu mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo, alisema tayari Serikali imeanza utaratibu wa kuziwezesha hospitali za rufaa za mikoa, kuanza kutoa huduma kwa waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya na pombe.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...